Peter Mwakatundu, nakutafuta rafiki

Ugumu wangu

JF-Expert Member
May 6, 2021
1,685
3,549
Wakuu habari za mida hii,

Naomba kwenda kwenye maada tajwa hapo juu:

Namtafuta mtu huyu kwa Jina lake halisi ni Peter Mwakatundu nimepotezana nae miaka kadhaa nyuma, kwa kumbukumbu ya machache ninayokumbuka.

Tuliwahi abudu pamoja nae kwenye kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), pale kilimani Barabara ya kwenda Pugu station na mnada wa Ng'ombe, mchungaji wa kanisa kipindi hicho sijui kwa Sasa aliitwa Kibona mfupi mweusi na huyu, Peter alikuja pale Kama mwalimu wa chekechea na baadae akateuliwa kuwa mhasibu wa kanisa.

Pia aliwahi kufungua kituo Cha Tuition center gongo la mboto kipindi hicho ilikuwa nyuma ya kituo Cha police, haya ni machache nakumbuka alikuwa mtu wa karibu sana kwangu na rafiki mkubwa sana tulikuja kupotezana wakati nimeenda kuanza kidato Cha tano Arusha sikuonana nae Tena maana hatukuwa hata na simu kipindi hicho.

Nakuomba popote ulipo au Kuna mtu wa karibu anamfahamu naomba mjulishe rafiki yako kijana wa kinyaturu tokea Singida, alikuwa rafiki yako na hata siku ya kuondoka alikuachia suruali moja ya blue bahari chini mbwaga.

Kidogo na Bible mwambieni namtafuta popote si kwa ubaya Ila nimekumbuka mengi mno, akumbuke pia tukio moja la kuokota pesa za machange ya shilingi ishirini tu kwenye mfuko wa rambo jumla zikiwa elfu 6 tukaenda nazo kanisani kuziombea na tukaenda kulia chips pale mwisho wa lami gongo la mboto.

Peter Mwakatundu ana ndugu yake ni mjeda wa cheo kizuri kule Kigamboni pia akumbuke alienda kunitambulisha kwa ndugu yake huyo kwa sasa sipakumbuki hata Nyumba tulienda.

Peter nakutafuta, nakutafuta sana kama upo hai nakutafuta mno nimekutafuta social media zingine nimekikosa hadi nimeamua kuja hapa pia tafadhali Kama unamjua mkumbushie tu kwa kumbukumbu hizi na mwambie namtafuta Sana.
 
Hi
Screenshot_20210826-171457_Facebook.jpg
 
Back
Top Bottom