Peter Msigwa apiga mil. 200 za Lowassa, Iringa Mjini mpo?

Peter Msigwa apiga mil. 200 za Lowassa, Iringa Mjini mpo?

Hv utajiri wa lowasa ni kiasi gani au ni tajiri namba moja afrika maana toka tusikie anahonga pesa ni muda mrefu sana , hzo pesa zake haziishagi ? Kama ana pesa kiasi hko bora tumpe nchi tuuu, afu note kwamba majungu cyo mtaji mi ni ccm ila tufike pahala tuwe tunaongea point bin haki
 
Watu nawashangaa sana mara lowassa kafanya hivi au vile. Sasa ww inakuhusu nn basi kama katoa mil 200 za mkutano? Na hao wanaotumia kodi zetu kwa ajiri yao
 
daah!! kwel dada uko kweny period, acha ungese..
utaolewa muda cyo mref alaf utaenda kumuhudumia mme wako, najua n kukosa kazi ndo mana unaanzisha uzi wa kmbea
 
mgombea wa kiti cha ubunge wa jimbo la iringa mkoani iringa kupitia chama cha demokrasia na maendeleo, peter msigwa anatarajia kutumia milioni 200 kuuandaa mkutano wa mgombea wa urais wa chadema/ukawa edward lowasa, unaotarajia kufanyika mwishoni mwa juma hili.fedha hizo zitakazotumika kuandaa maandamano ya vyombo vya moto muziki na posho kulingana na chanzo cha kuaminika ndani ya chama hicho kinasema kwamba kiongozi huyo amezipokea kutoka kwa edward lowasa ambaye amekuwa rafiki yake mkubwa licha ya hivi karibuni msigwa kumsema vibaya kwa kuwaambia wananchi kwamba kila atakayemuunga mkono lowassa akapimwe akili.hatua hiyo inakuja ikiwa ni wiki ya pili sasa tangu mbunge huyo alipopokea shilingi milioni 50 kama hongo kutoka kwa lowassa kwa ajili ya utengezezaji wa mabango makubwa ambayo yamewekwa kwenye mitaa mbalimbali mjini iringa.msigwa ambaye ameamua kukodi ukumbi wa baa ya sambala na kuufanya ofisi ya chama kutokana na ubovu wa ofisi ya chadema iringa uliopo mtaa wa mshindo ambayo ukiitaza haina tofauti na banda la kuku.mkutano huo unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa juma hili siku ya jumapili utatanguliwa na maandamano yakiongozwa na pikipiki, boda boda na watembea kwa miguu ambao wote wanatakiwa kulipwa sh 50000 kwa ushiriki wao.ambapo chanzo hicho kimesemwa kuwa kila bodaboda itagharamiwa mafuta pamoja na fedha kiasi cha shilingi elfu tano huku wengine wakilipwa elfu kumi.kuliona hili nimefika katika kituo cha bodaboda eneo la stendi kujua ni kiasi gani hulipwa kwa safari moja ya mgombea ambao wamesema "sisi! Kwa mimi huwa nalipwa shilingi elfu tano huwa tunalipwa shilingi elfu tano na kujaziwa mafuta fresh tu, ila tukiwambia atuongezee kiasi cha fedha anazinguaga yule" amesema mmoja ya madereva wa bodaboda eneo la kituo kikuu cha mabasi mjini hapa ambaye hakutaka jina lake kutajwa.sikuishia hapo nikakutana na madereva wa pikipiki za miguu mitatu wanaopaki eneo karibu na mwembetogwa kujua kiasi cha fedha ambacho hulipwa kwa maandamano ya mbunge huyo wamesema" hapa tunachukuaga ten ten tu, akijaza mafuta tunatembea" amesema mmoja wa madereva hayo" ( jina lake hakutaka liwe wazi.wakizungumza juu ya ushabiki wao kwa chama hicho madereva hao wamesema kwamba " wenyewe huwa wanasema ccm itashinda kwa kishindo mwaka huu lakini ukawa sisi huwa tunatafuta mkwanja tuu hakuna uchadema hapa."hata hivyo imebainika kuwa mil 200 hizo alizokabidhiwa msigwa ni kutokana na kumtetea lowassa wakati wa mada iliyorushwa channel ten ambapo polepole alizungumza kuhusu ulweli wa lowassa na msigwa akamtetea.bodaboda mjini iringa watalipwa sh 50000, bajaji 50000 huku madereva tax wakilipwa sh 100000 ili kuonyesha kwamba anakubalika.mkutano huo wa ukawa unataraji kutumia takribani mil 500 ili kufanikisha iringa mjini."sisi bodaboda kipindi hiki asipotupa chetu mapema ataisoma namba jimbo hili hajaliwekea hati miliki tutamtupa kapuni" alisema mmoja wa waendesha bodaboda
loh mamako atakuwa amesalimika kweli...
 
