Picha: Bodaboda na Simba uso kwa uso

Picha: Bodaboda na Simba uso kwa uso

Simba alikuwa kashiba...suppose angekuwa na njaa au angekuwa na watoto! Sipati picha.
 
ukisikia ana kwa ana na simba ndio kama hivi. Mwendesha Bodaboda ni mwenye bahati mno loh
 
huyo boda boda akafanye sala ya Toba..
la sivyo angesha R.I.P
hivi hiyo pikipiki ingegoma kuwaka ingekuwaje?
hivi huyo Simba angenguruma tu hali ingekuwaje? huo mngurumo wake angepata hata ufahamu wa kuwasha pikipiki?
 
Ilitokea ghafla katika barabara ya Makongolosi kuelekea Rungwa mkoani Mbeya. Ghafla kwenye kona mnyama simba kakutwa kajipumzisha katikati ya barabara eneo la pori la simba.

Wakati magari yakiwa yamesimama, mara Bodaboda akatokea na bila kujua akataka kuyapita kwa kasi (kuchepuka) ndipo alipokutana uso kwa uso na mnyama huyo hatari. Hata hivyo aliweza kugeuka na kukimbia wakati na simba naye akanyanyuka na kuingia porini.


View attachment 227826View attachment 227827View attachment 227828

Inaonesha simba nae amekuwa confused na helmet ya mwendesha bodaboda. Kwani ameona sio kichwa cha kawaida cha mwanadamu.

Ila mwenye bodaboda sio mwoga, ingekuwa wewe si ungeachia hiyo bike na kulala mbele!!
 
Hata hivyo Simba alipoangalia kofia gumu hilo alidhani askari wa game. Hata kama angemvamia kichwani angeng'ata wapi.
 
Hapo angekuwa nyara mwenzake masai simba angetimua mbio za hatari,anajuaga muziki wa yero.
 
Hapa ningekuwa mimi ningezimia aisee maana muoga kinyama, mnyama mwenyewe simba!! Nilishawahi kukutana na kitimoto pori asubuhi asubuhi saa 12 wakati nakusanya kuni za kupika chai,

siku hiyo nakumbuka miguu iliishiwa nguvu nikaanguka chini bahati nzuri nilikuwa na ba'mdogo wangu akapiga ukunga ndio noah akasepa.

Samahani LUGHA gongana hapa: kupiga ukunga maana yake nini? Au ndo kupiga yowe/mayowe?
 
Hapa ningekuwa mimi ningezimia aisee maana muoga kinyama, mnyama mwenyewe simba!! Nilishawahi kukutana na kitimoto pori asubuhi asubuhi saa 12 wakati nakusanya kuni za kupika chai,

siku hiyo nakumbuka miguu iliishiwa nguvu nikaanguka chini bahati nzuri nilikuwa na ba'mdogo wangu akapiga ukunga ndio noah akasepa.
.........Mkuu, maeneo gani hayo ulipokutana na Kitimoto pori asubuhi asubuhi na mimi niende kuokota kuni? Daah, nimechoka kula nyama ya kitimoto wa kufugwa lol!!.
 
Ndivyo walivyo vihere here huwa vinawaponza sana

Pamoja na ya kwamba Wanyama kama simba hawazoeleki, ila kwa watu kama hao wa bodaboda wanaopita hiyo sehemu kila mara wameshazoea hayo mazingira, ni tofauti na sisi wa huku mujini.....ningekuwa mimi ndio naendesha hiyo bodaboda ingezimika ghafla na isingewaka tena.....ningeduwaa....ila mcheki huyo jamaa, yuko cool tu! Wanajuana hao.....
 
Watoto wa mjini mnaogopa hata sungura itakuwa simba, sisi wa bush ni kawaida tu, utaogopaje mali asili?
 
Picha ya kutengeneza hakuna ukweli wowote mpiga picha alikuwa kwenye ford xlt angalia wiper zinapoishia eti napikipiki imeonekana na engine gari liko juu angemuona kwa chini sasa wapo kima kimoja na gari....zakuambiwa changanya na zako..Jkikwete.

Aliinuka akapiga hiyo picha kwa uzuri. Whatever the case, ni picha ambayo imetufurahisha wachangiaji, na wachangiaji wamechangia na kutoa changamoto,angalau tumeongeza dakika kadhaa za maisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom