Picha: Harambee ya M4C yavuna milioni 323 za kitanzania jijini Dar

Mbowe haitatokea nyinyiem mumrudishe kijijini labda Mungu kupitia mipango yake, baba yake Mbowe alitoa pesa kumchangia Nyerere aende U.N.
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema hakiogopi yaliyompata Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Dk. Stephen Ulimboka ambaye alitekwa, kuteswa na kutupwa katika msitu wa Mabwepande, jijini Dar es Salaam, Juni mwaka huu.

CHADEMA kimesema, wapenda mageuzi sehemu mbalimbali duniani, walikamatwa, kuteswa na kuuawa, lakini tawala kandamizi hazikufanikiwa kuzima mabadiliko yaliyokuwa yakihitajiwa na wananchi.

Kauli hiyo ilitolewa juzi usiku na Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe, katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, wakati wa harambee iliyoandaliwa na vijana wa chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam waliofanikisha kupatikana kwa zaidi ya milioni 500 kwa ajili ya vuguvugu la mabadiliko (M4C) ambapo sh milioni 270 ni fedha taslimu na ahadi sh milioni 253.

Mbowe aliwataka wananchi kutoogopa yaliyomkuta Dk. Ulimboka ambaye inadaiwa alifanyiwa kitendo hicho cha kinyama na watu wanaodaiwa kutoka Idara ya Usalama wa Taifa kwa lengo la kumdhibiti asiendelee kuwashawishi madaktari kugoma.

Alisema, mabadiliko yoyote yanahitaji usajiri, hivyo ni vema wananchi wakajiandaa na matukio yoyote kwa sababu serikali haioneshi nia ya kutatua kero za wananchi, wala kusikiliza manung'iniko yao.

"Tuache woga ndugu zangu, mabadiliko tunayotaka yanaweza kupatikana kwa njia ngumu, sisi hatuogopi yale yaliyomkuta Dk. Ulimboka, tunaamini mageuzi yatapatikana muda si mrefu," alisema.

Mbowe alisema, CHADEMA haitachukua nchi kwa kutumia mtutu wa bunduki wala maandamano, bali vuguvugu la mabadiliko (M4C), ndilo litakalofanikisha azma hiyo.

Aliongeza kuwa, CHADEMA kimejipanga kwa hilo kutokana na kuwa na dhamira yake ya kweli na akili walizojaaliwa na Mungu katika kuwatafutia ukombozi Watanzania.

"Nchi hii tutaingoza vizuri… tutawakomboa Watanzania, hatuwezi kumuachia mtu kuongoza nchi wakati hawezi kusimamia rasilimali za taifa, hawezi kusimamia madini wala gesi, ufisadi wa kutisha, ni lazima kufanya mabadiliko ya kweli ili nchi iweze kusonga mbele, tuwaachie urithi mzuri watoto wetu, CCM ni lazima waondoke," alisema.

Mbowe alisema, wananchi wanatakiwa kuungana pamoja na kuondoa woga ili kujenga taifa bora na kupata ushindi mnono katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Alisema, hivi sasa hawezi kuzungumzia kama anagombea ubunge wala urais kwa sababu haongozi kundi au genge la watafuta vyeo na madaraka, bali kundi la watu wanaopenda mabadiliko.

Kipaumbele cha CHADEMA
Alisema endapo CHADEMA itaingia madarakani, kipaumbele cha kwanza hadi cha tatu, kitakuwa ni elimu kwa sababu CCM haijaipa uzito mkubwa kwa makusudi.

Mbowe alisema, CCM imefanya hivyo kwa kuwa inataka watu wawe wajinga ili wapate mwanya wa kuendelea kuwatawala kwa urahisi.

"Serikali ya CCM imewadumaza Watanzania na kuwafanya kuwa masikini wa akili kuliko rasilimali kwa kuwa, waliona wakiwasomesha watailinda dhahabu na rasilimali nyingine muhimu ambazo zitawasaidia kupambana na umasikini," alisema.

Aliongeza kuwa, endapo CHADEMA itaingia madarakani, itakuwa na fursa ya kusilikiza matatizo ya walimu, kuwasikiliza madaktari na hata wafanyakazi katika sekta nyingine ili kuhakikisha kila Mtanzania anaishi maisha bora.

Michango ya kuing'oa CCM
Katika harambee hiyo ya juzi iliyoandaliwa na vijana wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kukiwezesha chama hicho kufikia azma yao ya kuingia madarakani mwaka 2015, zaidi ya sh milioni 500 zilipatikana.

Wanachama na wapenda mabadiliko kutoka katika mikoa mbalimbali pia walishiriki kwenye harambee hiyo kwa njia ya simu na kutuma fedha, na wengine waliahidi kuziingiza katika akaunti ya M4C ili kuimarisha harakati za vuguvugu hilo la mabadiliko.

Mara baada ya kukamilisha harambee hiyo, aliyekuwa Mbunge wa Arusha, Godbless Lema alitangaza kiasi cha fedha zilizopatikana kuwa ni sh milioni 385 ambazo hazijajumlishwa na fedha zilizochangwa katika mitandao ya simu.

Aidha, alisema Oktoba mwaka huu wanachama wa CHADEMA wanaoishi nchini Uingereza, watakipatia chama hicho magari manne aina ya Canter na ifikapo Desemba watatoa helikopta kwa ajili ya kusaidia harakati hizo.

Pia, alitaja namba za akaunti za M4C kuwa ni pamoja na 01J1080100600 kuchangia kwa maana ya ukombozi wa nchi.

Mwenyekiti wa M4C, Alex Mayunga alisema, fedha hizo zitatumika kununulia magari pamoja na vifaa mbalimbali vitakavyofanikisha kampeni na kutangaza chama nchi nzima kuhakikisha wanashinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

SOURCE: Hapa CHADEMA: Hatuogopi ya Dk. Ulimboka
 
Ndio maana nimekuambia toka mwanzo, habari za vijiweni usizilete hapa JF, zipeleke kwa hao hao wanywa gongo!!
CCM haina mamlaka ya kumruhusu mtu avoid au ku evade kulipa kodi. TRA ndio wasimamizi wakuu wa mapato Tz na wala siyo CCM! TRA hamwana mamlaka ya kumnyanya mtu cuz eti siyo CCM! Ingekuwa ni hivyo akina Sabodo,Ndesamburo na Slaa wasingekuwa wanafanya biashara.

Cha muhimu ni wewe mlipa kodi kuhakikisha unacomply na tax laws. Na kwa sasa wananchi wengi wapo aware sana na masuala ya kodi.
Kwani TRA ipo chini ya serikali ya Chama gani?
 
Kumbe zilipatikana mil 300 tu??? Pamoja na promo yote, kama wameshinndwa kufikisha lengo la mil 500 walilokuwa wameliweka, vivyo hivyo na 2015 kura hazitatosha!!

Anaza kutafuta pain killers na dawa za pressure. Nahisi utapata matatizo.
 
Hivi milioni 70 unaweza kupata Chopa mbili na magari 100? Ninavyojua bei ya Chopa moja ni dola 300,000.
 
Kumbe zilipatikana mil 300 tu??? Pamoja na promo yote, kama wameshinndwa kufikisha lengo la mil 500 walilokuwa wameliweka, vivyo hivyo na 2015 kura hazitatosha!!

hizo M 300 nyingi ni ahadi...
 
Tafrija ilifanyika Dar vipi wale wadau wakubwa wa Chadema ndani JF akina molemo, Gwalihenzi, Mwita Maranya na Aweda mjumbe wa mkutano mkuu wa taifa mlialikwa au mnuso ndio ilikuwa kwa kujuana neema za M4C ziwe kwa wote wasio wengine mtoke povu la mdomo kutetea kundi walaji na huku hamnufaiki na ulaji wenyewe. Nimepitia picha siwaoni na watu hawakuwa wengi kiasi hicho.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
RITZ je million 70 huioni bali unatamani million 500 nitakucheki baadae
A%20S%20465.gif
 
mkuu nngu007 cash ni milioni 270 na ahadi 253milioni, kwahiyo wamevuka lengo la kupata milioni 500 kwa mkoa wa DSM, halafu mbona mlolongo wa picha zote sijaona picha ya kamanda Lema.
 
Last edited by a moderator:
Wakati ccm wakitaget kuiba mafao ya watumishi sisi tunachanga senti zetu na hadi kufika 2015 tutakuwa na pesa nyingi tu
 
Tafrija ilifanyika Dar vipi wale wadau wakubwa wa Chadema ndani JF akina molemo, Gwalihenzi, Mwita Maranya na Aweda mjumbe wa mkutano mkuu wa taifa mlialikwa au mnuso ndio ilikuwa kwa kujuana neema za M4C ziwe kwa wote wasio wengine mtoke povu la mdomo kutetea kundi walaji na huku hamnufaiki na ulaji wenyewe. Nimepitia picha siwaoni na watu hawakuwa wengi kiasi hicho.

Chama
Gongo la mboto DSM

Mkuu chama,
Hao ni Chadema-Kata wanatumika kwenye maandamano na mitandao ya kijamii lakini M4C ina wenyewe kina Mbowe, Slaa, Lema...hata wabunge wa Chadema kutoka Meatu, Ukerewe, Bariadi, Rukwa, hawakualikwa.
 
Last edited by a moderator:
Hivi milioni 70 unaweza kupata Chopa mbili na magari 100? Ninavyojua bei ya Chopa moja ni dola 300,000.

I'm sure popote alipo Zitto atakuwa anacheka sana, haiwezekani kumchukua mwenyekiti wa taifa na kufanya maandalizi ya milion 40 kisha mkakusanya milioni 70.
 
Lengo ni kupata bilioni 5 lakini wamepata milioni 70 pamoja na ahadi, kama Dar mlipanga kupata milioni 500 ndio sehemu mliokuwa mnaitegemea lengo limekwama...sasa unakwenda kumualika Sinta na Joketi unategemea nini.

Ritz,
Acha dharau especially mwezi huu wa ramadhani, Jokate na Sinta si watu?

Je Jokate hajaalikwa kama mhamasishaji kwenye mabalozi wa Elimu wa taasisi ya TEA ?

Akitoa Sabodo mnapiga kelele, huko kilombero wanachangia mia mia mnazipigia kelele,

Haijalishi nani anachangia, mradi kazipata kihalali basi muwaache watu wachangie,

CCM inachangiwa sana mpaka sasa na haibagui wanaowachangia, vijana ndio wamefurika hapo ....nafahamu CCM ikitaka hata 80bn watapata na watu wataomba kuchangia bila kificho chochote maana wanajua zimwi likujualo....

Ni ukweli usiopingika ukitaka ajira yako ikae vizuri join the team on power ...lakini nakuhakikishia not for long, mimi nimetuma mchango wangu thru MPESA ya mlinzi ili nijinusuru kibarua changu , tulifuatilia kwa umakini sana watumishi zaidi ya 55....

Mmechokwa , hamna mvuto, vijana tutawatoa maana nguvu ya CDM ni vijana wa vipato vya kati...waje wengine tuone angalau for ten yrs hiyo itawapa akili mjipange kurudi na kuacha ulaghai na vitisho mbuzi, ujumbe nakupa huo

Mwisho kabisa, ningependa kujua kama umefunga na unashika kwa uthabiti maandiko matakatifu, maana dini yenu haifundishi kubeza na kudharau wengine

Ninafahamu sasa utaanza kutumia hizi pictures za akina jokate na mbowe, kujibu mapigo ya JK na akina Millen Magese (tofauti nadhani JK asks for Beck's photo for nothing, whilst Mbowe's pic was for 50k )
 
Back
Top Bottom