Peter Msigwa apiga mil. 200 za Lowassa, Iringa Mjini mpo?

Peter Msigwa apiga mil. 200 za Lowassa, Iringa Mjini mpo?

Huu ni uongo mkubwa... CCM kwnn uongo ndio maisha yenu...😨😨👎👎

CCM ndio kazi yao... jpili iliyopita Dar hadi magari yanapita mtaa kwa mtaa, ila watu wamegoma wengi tu... na unapewa elfu 10,000 na t shirt ya CCM

Pia ma boda boda walipewa elfu 10,000 na kujaziwa mafuta bure full tank ktk sheli za BIG BON kkoo na PUMA fire Dar es Salaam...

Mtoa mada, acha upumbavu... mkutano wowote maandalizi hela lazima..

ila mikutano ya UKAWA, LOWASSA watu wanakuja wenyewe... kwa nauli zao...!!
 
Sasa kipi kinakuwasha, mwambie na makomeo afanye hayo afilisike. Uliona wapi kampeni bila hela, acha wehu
 
mgombea wa kiti cha ubunge wa jimbo la iringa mkoani iringa kupitia chama cha demokrasia na maendeleo, peter msigwa anatarajia kutumia milioni 200 kuuandaa mkutano wa mgombea wa urais wa chadema/ukawa edward lowasa, unaotarajia kufanyika mwishoni mwa juma hili.

Fedha hizo zitakazotumika kuandaa maandamano ya vyombo vya moto muziki na posho kulingana na chanzo cha kuaminika ndani ya chama hicho kinasema kwamba kiongozi huyo amezipokea kutoka kwa edward lowasa ambaye amekuwa rafiki yake mkubwa licha ya hivi karibuni msigwa kumsema vibaya kwa kuwaambia wananchi kwamba kila atakayemuunga mkono lowassa akapimwe akili.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni wiki ya pili sasa tangu mbunge huyo alipopokea shilingi milioni 50 kama hongo kutoka kwa lowassa kwa ajili ya utengezezaji wa mabango makubwa ambayo yamewekwa kwenye mitaa mbalimbali mjini iringa.

Msigwa ambaye ameamua kukodi ukumbi wa baa ya sambala na kuufanya ofisi ya chama kutokana na ubovu wa ofisi ya chadema iringa uliopo mtaa wa mshindo ambayo ukiitaza haina tofauti na banda la kuku.

Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa juma hili siku ya jumapili utatanguliwa na maandamano yakiongozwa na pikipiki, boda boda na watembea kwa miguu ambao wote wanatakiwa kulipwa sh 50000 kwa ushiriki wao.

Ambapo chanzo hicho kimesemwa kuwa kila bodaboda itagharamiwa mafuta pamoja na fedha kiasi cha shilingi elfu tano huku wengine wakilipwa elfu kumi.

Kuliona hili nimefika katika kituo cha bodaboda eneo la stendi kujua ni kiasi gani hulipwa kwa safari moja ya mgombea ambao wamesema "sisi! Kwa mimi huwa nalipwa shilingi elfu tano huwa tunalipwa shilingi elfu tano na kujaziwa mafuta fresh tu, ila tukiwambia atuongezee kiasi cha fedha anazinguaga yule" amesema mmoja ya madereva wa bodaboda eneo la kituo kikuu cha mabasi mjini hapa ambaye hakutaka jina lake kutajwa.

Sikuishia hapo nikakutana na madereva wa pikipiki za miguu mitatu wanaopaki eneo karibu na mwembetogwa kujua kiasi cha fedha ambacho hulipwa kwa maandamano ya mbunge huyo wamesema" hapa tunachukuaga ten ten tu, akijaza mafuta tunatembea" amesema mmoja wa madereva hayo" ( jina lake hakutaka liwe wazi.

Wakizungumza juu ya ushabiki wao kwa chama hicho madereva hao wamesema kwamba " wenyewe huwa wanasema ccm itashinda kwa kishindo mwaka huu lakini ukawa sisi huwa tunatafuta mkwanja tuu hakuna uchadema hapa."

hata hivyo imebainika kuwa mil 200 hizo alizokabidhiwa msigwa ni kutokana na kumtetea lowassa wakati wa mada iliyorushwa channel ten ambapo polepole alizungumza kuhusu ulweli wa lowassa na msigwa akamtetea.

Bodaboda mjini iringa watalipwa sh 50000, bajaji 50000 huku madereva tax wakilipwa sh 100000 ili kuonyesha kwamba anakubalika.

Mkutano huo wa ukawa unataraji kutumia takribani mil 500 ili kufanikisha iringa mjini.

"sisi bodaboda kipindi hiki asipotupa chetu mapema ataisoma namba jimbo hili hajaliwekea hati miliki tutamtupa kapuni" alisema mmoja wa waendesha bodaboda

twafaaaaaaaaaaaa
 
Mgombea wa kiti cha ubunge wa jimbo la Iringa Mkoani Iringa kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo, Peter Msigwa anatarajia kutumia milioni 200 kuuandaa mkutano wa mgombea wa urais wa Chadema/Ukawa Edward Lowasa, unaotarajia kufanyika mwishoni mwa juma hili.

Fedha hizo zitakazotumika kuandaa maandamano ya vyombo vya moto muziki na posho kulingana na chanzo cha kuaminika ndani ya chama hicho kinasema kwamba kiongozi huyo amezipokea kutoka kwa Edward Lowasa ambaye amekuwa rafiki yake mkubwa licha ya hivi karibuni Msigwa kumsema vibaya kwa kuwaambia wananchi kwamba kila atakayemuunga mkono Lowassa akapimwe akili.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni wiki ya pili sasa tangu mbunge huyo alipopokea shilingi milioni 50 kama hongo kutoka kwa Lowassa kwa ajili ya utengezezaji wa mabango makubwa ambayo yamewekwa kwenye mitaa mbalimbali mjini Iringa.

Msigwa ambaye ameamua kukodi ukumbi wa Baa ya Sambala na kuufanya ofisi ya chama kutokana na ubovu wa ofisi ya Chadema Iringa uliopo Mtaa wa Mshindo ambayo ukiitaza haina tofauti na banda la kuku.

Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa juma hili siku ya jumapili utatanguliwa na maandamano yakiongozwa na pikipiki, boda boda na watembea kwa miguu ambao wote wanatakiwa kulipwa sh 50000 kwa ushiriki wao.

Ambapo chanzo hicho kimesemwa kuwa kila bodaboda itagharamiwa mafuta pamoja na fedha kiasi cha shilingi Elfu tano huku wengine wakilipwa elfu Kumi.

Kuliona hili nimefika katika kituo cha bodaboda eneo la stendi kujua ni kiasi gani hulipwa kwa safari moja ya mgombea ambao wamesema "sisi! kwa mimi huwa nalipwa shilingi elfu tano huwa tunalipwa shilingi elfu tano na kujaziwa mafuta fresh tu, ila tukiwambia atuongezee kiasi cha fedha anazinguaga yule" amesema mmoja ya madereva wa bodaboda eneo la kituo kikuu cha mabasi Mjini hapa ambaye hakutaka jina lake kutajwa.

Sikuishia hapo nikakutana na madereva wa pikipiki za miguu mitatu wanaopaki eneo karibu na mwembetogwa kujua kiasi cha fedha ambacho hulipwa kwa maandamano ya mbunge huyo wamesema" hapa tunachukuaga ten ten tu, akijaza mafuta tunatembea" amesema mmoja wa Madereva hayo" ( jina lake hakutaka liwe wazi.

Wakizungumza juu ya ushabiki wao kwa chama hicho madereva hao wamesema kwamba " wenyewe huwa wanasema CCM itashinda kwa kishindo mwaka huu lakini Ukawa sisi huwa tunatafuta mkwanja tuu hakuna uchadema hapa."

Hata hivyo imebainika kuwa mil 200 hizo alizokabidhiwa Msigwa ni kutokana na kumtetea Lowassa wakati wa mada iliyorushwa Channel Ten ambapo Polepole alizungumza kuhusu ulweli wa Lowassa na Msigwa akamtetea.

Bodaboda mjini Iringa watalipwa sh 50000, bajaji 50000 huku madereva Tax wakilipwa sh 100000 ili kuonyesha kwamba anakubalika.

Mkutano huo wa Ukawa unataraji kutumia takribani mil 500 ili kufanikisha Iringa mjini.

"Sisi Bodaboda kipindi hiki asipotupa chetu mapema ataisoma namba Jimbo hili hajaliwekea hati miliki tutamtupa kapuni" Alisema mmoja wa waendesha bodaboda
Kwani wewe umelipwa sh ngapi kwa kuweka huu utetezi wako?
 
Elfu hamsini bodaboda??? Kwani bodaboda wana kura ngapi?! Hivi ule umati wa gongo la mboto ambapo alikwenda ghafla walipewa bei gani? Ikumbusheni tbc iwepo jangwani j'mosi hii ili kikwete asiwe tena chombo cha habari cha dharura kutuambia wamekwenda wangapi mkutanoni.
 
