Picha hii inatuaibisha watanzania

MPHINGU

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
519
1,000
Kuna picha za kutisha tunazo ziona zinazo tokea kwenye nchi zisizo salama, hizo picha tukiziona mitandaoni, hazitushangazi kwa vile nchi hizo hazina usalama kwao kujeruhi,kuuwa,kubaka hata Kula nyama ya binadamu nikawaida tu.

Kwa hapa Tanzania ni tofauti, sababu Tanzania inajulikana duniani kuwa ni nchi salama duniani na ni kisiwa cha amani na ni nchi yenye kulinda haki za binadamu na ni nchi inayo sifiwa kuwa polisi wake wana weledi wa kulinda haki za raia wake.

LAKINI KWA PICHA HII HAPA
Kama ni ya ukweli(sio edit wala maigizo) itatuharibia sifa ambazo jeshi letu la polisi pamoja na chama tawala (kwenye picha kuna kiongozi wa chama) walizo nazo, kwa sababu kwenye nchi zenye utawala bora, haija wahikutokea POLISI amfanyie KILEMA kitendo cha aibu kama icho
 

Blessed

JF-Expert Member
Nov 16, 2011
3,066
2,000
K
Haya ndio madhara ya kupeleka form four failure kwenye jeshi letu la polisi!
Sasa majitu manne yamemzunguka huyo kilema inamaana anauwezo wa kukimbia?
kilema na mlemavu unaweza kudhani haina tofauti, lakini kwao ina maana kubwa zaidi, mlemavu ni neno sahihi zaidi kutumia!
 

Gemini6

Senior Member
Jun 21, 2017
153
250
Nikiangaliaga maandamano ya nchi za wenzetu,hasa ulaya na baadhi za arabuni,then ukatizama hapa kwetu waweza dhani vyombo vyetu vya ulinzi vina laana.
 

MPHINGU

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
519
1,000
Mkuu hao walemavu kilicho watuma waandamane ni dhamira ya yaki yao ya kushi na kuingia popote wewe na mimi tulio kamilika viungo tunayo
 

chibuga mugeta

JF-Expert Member
Jun 29, 2012
1,043
2,000
Kuna picha za kutisha tunazo ziona zinazo tokea kwenye nchi zisizo salama, hizo picha tukiziona mitandaoni, hazitushangazi kwa vile nchi hizo hazina usalama kwao kujeruhi,kuuwa,kubaka hata Kula nyama ya binadamu nikawaida tu.
Kwa hapa tz nitafauti, sababu tz inajulikana duniani kuwa ni nchi salama duniani na ni kisiwa cha amani na ni nchi yenye kulinda haki za binadamu na ni nchi inayo sifiwa kuwa polisi wake wana uweledi wa kulinda haki za raia wake.
LAKINI KWA PICHA HII HAPA
kama ni ya ukweli(sio editi wala maigizo) itatuharibiya sifa ambazo jeshi letu la polisi pamoja na chama tawala (kwenye picha kuna kiongozi wa chama) walizo nazo, kwa sababu kwenye nchi zenye utawala bora, haija wahikutokea POLISI amfanyie KILEMA kitendo cha aibu kama icho
Huyo pembeni ni kada wa CCM hivyo wapo ktk kutimiza ilani ya CCM safi sana
 

fred1149

JF-Expert Member
May 30, 2016
203
250
Mi nafikiri kuwa suala la kila mtu kufuata sheria halihusu jinsia wala ulemavu. Nakubaliana nao kuwa walemavu huwa wanapewa vipaumbele na kusikilizwa pale wanapokuwa na madai yao na pia hata waziri yupo kwa ajili yao.

Tatizo kubwa ni hili la kila mtu akiwa na tatizo fulani basi maandamano au kufunga barabara ndo solution. Hili halikubaliki kwa community ambayo Kuna utawala wa sheria. Hakukuwa na haja ya kufunga barabara Zaidi ya viongozi wao kwenda kumuona kamanda mpinga.

Polisi nao pia wanapenda kupumzika na wake zao, kucheza na watoto wao, mtoko na wake zao na kutunza familia. Sasa wanapokuwa wanavurugwa kwa mambo ambayo yanaweza kutatulika kiurahisi na wao wanakuwa na hasira maana na wao wanapenda kuishi kama watu wengine na kupumzika na matokeo yake hasira zao ndo matokeo ya hayo wanayofanya.

Mfano mtu amekesha usiku kucha, hasubuh anaenda kupumzika, anaitwa tena kuwa Kuna walemavu wamefunga barabara. ILA NINAPINGA VIKALI KWA HATUA WALIZOCHUKUA DHIDI YA WALEMAVU NA IWE MWANZO NA MWISHO KUFANYA HIVYO NA HATUA KALI ZICHUKULIWE PINDI WAKIRUDIA.

