GOOD JOB
Kazi ya Chama cha siasa sio uchaguzi tu bali pia kuelimisha, kuamsha hamasa, na kuongoza Wananchi. Tumeona CCM wakipata uongozi wanajilundika Dar...CDM mjitahidi hizi movement ziwe endelevu.
***Katika hiyo mikutano na Maandamano viongozi wa CDM wasiishie kulaumu na kukosoa tu, bali pia wawaelimishe wananchi mambo mbalimbali kama kufanya kazi kwa bidiii mana serekali yao imewasahau, kusimamia mali za umma, kuacha kutoa na kupokea rushwa, kuwa waaminifu, na kujikinga na maradhi kama Ukimwi, ajali na vitu kama hivyo mana wakifa au wakiwa dhaifu yale CDM wanayoyapigania itakuwa kupoteza muda.
Pia CDM ijaribu kuwavutia akina mama na wanawake kwa wingi mana hao ndio wapiga kura, na misimamo yao sio rahisi kubadilika. Kwenye hizo campain zenu piganieni matatizo yanayowakumba akina mama kama AFYA YA UZAZI, Unyanyasaji, ELimu na mambo kama hayo yatakayowavutia kujiunga na harakati za kuikomboa Nchi.