Uzembe wa serikali katika kuhakikisha mipango miji, udhaifu wa wananchi katika kudai haki zao za msingi utatuletea maafa makubwa sana.
Halafu tutabakia kumlilia Mungu atusaidie kwa uzembe na upuuzi tuufanyao.
Maafaya haya ya mafuriko ni matokeo ya moja kwa moja ya uzembe wa mamlaka za mipango miji, watoa vibali vya ujenzi na wananchi wenyewe.
Unapoziba mkondo wa maji bila ya kujenga mbadala, bora tu upate sehemu ya kujenga yanapotokea haya ya mafuriko unakuwa na maelezo yepi? Wapi tunapata ujasiri wa kutaka Mungu atusaidie kwa uzembe tuliofanya?
Unapopanda pilipili utegemee kuwashwa, kama utatamani kujiramba inabidi upande zabibu.
Mungu anaingiaje hapa katika uzembe wetu?
Dua za makanisani na misikitini zitasaidia nini wakati uzembe tumeshaufanya kuwa ndio tabia na mazoea yetu?
Kama tutaelewa somo litokanalo na maafa, janga hili la mafuriko ya leo basi tutajipanga vyema kuepusha maafa makubwa zaidi siku zijazo.