WanaJF,
Binafsi uwa nafanya judgment kwa mtu kwa kuzingatia kiwango chake cha elimu. Siku zote.
Tangu zamani nilimdharau Mbowe kwa kuwa ni kijana aliyepata sifuri kwenye mitihani ya kidato cha 6 ilhali alikuwa na dhana zote za kuweza kumfanya afaulu vizuri!
Katika hali kama hiyo, baada tu ya kupewa uenyekiti CHADEMA, niliamini kwa 100% chama kitaelekezwa kuzimu. Na leo yametimia.
Ila kikubwa kilicho nipelekea kuandika huu uzi, ni baada ya kuona Prof Lipumba na wasomi wengineo kukubali kuongozwa na mtu kama Mbowe. Kweli!!!?
Lakini ukitazama sababu hasa ya mtu msomi kama Prof Lipumba, pamoja na mambo mengine, utagundua kuwa amekubali kudhalilika kisa maslahi binafsi. Hilo liko wazi.
Prof Lipumba please honour your doctorate. You can not bow to someone like Mbowe. He's too low for u.
Hamy-D,Ninapopata nafasi huwa napitia jamii forum ili kupata habari kama ninavyopata habari kupitia vyombo vingine kama Tv,radio na magazeti.Kinachonisikitisha na kunisononesha ni pale ninapokuta mtu badala ya kuweka habari anatapika humu jamii forum-Huwa ninatamani sana kumjua physically mtu huyo kwani huwa inanishanganza ni kwanini anaamua kujizalilisha.
sasa nirudi kwenye hoja.Hivi elimu ni nn?
Kwa uelewa wangu elimu ni -Maarifa aliyonayo mtu katika jambo fulani+Uwezo wa mtu kufanya tafakuri na tafakari ya mambo,Uwezo wa kutetea kile anachoamini,Uwezo wa kumudu mazingira yanayomzunguka (Kuzuia mihemko) uwezo wa kujiamini,kujieleza na kuwaelekeza wengine lile unaloliamini na wakakuelewa na siyo vyeti.
-Uongozi na Elimu(wingi wa vyeti) ni vitu viwili tofauti
-Kikwete ni Rais wa Tanzania-Je ndiye Msomi wa Juu kabisa nchi hii?
-Jenister Mhagama-N/W-Elimu ndiye Msomi mkubwa Kabisa pale Wizara ya Elimu
-Nape,Kinana,Mwigulu ndio wasomi nguli kabisa pale ccm
na je zile familia ambazo mama anaelimu(Vyeti vingi kuliko baba)Je baba anakuwa amepoteza sifa ya kuwa kichwa cha Nyumba?
-Angalia Dr.Michael pale kwenye BMK pamoja na vyeti vingi mpaka cha PhD unaweza ukamwita anaelimu?Mtu aliyeshindwa kumudu mazingira(Kuzuia mihemko pale BMK) while watu wenye vyeti vichache wameweza kuyamudu.
-Je kiongozi wako wa Mtaa,Kanisa au Msikiti ana vyeti vingapi?mbona anakuongoza.
Hamy-D unatuzalilisha wana ccm bwana-Kuwa mwana ccm haina maana akili yako iwe likizo throughout the year.