PIA NA WALEMAVU NAO WASICHUKUE ULEMAVU WAO KATIKA KUSHINIKIZA AU KUANDAMANA AU KUFUNGA BARABARA KWA SHINIKIZO AMBALO LINAWEZA KUTATULIKA KWA KUONANA NA VIONGOZI NA HIVYO WANA WAJIBU WA KUTII SHERIA BILA SHURUTI. OFISI YA IGP IPO NYUMA YA POSTA, WANGEWEZA KWENDA KUMUONA NA WANGEMALIZA SHIDA YAO
 

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
5,668
2,000
Mi nafikiri kuwa suala la kila mtu kufuata sheria halihusu jinsia wala ulemavu. Nakubaliana nao kuwa walemavu huwa wanapewa vipaumbele na kusikilizwa pale wanapokuwa na madai yao na pia hata waziri yupo kwa ajili yao. Tatizo kubwa ni hili la kila mtu akiwa na tatizo fulani basi maandamano au kufunga barabara ndo solution. Hili halikubaliki kwa community ambayo Kuna utawala wa sheria. Hakukuwa na haja ya kufunga barabara Zaidi ya viongozi wao kwenda kumuona kamanda mpinga. Polisi nao pia wanapenda kupumzika na wake zao, kucheza na watoto wao, mtoko na wake zao na kutunza familia. Sasa wanapokuwa wanavurugwa kwa mambo ambayo yanaweza kutatulika kiurahisi na wao wanakuwa na hasira maana na wao wanapenda kuishi kama watu wengine na kupumzika na matokeo yake hasira zao ndo matokeo ya hayo wanayofanya. Mfano mtu amekesha usiku kucha, hasubuh anaenda kupumzika, anaitwa tena kuwa Kuna walemavu wamefunga barabara. ILA NINAPINGA VIKALI KWA HATUA WALIZOCHUKUA DHIDI YA WALEMAVU NA IWE MWANZO NA MWISHO KUFANYA HIVYO NA HATUA KALI ZICHUKULIWE PINDI WAKIRUDIA. PIA NA WALEMAVU NAO WASICHUKUE ULEMAVU WAO KATIKA KUSHINIKIZA AU KUANDAMANA AU KUFUNGA BARABARA KWA SHINIKIZO AMBALO LINAWEZA KUTATULIKA KWA KUONANA NA VIONGOZI NA HIVYO WANA WAJIBU WA KUTII SHERIA BILA SHURUTI. OFISI YA IGP IPO NYUMA YA POSTA, WANGEWEZA KWENDA KUMUONA NA WANGEMALIZA SHIDA YAO
Polisi wote waliomba kazi hiyo na wakaapa kuitumikia kazi hiyo kwa weledi!! Kama wanaona wamechoka waondoke waje wengine!!
 

fred1149

JF-Expert Member
May 30, 2016
203
250
Hakuna anaependa kazi, kila mtu anapenda apumzike na watoto na mwandani wake, kwa hiyo kutokn na kukosa kazi na elimu zetu kuwa za wastani, mtu anaona kuliko kuwasumbua wazazi au kutokana na maisha duni tunayoishi ambayo kila mtu katoka, ndo solution linakuwa ni kuomba hata kazi kama hyo ambayo leo vifo vingi vinawapata. Kwani Kuna mtu anaependa kufa, au kufanya kazi 24 hrs Bila kupumzika na bado anaweza fanya hata siku 4 mfululizo Bila kupumzika kutokn na fujo kama za uchaguzi kipindi kile, kibiti na kisha hata hii ya walemavu? Sometimes ndipo hasira inapoanzia kwani suala la kukamatwa kwa walemavu eti kisa kuendesha bajaji mjini nakumbuka ni agizo la waziri mkuu. Ni kiasi cha kwenda kwake au kwa IGP na najua wao hawana cha appointment wala usumbufu, direct mpaka ofisini na kutoa malalamiko yao. Huenda hao traffic au Polisi wangeweza kukamatwa au tamko kutolewa tena. Kulikuwa na haja ya kuandamana? Au kufunga barabara? Au walichofanya sio kosa? Je watashtkiwa kutokn na ULEMAVU WAO au kama mtu yoyote? Hatuwez kushindwa kuchukua hatua kisa ni walemavu, hii inaweza sababisha na watu wengine kuona hiyo ndo solution. Pia waliambiwa watoke kiustaarabu wakakataa. Hivi mfano wangekaa siku nzima, shughuli zote zisimame, kodi ya serikali ipungue, watu wengine wasipate riziki zao, wengine wapate hasara kwa kubeba bidhaa zinazoweza kuharibika mapema, wengine wasingeenda ofisini mapema na wangeweza kufukuzwa kazi, biashara ingedoda, eti kisa walemavu wachache wamefunga barabara na hawataki kutok? Wanahaki gani hyo kuzidi wengine? Mbona process zingine za kiserikali wakazifuata Bila shuruti au kutumia ULEMAVU? Je na albino nao wakifunga barabara kisa serikali haijawapa madawa yao? Hapo kila mlemavu akichukua sheria mkononi, si barabara zote dar zingefungwa siku nzima? ILA SITETEI KITENDO CHA POLISI KUPIGA RAIA MAANA NI KINYUME NA SHERIA ILA NA WANANCHI TUCHUKUE UAMUZI AMBAO UNAWEZA KUWA WA BUSARA KATIKA KUJIPATIA HAKI ZAKO. KUMBUKA KUNA MSEMO UNASEMA "WHERE THE DIPLOMACY FAILED, THEN USE OF FORCE IS APPLIED"
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom