Tunataka tunyong'onyeshe CCM kuanzia year 1 na ifikapo 2014 iwe imebakiwa na ving'ang'anizi vichache aina ya Saddam Hussein na Gaddafi. We should remain focused on 2015. CDM kwa sasa tunatakiwa tufanye yafuatayo:
1. Kujenga heshima miongoni mwa watanzania mikoa yote dini zote na watu wa umri wote
2. kujenga imani miongoni mwa watanzania mikoa yote, dini zote na watu wa umri wote
3. Tufute dhana ya CDM ni chama cha vurugu
4. Tutumie ipasavyo nafasi tunayopata katika Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukwepa kuonekana vilaza na badala yake tutoe hoja, tuulize maswali na tupinge vitu vyevye mantiki na maslahi kwa watanzania bila kujali dini, itikadi na mtu atokako.
5. Kuzungumzia umuhimu wa amani kuliko CCM ili kuwa prove wrong kuwa lengo la CDM ni kuleta vurugu na kuondoa amani iliyojengwa na waasisi wa Taifa letu.
6.Kutekeleza ahadi zote mtoazo kwa vitendo bila kutoa visingizio vya kutetea failure
Kwa kufanya haya na mengine mengi mtakayo yaona yanafaa kutawatengenezea njia nyeupe ya kuwabwaga hawa CCM kirahiiiisi bila kutumia nguvu nyingi.
Tuko pamoja, tunawaunga mkono na tunahitaji mabadiliko na ninaamini CDM bado mpo kwenye mkondo mzuri wa kuleta mabadiliko
PEOPLES POWER FOREVER AND EVER!!!