Kwanini mageuzi ya kusitasita ya Rais Samia yanachochea hasira ya kisiasa nchini Tanzania?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,860
34,319
.

Chanzo cha picha,Reuters
Maelezo ya picha, Kiongozi wa chama cha upinzani Chadema Freeman Mbowe amekamatwa mara mbili wiki za hivi karibuni Maelezo kuhusu taarifa

Wimbi la hivi karibuni la utekaji nyara, kukamatwa na mauaji ya kikatili ya kiongozi mmoja wa chama cha upinzani nchini Tanzania, yameonekana kufifisha mwanga wa matumaini ya kisiasa - ambayo yalikuja baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuingia madarakani mwaka 2021.

Kulikuwa na ahueni kubwa pale Samia - rais wa kwanza mwanamke wa Tanzania - alipoingia madarakani, na vyama vya upinzani vikaruhusiwa kuandaa mikutano ya hadhara na kuikosoa serikali bila hofu ya matokeo hasi.
Lakini wasiwasi unaongezeka kwamba Tanzania inarudi nyuma katika enzi za mtangulizi wake, John Pombe Magufuli.

Katika kipindi cha wiki kadhaa, viongozi wawili wakuu wa upinzani wamekamatwa mara mbili, na kiongozi mwingine wa upinzani, Ali Kibao, alitekwa nyara na kuuawa na mwili wake kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana.

"Hali ya kisiasa nchini Tanzania inatia wasiwasi sana," anasema Makamu mwenyekiti bara wa chama kikuu cha upinzani, Chadema, Tundu Lissu.

Alikuwa akizungumza na BBC wiki moja kabla ya kukamatwa kwake siku ya Jumatatu, wakati chama chake kilipopanga kuandamana kupinga mauaji ya Kibao na kutoweka kwa wakosoaji wengine kadhaa wa serikali. Baadaye Lissu aliachiwa kwa dhamana.

Pia aliachiliwa kwa dhamana mwezi uliopita, kufuatia kukamatwa siku moja kabla ya mkutano wa chama cha upinzani uliopigwa marufuku katika mji wa kusini-magharibi wa Mbeya.

Chadema inasema wanachama wake wapatao 100 walishikiliwa ili kuzuia mkutano huo usifanyike.

"Tunaanza kuona aina ya wimbi la ukandamizaji na ghasia za serikali ambazo zilikuwepo katika kipindi cha 2016 hadi 2020 [wakati wa utawala wa Magufuli]," Lissu aliiambia BBC.

Mageuzi yanayofifia​

o

Chanzo cha picha,AFP
Maelezo ya picha,Tundu Lissu akiwa hospitalini baada ya watu wasiojulikana kumfyatulia risasi kwenye gari lake mwaka 2017.

Mwaka 2017, Lissu alipata majeraha makubwa wakati wa jaribio la kutaka kumuua, pale gari lake lilipopigwa risasi 16.

Alitibiwa nje ya nchi na alikaa uhamishoni nchini Ubelgiji hadi aliporejea mwaka jana, kama anavyosema, "ili kuanza mwanzo mpya" baada ya rais kuondoa marufuku ya mikutano katika nchi.

Lissu sasa anayaona mageuzi yaliyoahidiwa yakififia.

“Hakuna mageuzi yoyote. Hakuna mageuzi ya kidemokrasia,” aliambia BBC.

Matukio ya vurugu yanayochochewa kisiasa na “yanayohusishwa na vikosi vya usalama" akituhumu, na kuongeza kuwa ni ishara ya hali mbaya zaidi ijayo.

Polisi wamekana kuhusika, huku Katibu Mkuu wa chama tawala cha CCM, Emmanuel Nchimbi akikataa kuzungumza na BBC.

Hakuna shaka kwamba ukandamizaji huo umechafua taswira ya rais.

Mashirika ya haki za binadamu na wanadiplomasia wa nchi za magharibi wametoa wito wa kukomeshwa mara moja "ukamataji wa kiholela" na wametaka "uchunguzi huru na wa uwazi."

Katika majibu yake, rais aliwaonya “watu wa nje” dhidi ya kuingilia masuala ya ndani ya Tanzania, lakini kwa upande mwingine alilaani mauaji ya Kibao, na kuamuru uchunguzi ufanyike haraka.

"Nchi yetu ni ya kidemokrasia, na kila raia ana haki ya kuishi," alisema.

“Inashangaza kifo cha ndugu yetu Kibao kimeibua kilio kikubwa cha kulaani, majonzi na shutuma za kuita serikali wauaji.

“Hii si sawa. Kifo ni kifo. Tunachopaswa kufanya Watanzania ni kusimama pamoja na kukemea vitendo hivi,” aliongeza.

