PICHA: Mafuriko yalikumba jiji la Dar es Salaam

Nafikiri Siri Kali ianze kuweka stock ya kutosha kukabiliana na PINDUAPINDUA!
Mama/Baba lishe nao wachukue taadhari za kutosha!
Raia nao waache kutapisha mashimo ya vyoo vyao, Japo vingi vimeshafanya hivo automatically!
poleni sana mnaobanana Dar!
 
ila jamani dar ni ovyo kabisa,sehemu kubwa ni unplanned ata majanga kama aya yakitokea ni balaa tupu
hivi adi sasa icho kikao cha mkuu wa mkoa+wana-maji +jwtz wamechukua hatua gani?na hii mvua ikiendelea adi xmas ni kiama dar

pathetic poor town planning
 
jangwani hapo
406277_10150439474169366_548314365_8643829_1488863701_n.jpg

HII PICHA IMENIHUZUNISHA KUPITA MAELEZO!
Ni juzijuzi tu tumesherehekea miaka 50 ya UHURU na Slogan nzito sana " TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA SASA TUNASONGA MBELE"!!
Aliyeishawishi Serikali kutumia Slogan hii kweli ni DARING! SHAME!
HIVI, SERIKALI HAIWEZI KUTOA ANOTHER 65 Billion KUWASAIDIA HAWA WANANCHI KAMA HAWA , NA KUREKEBISHA MIUNDOMBINU?
 
Mods
Hii comment imechukuliwa na mafuriko?

Uzembe wa serikali katika kuhakikisha mipango miji, udhaifu wa wananchi katika kudai haki zao za msingi utatuletea maafa makubwa sana.
Halafu tutabakia kumlilia Mungu atusaidie kwa uzembe na upuuzi...
imepotea katika thread.
 
Uzembe wa serikali katika kuhakikisha mipango miji, udhaifu wa wananchi katika kudai haki zao za msingi utatuletea maafa makubwa sana.

Halafu tutabakia kumlilia Mungu atusaidie kwa uzembe na upuuzi tuufanyao.

Maafaya haya ya mafuriko ni matokeo ya moja kwa moja ya uzembe wa mamlaka za mipango miji, watoa vibali vya ujenzi na wananchi wenyewe.

Unapoziba mkondo wa maji bila ya kujenga mbadala, bora tu upate sehemu ya kujenga yanapotokea haya ya mafuriko unakuwa na maelezo yepi? Wapi tunapata ujasiri wa kutaka Mungu atusaidie kwa uzembe tuliofanya?

Unapopanda pilipili utegemee kuwashwa, kama utatamani kujiramba inabidi upande zabibu.
Mungu anaingiaje hapa katika uzembe wetu?

Dua za makanisani na misikitini zitasaidia nini wakati uzembe tumeshaufanya kuwa ndio tabia na mazoea yetu?

Kama tutaelewa somo litokanalo na maafa, janga hili la mafuriko ya leo basi tutajipanga vyema kuepusha maafa makubwa zaidi siku zijazo.
 
Poleni sana jamani kila aliyeguswa na hili janga kwa namna moja au nyingine. Mungu awatie nguvu na kuwazidishia uvumilivu. Inasitisha jamani na hivi serikali yetu ni kama iko likizo. Mungu atuepushe na maafa zaidi.
 
Nilikuwa juu gorofani MOI nikiangalia bonde la msimbazi, wakazi wakiwa juu ya paa, helikpta za polisi zikipita juu zikipiga picha.
Nikishuhudia mtu mmoja akidondoka kutoka paa hadi majini.
Akionekana kuogelea, akipigapiga maji, kuokoa maisha yake.
Mwishoni maji yakatulia.
Helikopta ziliendelea kuja na kupita.
Wakazi waliobaki wangali paani.
Terribly sad.
Sad...sad.....sad.
 
Unajua lilinijia wazo gani kila nilipoona hizo helikopta?
Nilijihisi kuwa na anti-aircraft missile au hata AK-47, ikipita nitungue,
wadondoke majini,
nikiwa na matumaini kuwa one of the big shot wa ikulu yumo kwenye helikopta.
Wish....
 
42 Reactions
Reply
Back
Top Bottom