Pesa za nani zinajenga mahekalu haya kijijini kwa Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pesa za nani zinajenga mahekalu haya kijijini kwa Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwikimbi, Jul 26, 2008.

 1. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Jana nilipita sehemu inayoitwa Msoga kama kama kumi ukitokea Chalinze, kwenda Arusha. Kuna kitongoji kinaitwa vicoba hapa ndo nyumbani kwa Jakaya Kikwete.Kuna ujenzi wa majengo kama 14 yanajengwa pale. wenyeji wanasema inajengwa ikulu pale.

  Muungwana Rais, kila Jumamosi anakuja kukagua ujenzi.Inasemekana kuwa anakuja kupitia Mlandizi, anafika Vocoba then anarudia Bagamoyo kupitia kwa wazee wake pale Bagamoyo.

  Pia kuna ujenzi wa majengo mawili ya ghorofa nne, yamejengwa na national housing nje kidogo ya Chalinze, inasemekana ni kwa ajili ya wafanyakzi watakao kuwa wanafanya kazi ikulu ya Vicoba.

  Je, ni nani anafadhili ujenzi wa ikulu mpyaa Vicoba? Kama ni serikali iko kwenye bajeti?

  Isije ikawa yale mambo ya Mobutu Sesseko kuhamishia ikulu kule Gbaolite!

  Mwenye information naomba anielimishe.
   
 2. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..hizo point mbili zina ukweli?

  ..ninachofahamu ni ujenzi wa makazi yake pale, kitu ambacho ni cha kawaida.
   
 3. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  anapata wapi mabilioni yote hayo kujenga makazi ya kifahari katika taifa maskini kama hili? mbona nyerere hakuweza kufanya haya kwa miaka yote 24 aliyokaa ikulu? wale waliosema jk ni nyereree na lowasa ni sokoine nielemisheni
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mwikimbi,
  Nani kakwambia Mwungwana hana hela? Yale mafaili ya Mangula yangefunguliwa pale kwenye kikao cha CCM cha kuchagua rais wabongo tungebaki hoi!
   
 5. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2008
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,435
  Likes Received: 2,310
  Trophy Points: 280
  Heshima mbele! mafaili gani hayo tena mkuu? tunaomba na sisi tuyafahamu!! Natanguliza asante!
   
 6. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  tunataka rais akistaafu aweze kuwa na nyumba ya kuishi na wakati mwingine siyo vibaya serikali ikamjengea kwa uwazi bila kificho. je kuna anayejua huu ujenzi wa kasi wa vicoba msoga nani anaufadhili? ni taratibu za kawaida? nikijibiwa maswali haya sina wasiwasi nao. mjue kuwa muungwana ana miaka miwili tu ikulu.
   
 7. Kaka K

  Kaka K Senior Member

  #7
  Jul 27, 2008
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 129
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huenda ikawa kweli, but let us not judge this book by its cover. Any one with detailed facts please bring them here. Ikiwezekana na ramani/picha ya hiyo project nzima ili tuweze kujua ni residential au ni IKULU.
   
 8. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #8
  Jul 27, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Hili ni jambo zito kidogo lakini ngoja kwanza facts zimwagwe hapa ndipo nilivae. kama ni kweli lina mwelekeo mbaya sana. ndiyo maana uharaka wa mabadiliko ya katiba nchini mwetu ni wa muhimu sana kuhakikisha kuwa usimamizi wa matumizi ya fedha zetu unaondolewa kutoka executive branch. Huwezi kumpa mtu pesa zako atumie halafu ukamtaka asimamie kuhakikisha kiwa anzitumia kulingana na matakwa yakoi. Ukimpa ni lazima uhakikishe msimaizi wa matumizi hayo siyo mshikaji wake.


  BTW: Kulingana na background yake, gia iliyomwigiza Ikulu, na utendaji wake baada ya kuingia Ikulu, sina wasiwasi kuwa kama kweli ujenzi huo upo basi ni kwa ajili ya makazi binafsi ya Kikwete. lakini ngoja tupate facts kwanza.
   
 9. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #9
  Jul 27, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,431
  Trophy Points: 280
  ..HAYO MAJENGO TANGU MSINGI ULIPOANZA MARA TU ALIPOINGIA MADARAKANI TULILETA TAARIFA HAPA.....PALE NI MAKAZI YAKE BINAFSI...PALE NDIPO ASILI YA UKOO WAO..BAGAMOYO WALIHAMIA TU...!!!....ANAJENGA MAKUMBA PALE ILI UKOO WAKE WOTE UHAMIE PALE.....SANJALI NA HUO UJENZI PIA MAKAZI YAKE YA MIGOMBANI STREET ALIBOMOA NA KUNUNUA KIWANJA CHA JIRANI YAKE PALE ..NATAYARI JUMBA KUBWA LIMESIMAMA PALE...

