Pete ya ndoa inaniponza......mawazo yako tafadhali

Pete ya ndoa inaniponza......mawazo yako tafadhali

Mayu

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2010
Posts
8,679
Reaction score
14,363
Wadau nipo njia panda naombeni ushauri wenu, nimefanya kosa kubwa na nalijutia
Tafadhali naomba ushauri badala ya kunituhumu

Mwezi nilikuta na demu mmoja tulisoma naye chuo kitambo alikuwa demu wangu for time being, so baada ya miaka kadhaa tukaja kukuta sehemu, shetani akanipitia nikavunja amri ya sita naye

Baada ya kurudi home nikagundua sina pete, nikajaribu kukumbuka nilipoiweka sikupata majibu
Baada ya siku kadhaa yule demu akzidi kunisumbua na kutaka niwe karibu naye sana lakini nikaona si vyema maana anaweza kusababisha mtafaruku kwa ndoa yangu

Baada ya kuona nampotezea akaniambia sasa unajifanya mjanja pete yako ni nayo na nahitaji sh 500,000 cash ama sivyo naharibu kwa mkeo kwamba pete ninayo na ulinikopa.

Kibaya zaidi wife aliniuliza pete umepeleka wapi nikadanganya nimeisahau ofisini nilikuwa nafungua printer sasa pete ikawa inani disturb nikaivua , nilipoenda jumatatu nikamwambia nahisi wahudumu wa usafi wameiiba maana siiona pale nimeiweka naendelea na uchunguzi.

Mwanzo nilimpuuzia lakini mshenzi yule kapeleleza hadi wife anapofanya kazi na kapata simu yake, juzi kampigia kamwambia "naomba mkumbushie mumeo deni langu mimi xxxxx nampigia simpati" halafu akakata simu.
Niliporudi wife kanibana nikamwambia ni mambo ya kazi tu akataka kujua no yake kaipataje, nikazuga zuga na ubabe wa kiume yakaisha

Nikipiga akili nimuendee Polisi naona kama kitanuka na wife atajua
Nikifikiria kumlipa akili hainipi kabisa....kilo tano?
Sijui nimueleze wife ukweli?

Nimejaribu kumpiia simu na kumbembeleza kagoma anachohitaji ni kilo tano au aniharibie kwa wife
Tafadhali ushauri wakuu lawama na madongo hayatanisaidia
PROBLEM SOLVED!!!!!!!!
Jana mchana nilimpiigia mshkaji wangu mmoja anakaa magomeni anapenda kunywa baa za magomeni polisi, nikamueleza aniunganishe kwa rafiki zake Polisi. Akaniambia kazi ndogo sana hiyo nikitoka kwa ofisi nimfuata magomeni.

Nilipofika nikakuta Askari wawili na mshkaji nikawapa habari wakaniambia palepale nimpigie simu na nijifanye nipo tayari kulipa lakini anipunguzie nina kilo tatu tu, demu akagoma na kudai mwisho kilo4, then tukapanga tukutane baa fulani kwa makabidhiano. Wakaniambia sasa twende polisi ukaripoti upate na RB ili demu asije akaleta ujuaji

Tulipofika eneo la tukio mimi nikakaa nje askari ndani, baada ya yule demu kuingia akiwa na shoga yake wakakaa na kuagiza vinywaji mara sakari polisi wakatokea, mpochini ya ulinzi kwa wizi wa simu mbili, pesa, pete na Laptop wanahitajika kituoni
Demu akataka kuleta za kuleta akatolewa maganda ikabidi awe mdogo, wakabebwa kwenye gari ya kukodi, ilibidi wabebwe wote maana inawezekana pete ikawa kwa yule mwingine na nia ilikuwa wakibisha wapekuliwe na kukutwa na kithibiti

Walipokuwa wanaelekea kituoni askari wakawaambia mimi nimemshtaki kwa wizi huo so kama hataki mambo yawe makubwa ni bora watoe hiyo pete wao watajua jinsi ya kuongea na mimi maana mimi nimedhamiria kumfunga na wanauhakika hiyo pete imo kwenye begi la mmojawao. Ikabidi wakubali kutoa pete na wakawahonga Polisi elf60 wafanye juu chini kumaliza mambo yasiende mbali.
Wakaonywa wasijaribu kufanya ujinga wowote ikiwemo kumpigia wife maana kesi inaweza kuendelezwa na wao watashindwa kuwatetea

Wakaachiwa, tukakutana nao wakanipa pete yangu wakaniambia nijihukumu mwenyewe nitatoa ngapi, Nikawapa Kilo moja
ukijumlisha na elf60 za yule mshenzi jamaa wakanza kulapombe mimi mbio home

Nashukuru sana kwa mawazo yenu sasa mnaruhusiwa kunipiga madongo muwezavyo as long as problem solved
Thank you JF
 
Pole kwa yaliyo kusibu. Tendo ulilofanya la kumsaliti mkeo halikua zuri. Sasa unachoweza kufanya ni kumwambia mkeo ukweli na kwa uangalifu Unaweza kumwambia jinsi ulivyokutana na huyo dada lkn usigusie kama mlizini manake hiyo inauma sana jaribu kukwepesha eneo hilo na ujitahidi kusema ukweli kwa 90% ili huyo dada akose cha kusema . Mwisho kabisa baada ya kupatana na mkeo muombe yeye aifuatilie pete hiyo.
 
