Picha hizi zinasikitisha, tunawafaidisha Wazungu

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,874
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg


Picha hii imepigwa Nigeria,mtoto akiwa amedhoofu kwa kukosa lishe bora,inasemwa Dada huyu Raia wa Denmark alijitolea kumchukua mtoto na kumuogesha,kumpatia lishe na matibabu.Na sasa mtoto kaanza kupata tabasamu na siha njema
 
dah, ...hiyo ni nchi inayouza mamilioni ya mapipa ya crude oil kila siku ... serikali zetu za kiafrika hovyo kabisa

Mawaziri wa Nigeria ni wezi kama wakina Yona na Mramba na wameficha mabilioni ya fedha ughaibuni halafu wakikamatwa wanafungwa kifungo cha nje bila kuwalazimisha warudishe hizo fedha walizoiba ili watoto wapate lishe ya kutosha na dawa kwenye zahanati!! Halafu Donald Trump akiwatukana waafrika mnakasirika kwani mkiambiwa ukweli mnaumia!!
 
Afrika yenyewe viongozi ndio hawa Akina mkurunzinza na mseveni vyama vikongwe ndio kama ccm na kina Mugabe sasa vitu kama hivyo lazima vitokee viongozi wote ni mafisadi
 
Ukisikia sadaka ambazo zinamgusa Mungu aliko ni kama hizi, mahekalu tunayoshindana kujenga hayana maana yo yote kama kuna majirani wanaokufa njaa karibu yetu.
 
Kweli mtoto kadhoofika. Lakini yapo mambo mengi yanaweza kuchangia watoto kuwa na afya mgogoro sio kukosa lishe tu!
Mama mzazi wa mtoto asipojiheshimu pindi ananyonyesha anaweza kumsababishia madhara mtoto na kupelekea mtoto kuthoofika kama huyo aliyepo kwenye picha.
Na hii hali haichagui mtoto kazaliwa taifa gani.
Hivyo basi kuna uwezekano hata huko Denmak kuna watoto wenye utapiamlo na waliodumaa kama huyo Mnigeria.
 
Daaaah,sasa wazazi wa huyo mtoto wako wapi?Na mbona hao wanaoshangaa hapo wako na siha njema?
Iweje yeye?
 
Kwa taarifa yenu hali hii inatengenezwa makusudi kabisa na hao hao wazungu,wao ndio wameziweka serikali zote za Africa madarakani lengo lao kubwa ni kutengeneza migogoro kati ya watawala na wananchi,ili wao baadae wazungu wajifanye miungu watu,kwa taarifa hakuna utawala wowote Africa ambao hauko chini ya mkoloni
 
Sasa hayo maseng..e hapo pembeni yanaangalia nini? utafikiri yalikua hayamuoni at the first place..sisi waafrika ni wajinga sana ndo maana hata baadhi ya maziwa na milima tunaambiwa waligundua wazungu..haiwezekani swala kama hili kuilamu serikali wakati hao pimbi hapo pemben wapo na wanaafya zao na hawakumfanyia kitu chochote..fala sana waafrika.
 
kawabie wachungaji hili

Wachungaji hawahusiki kabisa hapo. Suala la kusaidia jamii inayokuzunguka halina dini, wala kabila. Na niliposema mahekalu, nilijua kuna wadau watalenga nyumba za Ibada, nina maana yale majumba yetu makubwa makubwa ambayo idadi ya wakazi waishio ndani ni kama watatu hivi, yaani House girl, mlinzi na dreva.
 
Back
Top Bottom