Kurejea kwenye mazungumzo​

l

Chanzo cha picha,Getty Images
Maelezo ya picha,Samia Suluhu alikuwa naibu rais wa Tanzania, kabla ya kuwa rais

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Tanzania, Thomas Kibwana, anasema kunaonekana kukosekana kwa nia njema kati ya vyama vikuu vya kisiasa, jambo ambalo limesababisha mazungumzo yanayolenga kuleta mageuzi kukwama.

Aliongeza kuwa ingawa mivutano inaweza kuinufaisha upinzani kushinda kura, ila inachochea wasiwasi.

Samia alionyesha kuwa "yuko wazi kwa ajili ya mazungumzo" na, kwa mtazamo wa rais huyo, Chadema imefunga milango ya mazungumzo na kuchukua hatua ya maandamano,” anasema Kibwana.

"Hili ni la suala la pande mbili - wakae chini na kurejea kwenye mazungumzo," aliongeza.

Hapo mwanzoni, Samia alizingatia sana msemo wake uliorudiwa sana wa mambo manne - maridhiano, ustahamilivu, mageuzi na ujenzi upya.

Hatua zake za kurekebisha uhusiano na upinzani na kuanzisha mageuzi - hasa wakati ambao hakuwa chini ya shinikizo la kisiasa kufanya hivyo - zilimletea sifa ndani na nje ya nchi.

Bado kuna dalili za taswira nzuri anayotaka kuidumisha.

Mabango ya Samia​

m

Chanzo cha picha,BBC/Alfred Lasteck

Maelezo ya picha,Bango likimuonesha Rais Samia Suluhu na mwanasiasa maarufu wa upinzani Tundu Lissu
Bango moja katikati ya mji mkuu, Dodoma, linasema: “Rais wa Kila Mtanzania – bila kujali Chama, dini, kabila jinsia. Mama [Samia] anatimiza.”

Bango hilo lina picha yake akiwa kwenye mazungumzo na Lissu, ambaye sasa ni mmoja wa wakosoaji wake wakubwa.

Mabango mengine, ikiwa ni pamoja na katika jiji kubwa la Dar es Salaam, yanamwonyesha akiwa na viongozi wengine wa upinzani, akionyesha nia yake ya kutaka kuunganisha watu kutoka nyanja mbalimbali za kisiasa.

Yanaonekana kuwa ni matangazo ya kampeni kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi ujao na uchaguzi wa rais na wabunge mwaka mmoja baadaye.

Uchaguzi utakuwa mtihani wake wa kwanza. Alikuwa makamu wa Magufuli, na alirithi urais kufuatia kifo chake cha ghafla wakati wa janga la Uviko 19.

Kama ilivyo kwa Magufuli, yeye ni mwanachama wa Chama cha Mapinduzi, CCM, ambacho kimeshinda kila uchaguzi kilichoshiriki tangu uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka 1961.

Kwa mujibu wa chama cha pili kwa ukubwa cha upinzani, ACT-Wazalendo, harakati za Samia kufanya mageuzi huenda zimekwama kutokana na hofu ya CCM kwamba inaweza ikashindwa katika uchaguzi.

"Tumemsikia kigogo mmoja wa CCM akisema, ‘kama angeendelea na kasi hiyo aliyoingia nayo, angepoteza nchi kwa upinzani," kiongozi wa chama hicho Dorothy Semu aliambia BBC.

"Kwa hivyo labda aliimeza hofu hiyo kwamba ikiwa utafanya mageuzi, hatimaye utaishia kusalimu amri kwa upinzani," aliongeza.

Lakini Semu anahisi hali ya kisiasa ni bora kuliko wakati wa Magufuli: "Sasa tuna nafasi ya wazi zaidi kama raia.

Tunaweza kuzungumza juu ya siasa kwa uhuru. Tunaweza kujadili kama vyama vya siasa. Tunaweza kushiriki katika mikutano ya hadhara ya vyama ya kisiasa. Tunaweza kuandaa mikutano ya ndani,” aliambia BBC.

Semu aliongeza kuwa uchaguzi unapokaribia, "tuna matumaini, lakini hatuna uhakika kwamba kila kitu kitakwenda vizuri."

Wakili na mwanaharakati Fatma Karume aliiambia BBC kwamba mageuzi ya kweli hasa yapo kwenye urekebishwaji wa sheria za nchi ili rais awe na nguvu kidogo.

"Tanzania tuna kitu kinaitwa urais wa kifalme," anasema.

"Kile tulichonacho, ni mkuu wa nchi ambaye kapunguza tu kidogo uonevu...tuseme, hayuko kama Magufuli katika kutumia nguvu za kikandamizaji za serikali."

Chanzo. BBC
 
CCM walikuwa wanahadaa tu wananchi kuwa watafanya mageuzi makubwa!
Hicho kitu hakiwezekani kwa ccm hii bila kudai kama wenzetu Kenya walivyofanya!
 
Back
Top Bottom