Duuh,kaka huyo mwanamke atakuwa ni Kahaba aisee,huyo anaona kilo tano kuipata rahisi wakati watu ni salary ya miezi kadhaa ,huyo muite alafu nunua tindikali mwagie
 
wadau nipo njia panda naombeni ushauri wenu, nimefanya kosa kubwa na nalijutia
tafadhali naomba ushauri badala ya kunituhumu

mwezi nilikuta na demu mmoja tulisoma naye chuo kitambo alikuwa demu wangu for time being, so baada ya miaka kadhaa tukaja kukuta sehemu, shetani akanipitia nikavunja amri ya sita naye

baada ya kurudi home nikagundua sina pete, nikajaribu kukumbuka nilipoiweka sikupata majibu
baada ya siku kadhaa yule demu akzidi kunisumbua na kutaka niwe karibu naye sana lakini nikaona si vyema maana anaweza kusababisha mtafaruku kwa ndoa yangu

baada ya kuona nampotezea akaniambia sasa unajifanya mjanja pete yako ni nayo na nahitaji sh 500,000 cash ama sivyo naharibu kwa mkeo kwamba pete ninayo na ulinikopa.

Kibaya zaidi wife aliniuliza pete umepeleka wapi nikadanganya nimeisahau ofisini nilikuwa nafungua printer sasa pete ikawa inani disturb nikaivua , nilipoenda jumatatu nikamwambia nahisi wahudumu wa usafi wameiiba maana siiona pale nimeiweka naendelea na uchunguzi.

Mwanzo nilimpuuzia lakini mshenzi yule kapeleleza hadi wife anapofanya kazi na kapata simu yake, juzi kampigia kamwambia "naomba mkumbushie mumeo deni langu mimi xxxxx nampigia simpati" halafu akakata simu.
Niliporudi wife kanibana nikamwambia ni mambo ya kazi tu akataka kujua no yake kaipataje, nikazuga zuga na ubabe wa kiume yakaisha

nikipiga akili nimuendee polisi naona kama kitanuka na wife atajua
nikifikiria kumlipa akili hainipi kabisa....kilo tano?
Sijui nimueleze wife ukweli?

Nimejaribu kumpiia simu na kumbembeleza kagoma anachohitaji ni kilo tano au aniharibie kwa wife
tafadhali ushauri wakuu lawama na madongo hayatanisaidia

bro,hakuna kitu kibaya kama kuiyumbisha ndoa yako,fanya hivi,chukua hiyo laki 5 mpelekee huyo malaya akupe pete yako,uwe umeandaa polisi ambao utawastua baada ya kukabidhi hiyo hela na wewe kupata pete yako.huna haja ya kumpeleka mbalia au kituoni,baada ya kumkamata wamwambie anatuhumiwa kwa kosa la kuku "blackmail"ili ajipatie fedha.ni kosa tosha sana la kumfikisha mtu mahakamani.so aamue kwenda mahakamani kwa kuwa ushahidi wa kuchukua pesa upo(pesa iwe ni kithibiti cha rushwa aliyoomba)au arudishe pesa yako na kuachiwa huru.ukitumia nguvu kumnyang'anya itaonekana umemletea maaskari ili wamnyang'anye pesa.pia aonywe kutompigia mkeo simu,enddapo atafanya hivyo tena atachukuliwa hatua.hii kitu itakapokuja bumbuluka kwa waifu we komaa na msimamo wako kuwa ni mambo ya ofisini na alikuwa anakudai fullstop.ukijichanganya ndo mwanzo wa kuiyumbisha ndoa yako.
acha umalaya 2mbavu
 
Weeeeeeee! Usiwe zoba na kwenda kujishtaki kwa mkeo! Hii michezo ya mjini kwetu born town mbona simple sanaaaaaa! Wala hamna haja ya kwenda kujisalimisha kwa mkeo!

