PICHA: Athari za mvua jijini Dar es Salaam

PICHA: Athari za mvua jijini Dar es Salaam

usilaumu chama(CCM),hizi picha inabidi zitengeneze tangazo la kuhamasisha watu kuhama mabondeni.
 
Welsaid, hata hivyo si serikali tu ya kulaumiwa, wananchi ndio wenye kubeba zaidi lawama pamoja na udhaifu wa serikali. Binafsi ninapohitaji kujenga huwa ninaangalia mengi likiwemo hilo la mafuriko.

Nilitafuta kiwanja cha kujenga Morogoro, nikapata serikalini bila taabu cha low density, kilikuwa kipindi cha kiangazi ambapo maeneo mengi yamepimwa sehemu hiyo. Lakini nilipofanya uchunguzi wa kina niliona kiwanja hicho kina mchanga mwingi sana na katikati kumepita mkondo unaoonyesha dalili kipindi cha masika kuna maji yatokayo mlimani yanapita hapo kwa kasi. Pamoja na kwamba niliridhia kiwanja hicho lakinin nikabadili nia na kukiacha auziwe mwingine sababu ya dalili nyingi za mafuriko ingawa ni ya kupita kwa muda kwa kuwa kiko kwenye muinuko kidogo.

Anayesumbuliwa na mafuriko si serikali bali ni yeye aliyeamua kujenga hapo, hivyo makosa ni pande zote.

Bado hilo ni kosa la watendaji wa serikali (surveyors na planners). Wao ni wataalam waliosomea kazi hiyo ya kupanga makazi salama. Ni jukumu lao kumpatia mwananchi eneo salama la kuishi na ndio maana utapewa hadi na hati ya umiliki. Kama sehemu uliyoolipewa na wataalam sio salama kwa maisha na mali za mkazi huo ni uzembe wa watendaji kwani wana elimu na utaalam wa kubaini hilo. Kwa wewe mteja kulitambua hilo ni curiosity yako tu na yuke ambaye hakuweza kulibaini hapaswi kulaumiwa kwani kwanza siyo lazima awe na utaalamu huo lakini pili alishahakikishiwa hadi kupewa hati kuwa sehemu hiyo ni stahili kwa makazi
 
Huu ndio muda sahihi wa kwenda kuangalia maeneo ya kununua viwanja ili usije ukauziwa mbuzi kwenye kiroba.
 
Tatizo lenu mnaokaa dar ni kung'ang'ania kujenga maeneo ambayo ni mabondeni na serikali wakiwakataza ndio mnaanza kulalama.
Wakati mnachukua viwanjwa mnaambiwa msijenge mabondeni leo yamewakuta mnalaumu serikali haiwasaidii haya sasa kazi kwenu na serikali yenu
 
Tokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbali mbali ya Dar es Salaam, zimepelekea uharibufu wa barabara na mazingira.

Haya ni maeneo ya jiji la Dar es Salaam yaliyoathirika na mvua inayoendelea kunyesha na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi hasa wanaoishi bondeni au kwenye mkondo wa maji mfano mito.




attachment.php


attachment.php


Aprili 12, 2014

Duh! majanga jameni poleni wana Dar es Salaam lakini muekeze kwenye drainage systems na city planning. Sio kujenga tu maana kwenye picha hizi naona pia hata prime areas zilizoadhirika pia. CC kadoda11 Geza Ulole
 
Last edited by a moderator:
Kuna wakati aliekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mzee Makamba aliwakemea watu wanojenga kwenye mabonde,namnukuu "hivi nyie watu mnaopenda kujenga kwenye mabonde ya mito mmekuwa vyura?" Tatizo hapa sio CCM, tatizo ni watanzania tumekuwa wabishi, hatuwasikilizi viongozi wetu mpaka maafa yatokee ndo tunaanza kuliaumu serekali! Walishaambiwa siku nyingi hawa lakini wamekuwa viziwi na sasa wanavuna walichokipanda. Ukweli ndo huo na unauma.

Kuna mtu leo nilisikia akisema wana-ccm wengi hawana akili ya kujitegemea,most of them ni ignorance with high degree of poverty.SIKUAMINI NIMEKUJA KULITHIBITISHA HAPA KWENYE COMMENTS ZA WATU.
 
Hapana, nyumba hazipo majini, maji ndo yapo nyumbani

No,kuna wengine wamejenga sehemu sahihi ila kuna watu wengine wamejenga katika njia za maji hivyo mvua zinaponyesha maji yanakosa pakuelekea
 
Back
Top Bottom