Mwaka Huu Ccm Ndio Watalalamika Kuibiwa Maana Nimeona Wameanza Mapema
 
Kila kitu cha Lowasana kwann ccm hatujiamini kwann tunamwogopa lowasa kwann tunampa umaarufu Sana kinachotakiwa ccm nikutoa majibu ambayo Lowasa ameuliza sababu ya kuoanda KWA sukari chumvi vibiriti nk ndicho wanachotaka walala hoi
 
CCM inalipa watu wengi kweli kuleta media propaganda. Siasa za kilofa kweli hizi.
Natamani ningemjua anayegawa hela za kupiga media propaganda ili na mimi nikachukue mpunga
 
Mgombea wa kiti cha ubunge wa jimbo la Iringa Mkoani Iringa kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo, Peter Msigwa anatarajia kutumia milioni 200 kuuandaa mkutano wa mgombea wa urais wa Chadema/Ukawa Edward Lowasa, unaotarajia kufanyika mwishoni mwa juma hili.
Sasa hapo amepiga nini wakati umeshasema ni kwa ajili ya kuandaa mkutano?
Hatua hiyo inakuja ikiwa ni wiki ya pili sasa tangu mbunge huyo alipopokea shilingi milioni 50 kama hongo kutoka kwa Lowassa kwa ajili ya utengezezaji wa mabango makubwa ambayo yamewekwa kwenye mitaa mbalimbali mjini Iringa.
Ndugu, Kiswahili unakifahamu vizuri, au? Hapa napo unasema alipokea hongo ya 50m kwa ajili ya utengenezaji wa mabango!! Sasa hongo kivipi hapo? Hivi leo hii Magufuri akitoa 100 million akampa Ngeleja ili ategeneze mabango ya kampeni akiwa njiani kwenda Sengerema ina maana Ngeleja hapo atakuwa amechukua hongo?
Hata hivyo imebainika kuwa mil 200 hizo alizokabidhiwa Msigwa ni kutokana na kumtetea Lowassa wakati wa mada iliyorushwa Channel Ten
Sasa tuamini lipi? Hizo 200M ni kwa ajili ya kumtetea EL, au
Peter Msigwa anatarajia kutumia milioni 200 kuuandaa mkutano wa mgombea wa urais wa Chadema/Ukawa Edward Lowasa

Eh Mungu, Muumba wa mbingu na ardhi, ziwaishe siku kwa kasi ya mara tano zaidi ili huu uchaguzi upite manake waja wako wanazidi kujitoa ufahamu! Thanks God kwa sheria zetu ambazo zinatoa muda mfupi sana wa mambo ya kampeni vinginevyo sijui ingekuwaje kama tungekuwa tunapewa mwaka mzima wa kushuhudia ujinga ujinga kwenye mitandao ya kijamii.
 
tatizo letu sisi wana ccm tumezoea uwongo sana,watu tuandika habari zenye tija,tupambane na wenzetu kwa mbinu sio siasa za majitaka,mnashushia hadhi chama chetu ccm wakongwe bhana tujenga hoja wakuu
 
Hana chake huyo malofa wapumbavu mkapimwe akili zenu na huyo mchungaji anaesema uongo
 
Lowasa anavyowakimbiza mchakamchaka kitaeleweka tu
 
Sasa hapo amepiga nini wakati umeshasema ni kwa ajili ya kuandaa mkutano?Ndugu, Kiswahili unakifahamu vizuri, au? Hapa napo unasema alipokea hongo ya 50m kwa ajili ya utengenezaji wa mabango!! Sasa hongo kivipi hapo? Hivi leo hii Magufuri akitoa 100 million akampa Ngeleja ili ategeneze mabango ya kampeni akiwa njiani kwenda Sengerema ina maana Ngeleja hapo atakuwa amechukua hongo?Sasa tuamini lipi? Hizo 200M ni kwa ajili ya kumtetea EL, au

Eh Mungu, Muumba wa mbingu na ardhi, ziwaishe siku kwa kasi ya mara tano zaidi ili huu uchaguzi upite manake waja wako wanazidi kujitoa ufahamu! Thanks God kwa sheria zetu ambazo zinatoa muda mfupi sana wa mambo ya kampeni vinginevyo sijui ingekuwaje kama tungekuwa tunapewa mwaka mzima wa kushuhudia ujinga ujinga kwenye mitandao ya kijamii.

Hahahaaaaaa,umemkamata vizuri!
 
Back
Top Bottom