Picha: Bodaboda na Simba uso kwa uso

Picha: Bodaboda na Simba uso kwa uso



Nawashukuru kwa michango mizuri. Hiyo ni picha halisi ya tukio.

Naunga mkono hoja hata mimi nilikuwepo kwenye huo msafara wa magari mawili wala si photoshop kama wengine wanavyotaka kuamini!
 
Boda Boda huyo alirudi tena njia hiyo hiyo huku akiwa amembeba abiria! Mimi nilikuwa mmoja wa watu waliokuwa kwenye huo msafara wa magari mawili na ndio tulioshangazwa na hilo tukio tukaamua tupige picha hiyo. Aidha, hakukuwa na purukushani yoyote kati ya Simba na Boda Boda!
Huu uwongo haufanani ukweli kwa hiyo aliondoka akarudi tena akawakuta nyie mnasubiri dereva mwingine apite mpige picha?
 
Huyu jamaa haikosi alijisaidia haja kubwa kwenye suruali,na sipati picha speed baada ya kugeuza😀😀
 
Tunashukuru Afisa wa Wizara ya UJENZI ENG NTEMO MARTIN kwa kuweza kukata vizuri picha hizo katika msafara wa ukaguzi wa barabara
 
Kizimbuzi bhana sasa picha si hizo unaziona, anyway waendesha boda hawafikiliagi mara mbili
 
Hapa ningekuwa mimi ningezimia aisee maana muoga kinyama, mnyama mwenyewe simba!! Nilishawahi kukutana na kitimoto pori asubuhi asubuhi saa 12 wakati nakusanya kuni za kupika chai,

siku hiyo nakumbuka miguu iliishiwa nguvu nikaanguka chini bahati nzuri nilikuwa na ba'mdogo wangu akapiga ukunga ndio noah akasepa.

Mkuu nimecheka sana na kuishiwa pozi kusema kuwa miguu iliishiwa nguvu, na huyo ni nguruwe pori, simba si kweli ungezimia kabisa.
 
Ila watu wanakosea sana kujumuisha boda boda wote kwenye kapu moja! Kuna bodaboda wengi tu wana busara kuliko hata hao wanaoendesha magari hususani wale wa vijijini.
 
Ila watu wanakosea sana kujumuisha boda boda wote kwenye kapu moja! Kuna bodaboda wengi tu wana busara kuliko hata hao wanaoendesha magari hususani wale wa vijijini.

Waendesha bodaboda wote wana akili za kichina kama hizo bodaboda wanazoendesha
 
Waendesha bodaboda wote wana akili za kichina kama hizo bodaboda wanazoendesha

Wewe ungekuwa na akili ya kichina si ungeringa? Mnawadharau wachina wakati kutengeneza baiskeli hamuwezi. Wabongo bwana!!!
 
huyu simba atakuwa ameogopa hiyo helmet ya dereva wa bodaboda.
 
We mtu unapikipiki unaogopa simba! kwani pikipiki na simba nanianakimbia zaidi?
 
Aende kwenye nyumba ya ibada akamshukuru Mungu kwa kumuepusha na balaa...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom