Picha: Hii imekaaje?

Status
Not open for further replies.
Huyo jamaa yuko sahihi though kuna wakati anakuwaga mnazi sana.
Kuna siku Diwani wa UKAWA aliitwa jukwaan wakati Diwani anatoa Salam akamkatisha na kumwambia "Sema Mtukufu Oyee"
 
Hatujawahi kuwa na askari weledi nchi hii. Type yao ni ile ya colonial times, kupenda ukatili na kuogopwa!. Huenda Ndio system ya kijani!


Watanzania bhana, mtu unajifanya 'ujuaji' hata kwenye fani za watu. Na haya 'mahaba' ya kisiasa ndiyo yanawafanya kuwa mapunguani kabisa kichwani, mmekuwa vihiyo wa kupinga kila jambo.

Haya hebu ona picha hii hapa, alafu sema sasa:



Acheni kupayuka na kuropoka ropoka kwenye fani za watu. Ulinzi wa Rais ni profession kabisa yenye codes na ethics zake. Hawafanyi kwa kubahatisha.

-Kaveli-
 
Asante hata kwa hilo, bahati mbaya huwa hata siendi huko kwa vijana wa kileo!Lakini naamini hata wao huko wanazo hoja za maana
NeΓ±da kama hujarudi mbio huku
 
Hiyo kitu hairuhusiwi ku hold/kumshika kiogozi wa juu kwa mda hiyo ipo popote pale duniani!

Kuna wengine wanatumia njia hiyo kumdhuru rais,

Hawa Jamaa wanajua sana majukumu yao hawabahatishi na rais hawezi kuhoji
Duuu kuna watu ni kiboko ,mkuu huo mda ambao hautakiwi kwenye picha hii umeupimaje ?
 
Tatizo lako unakurupuka,hapo Putin ameenda kuwavaa wananchi waliojipanga Pembeni na kuanza kuwapa mikono!Eneo hilo sio salama sana na walinzi wanahitaji kufanya kama wanachokifanya,kutokumuexpose sana Rais!Lakini picha niliyoweka hapo juu ni ya jukwaa maalum la watu mashuhuri ambao wamewekwa kiutaratibu akiwemo Twaha!Line hiyo ilijulikana kabisa kuwa watapeana mkono na mh Rais!Ni watu waliowekwa mstari wa mbele wa jukwaa kulingana na umuhimu wao kwa shughuli husika hasa huyo Bwana Twaha ambaye ndiye wakili aliyewatetea wananchi kwa miaka yote hiyo mpaka Leo wamepata tumaini!Tofautisha mazingira
 
Huwezi ukaung'ang'ania mkono wa Rais usije kumdhuru. Tena nadhani walimheshimu huyo jamaa manake nijuavyo jamaa hupiga mkono wa mtu na kumuachia maumivu makali huku wanaondoka na Rais.
Aiseee hii imetokea wapi Mkuu ,hebu naomba hata kapicha jamaa wakipiga mkono wa mtu na kumwachia maumivu huku wakiondoka na Rais
 
Mwanya upi alikuwa nao wakati mono ulikuwa umeshadhitiwa? Kama ni kumpiga rais kibao au tanganyika jeki asingepata hiyo nafasi!
Wanausalama wao wanafata protoko na sio ku guess huyu anafaamiana au rais anafikiria nini kichwani.

Mfano, Kitwanga ni rafiki yake Magufuli, angekuwa kwenye huo umati halafu akanyosha mkono kusalimiana na Magufuli na kutaka kuongea nae halafu usalama wakamwacha, Magufuli ana budi kumpa mkono hata kama alikuwa nia ya kumsalimia. Na hakilalamika chemba walinzi wake watakuwa kwenye wakati mgumu kujitetea.
 

Hiyo ndiyo maana ya usalama. Hautakiwi uchukulie mambo kirahisi hasa unapokuwa na jukumu la kumlinda unayemlinda. Wakati akitafutwa kimataifa Carlos Ramirez alikutana na wasuluhishi kwenye uwanja wa ndege mahali fulani baada ya tukio la Vienna. Kiwanjani hapo yule mkuu wa wasuluhishi alipeana mkono na Carlos akiwa amejifunga bastola ndogo mkononi ndani ya koti. Huyo bwana alipaswa kufyatua amwue Carlos palepale, ila hakufanya hivyo na haijulikani kwa nini alishindwa kufanya hivyo. Carlos akarudi katika ndege salama akaendelea kusumbua mpaka muda aliyokamatwa. Mlinzi yuko sahihi. Wakati mwingine walinzi wa wakuu huwapiga vikumbo watu wanaonekana kumsonga mkuu anapopita njiani. Haya ni maoni yangu tu si ya kitaalamu sana.
 
Hao ndio zao! . Jamaa alipaswa akiishasalimiwa auachie mkono hivyo ikambidi jamaa wa usalama aingilie kati kuuzuia mkono ili kuwaachanisha!.

Pasco

kwanza rais ndo kashika mkono wa jamaa
 


'' Wabongo tunajua kila kitu, na ukitaka kuthibitisha hili kaa kwenye kahawa! '' by wise-comedian

πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ™‚πŸ™‚

-Kaveli-
 
Ukiangalia mkono wa kushoto wa Rais bado haujatua kwenye bega la la anayesalimiana naye,hii inamaana salami ilikuwa bado mbichi!
Vipi kama ndo alikua anatoa..
 
Ukitumia fikra huru utaelewa,mkono ambao ameshikana na Rais anawezaje kurusha kofi?
 
Hapo sio njiani,ni jukwaa maalum lilioandaliwa kwa watu mashuhuri hasa wanaohusika na shughuli hiyo!
 
'' Wabongo tunajua kila kitu, na ukitaka kuthibitisha hili kaa kwenye kahawa! '' by wise-comedian

πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ™‚πŸ™‚

-Kaveli-
Ndio kama wewe unavyotokwa mishipa kama unajua kila kitu!Kama hujui kwanin unapinga kwa nguvu zote hizo
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…