Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,811
- 34,193
Picha hii iliochapishwa katika mtandao wa Serikali ya Kenya wa Twitter imevutia hisia chungu nzima.Inamuonyesha Mwanamke mmoja wa kiislamu akikataa kumsalimia Rais Uhuru Kenyatta kwa kumshika mkono kwa sababu ya dini yake hairuhusu Mwanamke kumshika Mkono mwanamme ambae sio mume wake.
Mtumiaji mmoja wa mtandao wa Twitter Rais Uhuru Kenyata alijibu kwa kusema kuwa ''Dada yangu umedhihirisha umuhimu wa Mwanamke Wa Kiislamu, hakuna kusalimiana na mkono hata ikiwa ni Marais''. Mtandao wa Twitter wa serikali ya kenya umesema kuwa Rais ameonyesha heshima yake kwa dini tofauti.
Toa maoni yako.
chanzo.BBC Swahili