PICHA: Majengo marefu zaidi Duniani, Jengo la kwanza lipo Dubai(UAE), China yaongoza kuwa na majengo mengi marefu Duniani

Mleta uzi hebu mzalendo na nchi yako na bara lako la Africa,Sifia vilivyopo kwenye bara letu na Nchi yetu sio ivyo vya wenzetu
Waafrika tunakwama wapi?

Bara lenye Utajiri wa Maliasili.
 
1094602
dah! umenikumbusha mbalii...
 
Katika pitapita zangu mitandaoni, nikapita forum kubwa zaidi Dunia(Skyscraper City forum) nikakutana na uzi katika miongoni mwa sub forum huko ukizungumzia majengo marefu katika miji husika.

Nikavutiwa, nikaamua kutafuta orodha ya majengo marefu zaidi Duniani. Nikabahatika kupata Top 100 Tallest Buildings.

Jengo refu kuliko yote Duniani linaitwa Burj Khalifa lipo Dubai lina urefu wa Mita 828, floors 163.

La pili linaitwa Shanghai Tower lipo Shanghai (China) lina urefu wa mita 632, floors 128.

La tatu linaitwa Makkah Royal Clock Tower lipo Mecca (Saudi Arabia) lina urefu wa mita 601, floors 120.

La nne linaitwa Ping An Finance Center lipo Shenzhen(China) lina urefu wa mita 599.1, floors 115.

La tano linaitwa Lotte World Tower lipo Seoul(Korea Kusini) lina urefu wa mita 554.5, floors 123.

China ina majengo mengi zaidi marefu Duniani, ina jumla ya majengo 49 ambayo yapo top 100 Duniani, Jiji la Shenzhen linaongoza kwa kuwa na majengo mengi(majengo 8) zaidi kati ya majiji 19 nchini China yanayojumuisha majengo 49 marefu zaidi Duniani.

Nchi ya pili kuwa na majengo mengi marefu Duniani ni Arab Emirates(Falme za Kiarabu) , ina jumla ya majengo 21 marefu Duniani .

Nchi ya tatu kuwa na majengo mengi marefu Duniani ni Marekani, ina jumla ya majengo 15 marefu zaidi Duniani.

Nchi zingine zenye majengo marefu zaidi Dunia ni Taiwan(2), Vietnam(1), Malaysia(3), Kuwait(1), Urusi(3), Thailand(1) na Australia(1).

Matumizi makubwa ya haya majengo ni kwa ajili ya Ofisi, Hotel na Makazi ya watu.

Afrika hamna jengo hata moja ambalo lipo top 100, sijui tunakwama wapi?

NB: Wahandisi mtatusaidia kufafanua, kuna majengo mengine ni marefu zaidi lakini yana Floors chache na kinyume chake, mfano: Ping An Finance Center ni refu kuliko Lotte World Tower lakini lina floors chake kuliko Lotte World Tower.

View attachment 1093932View attachment 1093933View attachment 1093934View attachment 1093935View attachment 1093936
Safi sana Great Thinker Mwifwa
 
Tumuulize JK kwa nn aliruhusu yajengwe kipindi chake cha uongozi. Ila kaa ukijua dunia nzima hayo majengo mengi yanajengwa kama prestige na kujionesha kuwa nchi ina mafanikio. Na mengi dunia nzima yanajengwa wakati uchumi unaumuka. Kama uchumi unasinyaa kamwe hutaona ujenzi wa majengo marefu.

Magufuli katika utawala wake yasipojengwa maana yake muda wake wote uchumi umenyong'onyea. Sio mm masema ila ndiyo wataalam wa uchumi wanasema hivyo kwa tafiti zao. Jaribu kusoma utaelewa.
Kwenda zako! Eti prestige? Mnapenda sifa za kijinga kweli kweli.

Sasa hivi tunajenga SGR na bwawa la umeme ili kukuza uchumi!
 
Kwenda zako! Eti prestige? Mnapenda sifa za kijinga kweli kweli.

Sasa hivi tunajenga SGR na bwawa la umeme ili kukuza uchumi!
Niende wapi? Hata hiyo SGR ya umeme inayojengwa ni prestige tu. Uchumi wetu bado hauwezi kumaintain miundombinu kama hiyo. Siyo mara ya kwanza sisi kujenga SGR kwa sababu hata TAZARA ni SGR tofauti ni kwamba yenyewe haitumii umeme. TAZARA hata kulipa mishahara wafanyakazi wake hatuwezi hadi Mchina huwa anatuokoa mara kwa mara.

Sijui hii mnayojenga kama Mturuki atakuwa anakuja kutuokoa tukikwama kuiendesha. Na sioni muujiza wowote kwanini uendeshaji wake usiwe kama TAZARA au BRT. Tuweke akiba ya maneno muda utaamua kama SGR ni viable project kwa sasa.

Ile reli aliyotuachia Mjerumani yenyewe pia imetushinda kabisa na kuna wakati ilikufa kabisa. Planner wetu walitakiwa walijue hili na kuchagua miradi ya kufanya kwa kutumia hekima na busara.
 
Wahandisi tusaidieni kufafanua hapa,

kwa nini majengo mengine ni marefu zaidi lakini yana Floors chache na kinyume chake? mfano: Ping An Finance Center ni refu kuliko Lotte World Tower lakini lina floors chake kuliko Lotte World Tower.
 
Wahandisi tusaidieni kufafanua hapa,

kwa nini majengo mengine ni marefu zaidi lakini yana Floors chache na kinyume chake? mfano: Ping An Finance Center ni refu kuliko Lotte World Tower lakini lina floors chake kuliko Lotte World Tower.
Mimi sio mhandisi ila jibu rahisi ni kuwa urefu wa floor ndio unaleta hio tofauti.
Mfano jengo la Mita 100 floor zake ni 5m kwa urefu litakuwa na ghorofa 20, jingine Mita 96 floor zake zina urefu 4m hili litakuwa na ghorofa 24
 
37 Reactions
Reply
Back
Top Bottom