PICHA: Majengo marefu zaidi Duniani, Jengo la kwanza lipo Dubai(UAE), China yaongoza kuwa na majengo mengi marefu Duniani


Mwifwa

Mwifwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2017
Messages
31,483
Points
2,000
Age
19
Mwifwa

Mwifwa

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2017
31,483 2,000
Katika pitapita zangu mitandaoni, nikapita forum kubwa zaidi Dunia(Skyscraper City forum) nikakutana na uzi katika miongoni mwa sub forum huko ukizungumzia majengo marefu katika miji husika.

Nikavutiwa, nikaamua kutafuta orodha ya majengo marefu zaidi Duniani. Nikabahatika kupata Top 100 Tallest Buildings.

Jengo refu kuliko yote Duniani linaitwa Burj Khalifa lipo Dubai lina urefu wa Mita 828, floors 163.

La pili linaitwa Shanghai Tower lipo Shanghai (China) lina urefu wa mita 632, floors 128.

La tatu linaitwa Makkah Royal Clock Tower lipo Mecca (Saudi Arabia) lina urefu wa mita 601, floors 120.

La nne linaitwa Ping An Finance Center lipo Shenzhen(China) lina urefu wa mita 599.1, floors 115.

La tano linaitwa Lotte World Tower lipo Seoul(Korea Kusini) lina urefu wa mita 554.5, floors 123.

China ina majengo mengi zaidi marefu Duniani, ina jumla ya majengo 49 ambayo yapo top 100 Duniani, Jiji la Shenzhen linaongoza kwa kuwa na majengo mengi(majengo 8) zaidi kati ya majiji 19 nchini China yanayojumuisha majengo 49 marefu zaidi Duniani.

Nchi ya pili kuwa na majengo mengi marefu Duniani ni Arab Emirates(Falme za Kiarabu) , ina jumla ya majengo 21 marefu Duniani .

Nchi ya tatu kuwa na majengo mengi marefu Duniani ni Marekani, ina jumla ya majengo 15 marefu zaidi Duniani.

Nchi zingine zenye majengo marefu zaidi Dunia ni Taiwan(2), Vietnam(1), Malaysia(3), Kuwait(1), Urusi(3), Thailand(1) na Australia(1).

Matumizi makubwa ya haya majengo ni kwa ajili ya Ofisi, Hotel na Makazi ya watu.

Afrika hamna jengo hata moja ambalo lipo top 100, sijui tunakwama wapi?

NB: Wahandisi mtatusaidia kufafanua, kuna majengo mengine ni marefu zaidi lakini yana Floors chache na kinyume chake, mfano: Ping An Finance Center ni refu kuliko Lotte World Tower lakini lina floors chake kuliko Lotte World Tower.

burj-khalifa-jpeg.1093932
shanghai_tower_2015-jpeg.1093933
makkah-royal-clock-tower-jpeg.1093934
ping_financial_center_in_june_2017_-jpeg.1093935
lotte_world_tower-jpeg.1093936
 

Attachments:

J

jembe afrika

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Messages
7,286
Points
2,000
J

jembe afrika

JF-Expert Member
Joined Jan 15, 2014
7,286 2,000
Nitampataje injinia aliyejenga hiyo jengo refu la dubai
 
kALEnga kidamali

kALEnga kidamali

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2015
Messages
435
Points
500
kALEnga kidamali

kALEnga kidamali

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2015
435 500
Hivi na lile la pale mawasiliano ni la ngapi kwa urefu duniani maana si kwa urefu ule
 
Amalinze

Amalinze

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2012
Messages
6,724
Points
2,000
Amalinze

Amalinze

JF-Expert Member
Joined May 6, 2012
6,724 2,000
800m+ Urefu?? Basement imezama mita ngapi kwenda chini?
 
Humorous Junior

Humorous Junior

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2018
Messages
890
Points
1,000
Humorous Junior

Humorous Junior

JF-Expert Member
Joined Jul 19, 2018
890 1,000
umetisha mzee, leo umenifuta matongotongo bila kujua!
 
Humorous Junior

Humorous Junior

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2018
Messages
890
Points
1,000
Humorous Junior

Humorous Junior

JF-Expert Member
Joined Jul 19, 2018
890 1,000
800m+ Urefu?? Basement imezama mita ngapi kwenda chini?
usiulize mzee unaweza kuwa chizi ghafla!
Hawa wenzetu hawana akili za kutawala watu ila wanataka kutawala vitu ambavyo watu wanatumia! SISI HUKU AFRICA E.g. nchi ya jiwe tunataka kutawala watu tunaacha vitu.

Ndiyo maana kwa wenzetu maandamano ni kawaida kwa sababu watu hawatawaliwi! WANAJITAWALA
 
fidel castro wapili

fidel castro wapili

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2017
Messages
788
Points
500
fidel castro wapili

fidel castro wapili

JF-Expert Member
Joined Mar 18, 2017
788 500
Africa bado tuna safari ndefu lakin tutafika!
 
baba swalehe

baba swalehe

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2017
Messages
8,524
Points
2,000
baba swalehe

baba swalehe

JF-Expert Member
Joined Jun 6, 2017
8,524 2,000
Nilidondokaga kwenye hilo jengo

Nikafa ...

Sijui mmeelewa ?!
 
Mwifwa

Mwifwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2017
Messages
31,483
Points
2,000
Age
19
Mwifwa

Mwifwa

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2017
31,483 2,000
Tz hayo majengo ni mpaka yesu arudi
Afrika nzima hakuna jengo refu lililoingia top 100, kuna majiji makubwa kama Johhanesburg, Cape Town, Cairo, Tunis, Accra n.k hamna.

Bongo kwa maendeleo yetu kiduchu, tutasubiri sana.
 
Mwifwa

Mwifwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2017
Messages
31,483
Points
2,000
Age
19
Mwifwa

Mwifwa

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2017
31,483 2,000
Na yote yamejaa au vyumba bado vipo
Hapo sijajua ila ni nadra kuwa empty(kujaa nusu)

Humo kuna Ofisi, Hotel na makazi ya watu.

Unaweza kukuta jengo moja wanaishi watu 60,000 ambapo inaweza kulingana na idadi ya watu katika jimbo zima huku bongo.
 
Mwifwa

Mwifwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2017
Messages
31,483
Points
2,000
Age
19
Mwifwa

Mwifwa

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2017
31,483 2,000
umetisha mzee, leo umenifuta matongotongo bila kujua!
Hata mimi nilivutiwa sana kujua hichi kitu, tuliowengi huwa tunafia kwenye ardhi yetu bongo bila kutembea nje za wenzetu hata kidogo.

Kwa hiyo teknolojia inatufanya tujue mambo mengi bila kutembea kwenda kujionea live kwa macho
 
Counsellor Sima

Counsellor Sima

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Messages
385
Points
500
Age
48
Counsellor Sima

Counsellor Sima

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2016
385 500
Majengo marefu na Tanzania hahaaa.....tuna ya kufanya kwanza kabla ya hayo magorofa
 

Forum statistics

Threads 1,296,165
Members 498,559
Posts 31,236,889
Top