  UJENZI HUU NI NJE YA UJENZI AMBAO HUFANYWA NA SERIKALI KAMA STAHILI YA RETIREMENT PACKAGE AMBAO KWA KAWAIDA KIKWETE ATASTAHILI TENA KUJENGEWA NYUMBA NA OFISI SEHEMU ATAKAYOCHAGUA PALE ATAKAPOKARIBIA KUSTAAFU..MWAKA 2010.......AU KAMA BAHATI NBAYA HATAWEZA KUENDELEA NA MADARAKA KWA SABABU YOYOTE.......

  ZILE NYUMBA ZA NATIONAL HOUSING PALE ZIMEJENGWA KATIKA MKAKATI WA KUHAMISHIA MAKAO MAKUU YA MKOA WA PWANI PALE CHALINZE ....BAAADA YA KUONEKANA WAZI KUWA KIBAHA HAICHANGAMKI AU INAKARIBIA KUMEZWA NA DAR ES SALAAM......

  ..MOJA YA WASIMAMIZI WA MRADI WA MAJUMBA YA KIKWETE NI RAFIKI YAKE WA TANGU ZAMANI ..BAGAMOYO...BWANA SUBASH PATEL,,,,,ambaye pia humsimamia baadhi ya kazi zake nyingine.........hivi karibuni kwa heshima ya kikwete bwana subash alikarabati shule ya msingi aliyesoma kikwete.....hapo kijijini.....

  UKWELI NDIO HUO!
   
 10. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  mi naona hizo hela za ujenzi wa hayo majumba angesaidia japo vijana wa chalinze either kuwasomesha au hata kuwapa miradi ya ukweli ambayo itawasaidia kuwatoa maishani...
  kuliko sasa wanavyo taabika kwa kuuza machanuo na vyungu kwenye mabasi pale chalinze stand....
   
 11. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #11
  Jul 27, 2008
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 571
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Subash yule wa jengo la UVCCM?
   
 12. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #12
  Jul 27, 2008
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hapo ndipo utata mwingine unapoingia.
   
 13. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #13
  Jul 27, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  I can see now kwa nini mafisadi wanavuruga nchi usiku na mchana bila ya wasi wasi wowote.. Kama ni makazi binafsi ya muungwana as retirement package hivi kuna jinsi ambayo serikali inamchagulia aina ya nyumba atakayojengewa au muungwana mwenyewe anaamua tu wajenge mahekalu atakavyo?? Najaribu kuangalia nyumba ya Mzee ruksa pale mikocheni naona ni ya kawaida sana...Sasa huu ujenzi wa hapo chalinze unanistaajabisha sana....Jamani tuelimishane huenda nchi imeiingiliwa na jinamizi tuamshane mapema!!!
   
 14. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #14
  Jul 27, 2008
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hivi hizo cellfoni zenu, camera zake hazifanyi kazi? Tunaomba mtu ajitolee kupiga picha hizo nyumba, Dar na huko Chalinze ili utamu wa hii stori kolee na kupata nguvu.

  Magazeti yetu nayo mbona kimya?
   
 15. J

  JokaKuu Platinum Member

  #15
  Jul 27, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,775
  Likes Received: 5,000
  Trophy Points: 280
  ..jamani si achukue mkopo tu kama Sumaye ajenge nyumba yake binafsi.
   
 16. K

  Kinto Senior Member

  #16
  Jul 27, 2008
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 109
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Na anayeweza kutuletea picha za kasiri la BWM la Lushoto pia tungeshukuru, naona hawa jamaa sasa wanashindana, ila muungwana kawahi mno.
   
 17. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #17
  Jul 27, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,431
  Trophy Points: 280
   
 18. M

  Malila JF-Expert Member

  #18
  Jul 27, 2008
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Sina hakika kama ni huyohuyo ponjolo au mwingine lakini jina linafanana na hilo,km 22 toka Chalinze kwenda Bagamoyo kupitia kijiji cha Talawanda,kabla hujafika s/msingi Magurumatali jamaa wamemegewa ardhi kubwa ya kufa mtu,bango lao linasema wanatafiti kama kuna uwezekano wa kupata material za saruji,wanakijiji wanasema patajengwa kiwanda cha saruji,hata haieleweki ila ardhi imechukuliwa.Mitaa yote hiyo ni mitaa ya muungwana na jamaa zake.
   
 19. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #19
  Jul 27, 2008
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  wakwere ni navyowajua, basi watakuwa hawalipwa,si wanamwita muungwana wa ukaee,so mwana wa ukae karudi na friends kila kitu dezo tu.
   
 20. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #20
  Jul 27, 2008
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Sasa ndo mtajua kama RDC ilikuwa ya EL au ni ya mtu mwingine, Mkapa alikuwa cha mtoto huyu ndo atatutoa makamasi maana naona kaanza mapema.
   
Loading...