1. Polisi ndio Suluhisho! Tunza hizo massage anazo kublack mail umpe hio kil 5, ikiwezekana mrekodi then kahonge nusu kilo tu polisi,, unamchukua mmoja mnaenda kumuambush kwake ama kazini, anasweka ndani kwa mashtaka ya Wizi, Utapeli, Blackmail, Kujipatia feza isivo halali na ikiwezekana na madai ya fidia juu! Na ushenzi huu unamfanyia ijumaa jioni. Hapo zaman ni jatau! Siku mbili hizo za weekend lazima akulambe miguu msuluhishane!!!!!!!! Na mwanzo ni kuleta pete! Na kesi huifuti ndo inakuwa cha kumfungia mdomo! Akisema tu nyo.ko ndo ajiandae na gharama za kesi kwa umbea tu! Nyamaaaaaaaafff!

2. Unakodisha mateja tu, wanaenda kumtikisa kidogo nyumbani kwake na kumwambia akizubutu kukukaribia wanakuja kumbaka na kumpiga picha. Wewe siku hizi ni Muuza white sugar wa kuaminika amebugi men! Kukuchezea bosi wao! Atatetemekaje sasa na kusalimisha pete kiupole! Ile amekaa ndani hodi, miteja kama 6 na visu mkononi! Kwa kino hatokucost zaidi ya nusu kilo tu.

3.Tafuta namba za wazazi wake na UKASHITAKI yote, na uwaeleze ana pete yako, na unataka kumshtaki polisi, so hata akimwambia mkeo wajiandae na kesi nzito za hapo juu, ama arudishe mmalizane.

Ujue watu wanakupima tu, Ukionekana zimejaa wananywea! Ila ukitishika na nyau hata ukitoa Kilo 5, pete hupewi na mkeo haambiwi chochote! Uzobaa wako tu.
 
Dah!Hilo likurumbembe kazi unayo.Hapo juu wadau wametoa ushauri mzuri ufuate.Pole sana nadhani utakuwa unaiacha nyumbani ukienda kwenye uzinzi.
 
Dah!Hilo likurumbembe kazi unayo.Hapo juu wadau wametoa ushauri mzuri ufuate.Pole sana nadhani utakuwa unaiacha nyumbani ukienda kwenye uzinzi.

siyo kwamba ataacha kabisa uzinzi??????? teh teh mshahara wa dhambi........
 
Hivi kwani ukigegeda...pete inazuia nini.??, kisa kilichokufanya uivue.?? Kila mtu atajiuliza hilo swali kwann uvueee...
Watahis kitu tu
 
Hivi kwani ukigegeda...pete inazuia nini.??, kisa kilichokufanya uivue.?? Kila mtu atajiuliza hilo swali kwann uvueee...
Watahis kitu tu

Kuna wengine majuha tu wanaamini kuvua pete utakuwa unamtendea mwenzako huruma kuliko kula ama kuliwa hali ya kuwa umevaa kidoleni. Dhambi ni dhambi tu hiyo pete ni urembo tu ndoa inabakia moyoni kama unaiamini huwezi kufika kwenye uzinifu ukatoa pete kisha ukawa sahihi.
 
Muanzisha thread huu ndio ushauri ambao ni muafaka kupambana na huyo tapeli, na usisahau kurudi hapa kutufahamisha hii kitu imeishaje. Kila la heri.

bro,hakuna kitu kibaya kama kuiyumbisha ndoa yako,fanya hivi,chukua hiyo laki 5 mpelekee huyo malaya akupe pete yako,uwe umeandaa polisi ambao utawastua baada ya kukabidhi hiyo hela na wewe kupata pete yako.huna haja ya kumpeleka mbalia au kituoni,baada ya kumkamata wamwambie anatuhumiwa kwa kosa la kuku "blackmail"ili ajipatie fedha.ni kosa tosha sana la kumfikisha mtu mahakamani.so aamue kwenda mahakamani kwa kuwa ushahidi wa kuchukua pesa upo(pesa iwe ni kithibiti cha rushwa aliyoomba)au arudishe pesa yako na kuachiwa huru.ukitumia nguvu kumnyang'anya itaonekana umemletea maaskari ili wamnyang'anye pesa.pia aonywe kutompigia mkeo simu,enddapo atafanya hivyo tena atachukuliwa hatua.hii kitu itakapokuja bumbuluka kwa waifu we komaa na msimamo wako kuwa ni mambo ya ofisini na alikuwa anakudai fullstop.ukijichanganya ndo mwanzo wa kuiyumbisha ndoa yako.
acha umalaya 2mbavu
 
Dah pole sana. Hivi mnaamini kuwa kuna maswala ya mazingaombwe? Muwe mnafikiria kabla ya kutenda. Huyo mwenye mawazo ya kuchukua pete yako kukukomoa ili uwe nae anaweza hata kubeba manii yako katika kitambaa alichokufutia na kwenda kukushughulikia ili mkeo akose na yeye apate. Wanaume msiwe wepesi kutenda mambo ambayo baadae mtawaletea wmatatizo wake zenu. Hivi mnafikiri ndoa zote zinazovunjika huwa inatokea tu?? Zipo ambazo wanandoa hujikuta wakichukiana kimazingira kwa sababu kuna third party kaamua.
 
