Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 580
- 541
Dr.Zack
June 2,2026.06:54AM.
Baada ya Serikali ya Tz jana kutangaza kuwa Mh Rais Samia Suluhu Hassan kesho June 3,2026 anaanza ziara ya siku mbili Nchini Urusi ilinifurahisha sana.
Hii inaweza kuwa ni ziara bora zaidi na ya kimkakati sana tangu Mh Rais Samia Suluhu Hassan aingie Ikulu baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.Hii ziara ya Nchini Urusi ya Mh Rais Samia,kwangu mimi ni zaidi ya ziara.
Ziara hii imenipa nafasi ya kuja na neno lingine jipya kwenye mawanda mapana ya mahusiano ya kimataifa-mkakati yaani "GEOPOLITICAL DEPLOMACY".Kwenye mfumo huu mpya ambao wajuzi wa mahusiano ya kimataifa Mkakati wanatakiwa kuwafundisha Wanafunzi wao huko Vyuoni ni kwamba👇🏽👇🏽👇🏽
Kuna mambo Makuu kama Matatu hivi kwa mtazamo wangu Mimi "a state has to achieve" katika siasa mKakati za kimataifa za kisasa ambayo ni (I)Strategic Alliance to consolidate nation's powers(II)Alliance for Resource share na tatu (III)while defending National Security and Sovereignity.
Ziara ya Mh Rais Nchini Urusi inakwenda "kuioffer"Nchi yangu Tanzania mambo yote matatu kwa pamoja na hii ndio MIMI nimeipa jina leo kuwa ni aina mpya ya diplomasia ya dunia ambayo ni lazima(TZ) unakubali kuwa hauwezi kuwa na (I)Maadui wote na hauwezi kuwa na (II)Marafiki wote ndani ya dunia hii.
IPO HIVI👇🏽👇🏽
Katika aina hii mpya ya Diplomasia ya dunia ni kwamba,kwa maoni yangu inaigawa dunia katika mafungu makuu matatu ya kimkakati;(I)Alliance ya CHINA URUSI na wafuasi wao(II)Marekani na Ulaya na washirika wao na (III)Mashariki ya kati na washirika wao.
Katika aina hii ya "Triangle Geopolitical Diplomacy"Nchi za bara la Afrika Tanzania ikiwemo zitalazimika kuchagua strategic wadau ambao wanaweza kulinda kwanza (I)Maslahi yake ya Ulinzi Usalama na Uhuru wake kama Taifa kabla wadau hao hawajalinda(II)maslahi yake ya kiuchumi pekee yake na hii ndio nimeiita "Geepolitical diplomatic shift".
Mfano,Mswada wa Bunge la Senate la Marekani dhidi ya Tanzania unaoendelea kuchakatwa kule Marekani na Wabunge wetu kuupigia kelele sana wiki jana kuwa unaingilia Uhuru wetu kama Nchi ni mfano mzuri wa " Geopolitical alliance" ambayo hailindi maslahi ya ULINZI NA UHURU wa Tanzania ambao kwangu mimi mswada ule ni hatari kwa maslahi mapana ya uhuru wa Taifa langu Tanzania.
Ziara ya Mh Rais Samia Nchini URUSI kwa jicho la Sovereignity Diplomacy una lengo kuu la kulinda Uhuru wa Nchi kwanza then utatupa pia maslahi yetu mengine ya kiuchumi kama Nchi.
Kama Wanaharakati na wana Chadema wanaendelea kudhani kuwa wanaweza "kutumia"Nchi flani flani kubwa huko duniani kutekeleza programu zao za Political Terrorism ndsni ya Tanzania nadhani ziara ya Mh Rais URUSI IMEWAVURUGA😁
Mfano mwingine ni huu mgogoro wa Mkondo bahari wa Hormus pale Iran unaweza kukupa picha kuwa Geopoligical Diplomacy ndio msingi wa kwanza wenye kuweza kulinda maslahi ya Nchi yoyote ile duniani.
Nchi majirani na Iran(Middle East) ziliamua "kumaintain" ALLIANCE na jirani Iran kuliko kuungana kumpiga Tehran na hapa lengo lilikuwa ni kulinda maslahi yao kwanza ya Kiulinzi na Usalama wa kikanda (Geopolitical Security & Soverignity).
HITIMISHO.
Katika mfumo huu mpya wa Mahusiano ya Kimataifa-Mkakati(Geopolitical Diplomacy),Nchi yoyote kwanza inapaswa kulinda UHURU wake kabla ya kulinda Maslahi yake ya kiuchumi.
Planners wa ziara hii ya Mh Rais Samia URUSI wamekuwa na "akili mingi" sana na automatically inazima matishio ya awali dhidi ya Uhuru wa Nchi yangu Tanzania.
Tanzania Kwanza.🇹🇿🇹🇿🇹🇿