Pesa isiyo julikana kwenye account

Pesa isiyo julikana kwenye account

jiwe la maji

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2014
Posts
1,062
Reaction score
706
Kuna ndugu yangu kaja kuniomba ushauri afanye nini juu ya pesa shilingi laki tano aliyoikuta imezidi kwenye account yake.

Yeye ni mtu wa kawaida tu, hakuwa na mtu anayemdai wala hakuna mtu kama vile rafiki au ndugu ambaye anaweza kuwa labda amemtumia kama msaada. Kwakifupi amakuta pesa kwenye account yake ambayo afahamu imetoka wapi.

Yeye ni mtumishi wa umma, je akiitoa hiyo pesa akaitumia anaweza pata matatizo?
 
Kama waliideposite bahati mbaya akaitumia baadaae wakigundua wataanza ikata kwenye mshahara wake
 
Haya maswali mengine bana. Si akaombe bank statement atajua. Au kama vipi mwambie aniPM nimpeleke bar yenye mademu wazuri atapata matumizi tu.
 
Kama waliideposite bahati mbaya akaitumia baadaae wakigundua wataanza ikata kwenye mshahara wake
Nafikiri ikiwa hivyo wanaweza kuukata mshahara wake wote wa mwezi mara moja asibaki hata na cent.
 
Kuna ndugu yangu kaja kuniomba ushauri afanye nini juu ya pesa shilingi laki tano aliyoikuta imezidi kwenye account yake.

Yeye ni mtu wa kawaida tu, hakuwa na mtu anayemdai wala hakuna mtu kama vile rafiki au ndugu ambaye anaweza kuwa labda amemtumia kama msaada. Kwakifupi amakuta pesa kwenye account yake ambayo afahamu imetoka wapi.

Yeye ni mtumishi wa umma, je akiitoa hiyo pesa akaitumia anaweza pata matatizo?
Aiache tu walioiweka wataitoa.
 
Hela ya bank huwa haipotei hivyo akiitumia tuu watakuja kujua no yy ndiyo aliyeingiziwa hivyo watasubiri hela yyte ikiingia kwenye hiyo acc. Wanaitoa mwambie asichukue ila kama anataka kujikopesha basi anawezatumia
 
Aripoti tu kwa bank manager au customer service manager watajua imetoka wapi, mara nyingi inatokea kwa watu wa bank mwenyewe kukosea na kufanya wrong post, labda walikosea account number. Ni vizuri kaonyesha kujali, mwambie asishawishike akazitumia itamuondolea trust na bankers wake
 
Mwambie awaeleze bank au aombe taarifa zake za kifedha atajua hela ilipotoka.

Ila akiitoa na kuichezea mwisho wa mwezi ujao atachezea moto maana, kazini atakuwa anaenda kwa miguu na kupiga pasi ndefu.

Wataikata kutoka kwenye vyanzo vyake vya mapato kila hela inapoingia kwenye akaunti yake.

Mfano, kama unajua ule utaratibu wa zamani wa kukopa salio kwenye kampuni ya simu, mara ukiweka tu vocha inakatwa yote hadi deni liishe njia iyo hiyo inaweza ikatumika kwake.
 
Aripoti tu kwa bank manager au customer service manager watajua imetoka wapi, mara nyingi inatokea kwa watu wa bank mwenyewe kukosea na kufanya wrong post, labda walikosea account number. Ni vizuri kaonyesha kujali, mwambie asishawishike akazitumia itamuondolea trust na bankers wake
Ni kweli!
 
Kuna ndugu yangu kaja kuniomba ushauri afanye nini juu ya pesa shilingi laki tano aliyoikuta imezidi kwenye account yake.

Yeye ni mtu wa kawaida tu, hakuwa na mtu anayemdai wala hakuna mtu kama vile rafiki au ndugu ambaye anaweza kuwa labda amemtumia kama msaada. Kwakifupi amakuta pesa kwenye account yake ambayo afahamu imetoka wapi.

Yeye ni mtumishi wa umma, je akiitoa hiyo pesa akaitumia anaweza pata matatizo?

HABARI,
Awasiliane na uongozi wa bank husika hizo ni Kasoro za kibinadamu wakati mwingine hata computer hukosea pia.
Asijaribu kushawishika kuzitumia hilo litakuwa kosa la jinai na litamletea shida mbeleni.

LUMUMBA
 
Pesa mtu asiyeifanyia kazi huwa ina madhara, ni kama vile tu mtu kuokota mapesa barabarani alafu ukayafanyia natumizi kama vile kununua assets sijui watu wakianza kukuambia hongera utajibu vipi, binafsi napenda kupongezwa kwa vitu nilivyovipata kwa kazi ya mikono yangu.
 
Niliagana na Barclays kwa mtindo kama huu nilipita ma sarafu zao na zilikuja nikiwa nasaka sarafu vibaya mno.
Kama ni mtumishi inategemea yuko halmashauri gani maana kuna baadhi wamelipa sehemu ya madeni ambayo sio mshahara nadhani walianza alhamisi ila njia rahisi ni kwenda bank apate taarifa.
 
Back
Top Bottom