Acha wamlee an hisa nyng voda kiasi cha kulihujumu shirika ttcl wakati ilitaka kufufuka na Lain za kisasa wakaiua eti ed preside akaote
 
Hv utajiri wa lowasa ni kiasi gani au ni tajiri namba moja afrika maana toka tusikie anahonga pesa ni muda mrefu sana , hzo pesa zake haziishagi ? Kama ana pesa kiasi hko bora tumpe nchi tuuu, afu note kwamba majungu cyo mtaji mi ni ccm ila tufike pahala tuwe tunaongea point bin haki


Waende kwa Ritz wakope na wao wahonge badala ya kupandisha/kusomba watu kwa magari ya kokoto na michanga. Ebooh!
 
Mgombea wa kiti cha ubunge wa jimbo la Iringa Mkoani Iringa kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo, Peter Msigwa anatarajia kutumia milioni 200 kuuandaa mkutano wa mgombea wa urais wa Chadema/Ukawa Edward Lowasa, unaotarajia kufanyika mwishoni mwa juma hili.

Fedha hizo zitakazotumika kuandaa maandamano ya vyombo vya moto muziki na posho kulingana na chanzo cha kuaminika ndani ya chama hicho kinasema kwamba kiongozi huyo amezipokea kutoka kwa Edward Lowasa ambaye amekuwa rafiki yake mkubwa licha ya hivi karibuni Msigwa kumsema vibaya kwa kuwaambia wananchi kwamba kila atakayemuunga mkono Lowassa akapimwe akili.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni wiki ya pili sasa tangu mbunge huyo alipopokea shilingi milioni 50 kama hongo kutoka kwa Lowassa kwa ajili ya utengezezaji wa mabango makubwa ambayo yamewekwa kwenye mitaa mbalimbali mjini Iringa.

Msigwa ambaye ameamua kukodi ukumbi wa Baa ya Sambala na kuufanya ofisi ya chama kutokana na ubovu wa ofisi ya Chadema Iringa uliopo Mtaa wa Mshindo ambayo ukiitaza haina tofauti na banda la kuku.

Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa juma hili siku ya jumapili utatanguliwa na maandamano yakiongozwa na pikipiki, boda boda na watembea kwa miguu ambao wote wanatakiwa kulipwa sh 50000 kwa ushiriki wao.

Ambapo chanzo hicho kimesemwa kuwa kila bodaboda itagharamiwa mafuta pamoja na fedha kiasi cha shilingi Elfu tano huku wengine wakilipwa elfu Kumi.

Kuliona hili nimefika katika kituo cha bodaboda eneo la stendi kujua ni kiasi gani hulipwa kwa safari moja ya mgombea ambao wamesema "sisi! kwa mimi huwa nalipwa shilingi elfu tano huwa tunalipwa shilingi elfu tano na kujaziwa mafuta fresh tu, ila tukiwambia atuongezee kiasi cha fedha anazinguaga yule" amesema mmoja ya madereva wa bodaboda eneo la kituo kikuu cha mabasi Mjini hapa ambaye hakutaka jina lake kutajwa.

Sikuishia hapo nikakutana na madereva wa pikipiki za miguu mitatu wanaopaki eneo karibu na mwembetogwa kujua kiasi cha fedha ambacho hulipwa kwa maandamano ya mbunge huyo wamesema" hapa tunachukuaga ten ten tu, akijaza mafuta tunatembea" amesema mmoja wa Madereva hayo" ( jina lake hakutaka liwe wazi.

Wakizungumza juu ya ushabiki wao kwa chama hicho madereva hao wamesema kwamba " wenyewe huwa wanasema CCM itashinda kwa kishindo mwaka huu lakini Ukawa sisi huwa tunatafuta mkwanja tuu hakuna uchadema hapa."

Hata hivyo imebainika kuwa mil 200 hizo alizokabidhiwa Msigwa ni kutokana na kumtetea Lowassa wakati wa mada iliyorushwa Channel Ten ambapo Polepole alizungumza kuhusu ulweli wa Lowassa na Msigwa akamtetea.

Bodaboda mjini Iringa watalipwa sh 50000, bajaji 50000 huku madereva Tax wakilipwa sh 100000 ili kuonyesha kwamba anakubalika.

Mkutano huo wa Ukawa unataraji kutumia takribani mil 500 ili kufanikisha Iringa mjini.

"Sisi Bodaboda kipindi hiki asipotupa chetu mapema ataisoma namba Jimbo hili hajaliwekea hati miliki tutamtupa kapuni" Alisema mmoja wa waendesha bodaboda
Kumbe zinatumika vizuri kwa ajili ya maandalizi ya mkutano
 
Back
Top Bottom