Nakushauri wewe I mwanaume, msome mkeo kwanza kama anacho kifua na akili ya kuelewa wanawake wengine sie hatuna dogo ukishakiri basi ntakuona kila siku wewe ni mhalifu hata nkijakukuomba unikate kucha za miguuni wakati nina mimba ukigoma ntarelate na kosa lako ulilofanya miaka kumi ilopita. Msome mkeo kama anacho kifua cha ustahimilivu na uelewa basi mketishe chini mweleweshe, mwambie ni kosa unakubali na halitorudia tena nisaidie tufanyeje. Kama si mwelewa ni mtu kama MwanajamiiOne hapa basi minya, deal na hiyo issue kiume uue soo.
 
Last edited by a moderator:
bro,hakuna kitu kibaya kama kuiyumbisha ndoa yako,fanya hivi,chukua hiyo laki 5 mpelekee huyo malaya akupe pete yako,uwe umeandaa polisi ambao utawastua baada ya kukabidhi hiyo hela na wewe kupata pete yako.huna haja ya kumpeleka mbalia au kituoni,baada ya kumkamata wamwambie anatuhumiwa kwa kosa la kuku "blackmail"ili ajipatie fedha.ni kosa tosha sana la kumfikisha mtu mahakamani.so aamue kwenda mahakamani kwa kuwa ushahidi wa kuchukua pesa upo(pesa iwe ni kithibiti cha rushwa aliyoomba)au arudishe pesa yako na kuachiwa huru.ukitumia nguvu kumnyang'anya itaonekana umemletea maaskari ili wamnyang'anye pesa.pia aonywe kutompigia mkeo simu,enddapo atafanya hivyo tena atachukuliwa hatua.hii kitu itakapokuja bumbuluka kwa waifu we komaa na msimamo wako kuwa ni mambo ya ofisini na alikuwa anakudai fullstop.ukijichanganya ndo mwanzo wa kuiyumbisha ndoa yako.
acha umalaya 2mbavu
Sidhani kama ni sahihi kumwita huyo mdada Malaya..................Blackmailer sawa but not Malaya kwa sababu kama Malaya hata huyu mwanaume anaqualify kuitwa Malaya. Kisa cha kutoka nje ya ndoa yake ni nini. Malaya ni huyo mwanaume besides hajasema alivyomtongoza huyo mwanamke anayedai alikuwa wake wa zamani alimwambia nini..............
 
Pole kwa yaliyo kusibu. Tendo ulilofanya la kumsaliti mkeo halikua zuri. Sasa unachoweza kufanya ni kumwambia mkeo ukweli na kwa uangalifu Unaweza kumwambia jinsi ulivyokutana na huyo dada lkn usigusie kama mlizini manake hiyo inauma sana jaribu kukwepesha eneo hilo na ujitahidi kusema ukweli kwa 90% ili huyo dada akose cha kusema . Mwisho kabisa baada ya kupatana na mkeo muombe yeye aifuatilie pete hiyo.

Hapa nimeona busara katika kuukumbatia ukweli, ingawa mara nyingine kuukumbatia ukweli sana kunaunguza, mhusika atajaribu kuangalia kwa jinsi ya habari inavyohusikika kwake.

Lakini hilo la mwanamme kumuomba mkewe afuatilie pete iliyotoweka kwa makosa ya mwanamme ni kumtwika huyo mke dhahama lisilohusikana na makosa yake, aliyepoteza pete ndo arudishe pete. Mwanamme wa shoka ambaye ataweza kukiri kwamba kakosea hatakiwi kushindwa kuikomboa pete ya ndoa yake kutoka kwa mwanamke wa nje ambaye si mke wake.

Na hata akishindwa kufanya hivyo, kumtuma mke wake ni ukuwadi usio mfano kwangu.

Ni bora kuendelea na story ya "nilikuwa nafungua printer...wahudumu wakaniacha", uongo mzima, kuliko ukuwadi gonjwa wa kumtuma mke aende kukomboa pete kwa makosa ya mume.

Akimwagiwa acid usoni mwana wa watu huko?
 
Nilipendekeza amtume mkewe kwa kutaka kumjulisha huyo mwanamke kua hata mkewe issue yao anaifahamu so asiendelee kumtishia kwamba atamshitaki kwa mkewe na kumharibia. Otherwise huyu ndugu anapaswa kuchmbua kwa kina mawazo mbali mbali yaliyotolewa na wadau hapa jukwaani na mwisho aone nini anaweza kufanya au lipi ni jepesi kwake kufanya. Najua kila mdau ana nia njema ya kutaka kumsaidia mhanga . Halafu bora umegusia mambo ya acid so wawe careful.
 
Back
Top Bottom