Picha: Bodaboda na Simba uso kwa uso

Huyu bodaboda kifo kilikuwa kimeshamwita
 
hahahahaa! mkuu vp mlimchunguza vizuri huyo jamaaa wa bodaboda.....maana hapo lazima alijikojolea tu kama siio kujiny*a....huyo mnyama kasheshe lake ni zito balaaa
 
Kwenye nchi za wenzetu hii ni bonge la picha mkuu. ukiwa mchanja iwekee copyright la sivyo wajanja watachukua fursa.
 
Hawa boda boda sijui akili zao nani kazishika,wewe ushaambiwa ilo pori linaitwa "pori la simba" na yeye anakatiza na boda boda.

Mkuu ilo pori la simba kwanini wasiweke vibao vinavyoonyesha hatari kupita hapo kwa miguu au na boda boda?
 
Ha ha ha haaaaaa tehtehtehtethe mtoa mada leo umefanya siku yangu iwe nzuri nimecheka mpaka nimelia
 

Hoja yako ni nzuri sana...lakini unawafahamu vizuri waendesha bodaboda wewe...!!?? Hawa jamaa mostly ni wabishi na muchknows.
Unaweza mpa ishara zote na bado akakuona pimbi tu...Uliza madereva wenzako wanaopambana nao barabarani kila siku ndo utajua tunachokisema...
Lakini pia inategemea alikuwa na mwendokasi kiasi gani...!!

Tafakari...
 

Mkuu we kama ni dereva wala usingesema hivyo... Patience barabarani ni muhimu sana kwa dereva yeyote makini lakini umeshuhudia wangapi wanasababishaa ajali kwa kujifanya wanaharaka na kuona wengine wote wajinga tu?

Na hawa wabodaboda unadhani wanamuda wa kusubiria hata ukimuonesha ishara wakati upenyo wa kupita yeye anauona? Au ulitaka washuke wamsimamishe?

Na wengine hata honi za magari hawaziskii wanavaa earphones sasa utawasaidiaje na wao wanajiona professional?
 
ha ha ha akifika kijiweni lazima ajikague haja kubwa/ndogo zilimtoka si bure
 
Hivi kilicho mpa huyo simba ujasiri ninini maana gari liko mbele yake haliogopi na hio pikipiki ilivyomsogelea hata hakuogopa, sijui wana nini hawa
 
Jamaa wa bodaboda uko aliko atakuwa haamini anaona kama ndoto vile.
 

Khaaa.. mbele ya simba utatoa mkono? Si ajabu hata waliokuwemo kwenye hilo gari hali ya hewa ilichafuka...Kukutana na simba maeneo ambayo hukutegemea sio mchezo. hao jamaa wa bodaboda unawafahamu au unawasikia? Wana akili zinazowatosha wao tu, kama hawajali trafic light itakuwa taa za gari?
 
Ashukuru huyo simba pengine ni mzee au ni mgonjwa, angepata cha mtema kuni.
 
Hahahhaa animecheka sana sana ila ni hatareeeeeee, sipati picha jinsi alivyofunga breki dah, kifo sijui kina siri gani aiseee

Nina Uhakika Iwe Isiwe Alipofunga Tu Breki Lazima Alijamba Na Kutoa Kidooooooogo Big Haja Na Nahisi Alipofika Kwake Breki Ilikuwa MSALANI.
 

Inaonekana hujawahi kuendesha gari mijini. Hawa jamaa(boda boda) huo muda wa kuangalia "indicators" za gari mbele yao achilia kuheshimu sheria za barabarani na vitu kama hivyo hawana,

Ndio maana utazikuta pikipiki(zimeharibika) kama mlima kwenye vituo vya polisi, na wamelezwa pale muhimbili kama utitiri na ma "antena" kila mahali, tena chini.

MucheTZ
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…