Mungu kama upo kweli na unawaona hawa jamaa wakiendelea kutuibia raslimali zetu kwa kulindwa na majeshi yetu Mtwara kwa kweli tunasikitika tunakuomba MUNGU ufanye Jambo ili kutuokoa na hali hii. Mungu uliweza kuwavusha wana wa Israeli kutoka utumwani Misri, sasa nasi hatuna cha kusema tunakuomba utuonyeshe jambo moja tu kabla mwaka haujaisha huu, Sasa tumefikishwa mahali ambapo hatuwezi vumiliatena wakati wao wakipanda ndege na kuwapokea wanyang'anyi kwa jina zuri la wawekezaji. EE MUNGU SIKIA KILIO CHETU.
Acha kumsumbua Mungu wetu wewe; ulichagua mwenyewe, ukashangilia mwenyewe. Tulia kama upo kwa kinyozi. Walipogoma madaktari ukasema wanatetea maslahi yao.
Jiulize, kama ungekuwa Daktari wa zamu. Ukaingia wodi kama hii; ungefanyaje? Ukiwapa discharge wote wakafie kwao unaambiwa wewe si mwadilifu. Kipi bora? Mtu anakuja na ugonjwa wa homa anaondoka na TB. Mwingine anaondoka na ukurutu wa kutisha. Wakikataa madaktari tujue wameyaona tofauti na walivyofundishwa.
Tumwombee Mungu ulinzi Ulimboka wa watu, aliyaona haya moyo wake ukamsuta, akatuambia tukamwona mroho. Mungu tu atusamehe. Serekali yetu Tukufu yenyekusikia kilio, hebu tubadilishe tena vipaumbele vyetu.
Tusitishe kidogo barabara tujenge hospitali mpya moja tu yenye vifaa bora kwani kila mtu Tanzania ni mgonjwa fulani hivi.
Tunamkumbuka babu wetu wa Loliondo jamani. Laiti tungekuwa na hospitali yenye Mabingwa wote mahali pamoja. La Loliondo lingekuwa cha mtoto
