Wadau nipo njia panda naombeni ushauri wenu, nimefanya kosa kubwa na nalijutia
Tafadhali naomba ushauri badala ya kunituhumu
Mwezi nilikuta na demu mmoja tulisoma naye chuo kitambo alikuwa demu wangu for time being, so baada ya miaka kadhaa tukaja kukuta sehemu, shetani akanipitia nikavunja amri ya sita naye
Baada ya kurudi home nikagundua sina pete, nikajaribu kukumbuka nilipoiweka sikupata majibu
Baada ya siku kadhaa yule demu akzidi kunisumbua na kutaka niwe karibu naye sana lakini nikaona si vyema maana anaweza kusababisha mtafaruku kwa ndoa yangu
Baada ya kuona nampotezea akaniambia sasa unajifanya mjanja pete yako ni nayo na nahitaji sh 500,000 cash ama sivyo naharibu kwa mkeo kwamba pete ninayo na ulinikopa.
Kibaya zaidi wife aliniuliza pete umepeleka wapi nikadanganya nimeisahau ofisini nilikuwa nafungua printer sasa pete ikawa inani disturb nikaivua , nilipoenda jumatatu nikamwambia nahisi wahudumu wa usafi wameiiba maana siiona pale nimeiweka naendelea na uchunguzi.
Mwanzo nilimpuuzia lakini mshenzi yule kapeleleza hadi wife anapofanya kazi na kapata simu yake, juzi kampigia kamwambia "naomba mkumbushie mumeo deni langu mimi xxxxx nampigia simpati" halafu akakata simu.
Niliporudi wife kanibana nikamwambia ni mambo ya kazi tu akataka kujua no yake kaipataje, nikazuga zuga na ubabe wa kiume yakaisha
Nikipiga akili nimuendee Polisi naona kama kitanuka na wife atajua
Nikifikiria kumlipa akili hainipi kabisa....kilo tano?
Sijui nimueleze wife ukweli?
Nimejaribu kumpiia simu na kumbembeleza kagoma anachohitaji ni kilo tano au aniharibie kwa wife
Tafadhali ushauri wakuu lawama na madongo hayatanisaidia
hapa ndugu usijaribu coz ushajua nia ya huyo mdada c wa kumrudia hata kidogoWewe unataka kuleta matatizo makubwa kwenye ndoa yako,,mke wako akijua tu kama umemsaliti,,,jiandae,,na yeye lazima akusaliti,,hawa ndio wanawake wakijidital,,,we jifanye mjinga,,mrudie huyo mwenye pete yako,,jaribu ku mlaghai kwa maneno matamu na ahadi nzito,,ukiipata pete yako,,,kata mawasiliano kabisa..ila kuwa makini asije akakupiga picha au akaku record.
Ingekuwa mimi, ili mke aendelee kuniamini ningepitia dukani nachukua nyingine hata kama sina feza(siyo wa big brother) nalipa kidogo kidogo, nione atafika nayo wapi!Wadau nipo njia panda naombeni ushauri wenu, nimefanya kosa kubwa na nalijutia Tafadhali naomba ushauri badala ya kunituhumu Mwezi nilikuta na demu mmoja tulisoma naye chuo kitambo alikuwa demu wangu for time being, so baada ya miaka kadhaa tukaja kukuta sehemu, shetani akanipitia nikavunja amri ya sita naye Baada ya kurudi home nikagundua sina pete, nikajaribu kukumbuka nilipoiweka sikupata majibu Baada ya siku kadhaa yule demu akzidi kunisumbua na kutaka niwe karibu naye sana lakini nikaona si vyema maana anaweza kusababisha mtafaruku kwa ndoa yangu Baada ya kuona nampotezea akaniambia sasa unajifanya mjanja pete yako ni nayo na nahitaji sh 500,000 cash ama sivyo naharibu kwa mkeo kwamba pete ninayo na ulinikopa. Kibaya zaidi wife aliniuliza pete umepeleka wapi nikadanganya nimeisahau ofisini nilikuwa nafungua printer sasa pete ikawa inani disturb nikaivua , nilipoenda jumatatu nikamwambia nahisi wahudumu wa usafi wameiiba maana siiona pale nimeiweka naendelea na uchunguzi. Mwanzo nilimpuuzia lakini mshenzi yule kapeleleza hadi wife anapofanya kazi na kapata simu yake, juzi kampigia kamwambia "naomba mkumbushie mumeo deni langu mimi xxxxx nampigia simpati" halafu akakata simu. Niliporudi wife kanibana nikamwambia ni mambo ya kazi tu akataka kujua no yake kaipataje, nikazuga zuga na ubabe wa kiume yakaisha Nikipiga akili nimuendee Polisi naona kama kitanuka na wife atajua Nikifikiria kumlipa akili hainipi kabisa....kilo tano? Sijui nimueleze wife ukweli? Nimejaribu kumpiia simu na kumbembeleza kagoma anachohitaji ni kilo tano au aniharibie kwa wife Tafadhali ushauri wakuu lawama na madongo hayatanisaidia
Polisi mpango mzima
Najaribu kuongea nao wamenihakikishia mambo yatakuwa ok maana wameisha deal na issue hizo mara nyingi
Si wangefanya kinguonguo?
Pole kwa yaliyo kusibu. Tendo ulilofanya la kumsaliti mkeo halikua zuri. Sasa unachoweza kufanya ni kumwambia mkeo ukweli na kwa uangalifu Unaweza kumwambia jinsi ulivyokutana na huyo dada lkn usigusie kama mlizini manake hiyo inauma sana jaribu kukwepesha eneo hilo na ujitahidi kusema ukweli kwa 90% ili huyo dada akose cha kusema . Mwisho kabisa baada ya kupatana na mkeo muombe yeye aifuatilie pete hiyo.