Pesa 8 zenye nguvu Afrika

Pesa 8 zenye nguvu Afrika

Wazambia walifuta sifuri kadhaa kutoka kwenye Kwacha yao.

Hilo linakuonesha kwamba, thamani ya pesa haina maana ya uchumi mzuri.

Hata sisi tunaweza kuondoa sifuri tatu kwenye shilingi yetu, dola moja ya kimarekani iwe shilingi mbili na ushee.

Tunaweza kufanya hilo leo.

Lakini, hilo halitamaanisha kuwa uchumi wetu utaimarika mara elfu.
Mkuu kufuta sifuri hakuwezi kuipandisha thamani ya pesa ya nchi fulani dhidi ya dola. Kuna vitu kama vile exports na imports zenu katika nchi zinachangia sana. Ingekuwa hivyo zimbabwe kipindi ya mwisho cha Mugabe wangeweza kufanya hivyo.
 
Leo nikiwa na Rand 100 sawa na dola moja.

Kesho nikafuta sifuri 2 kwenye hiyo Rand, ikawa Rand mpya.

Kesho hiyohiyo Rand mpya moja itakuwa sawa na dola ngapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazambia walifuta sifuri kadhaa kutoka kwenye Kwacha yao.

Hilo linakuonesha kwamba, thamani ya pesa haina maana ya uchumi mzuri.

Hata sisi tunaweza kuondoa sifuri tatu kwenye shilingi yetu, dola moja ya kimarekani iwe shilingi mbili na ushee.

Tunaweza kufanya hilo leo.

Lakini, hilo halitamaanisha kuwa uchumi wetu utaimarika mara elfu.
Lakini kuondoa sifuri inaweza kuwa sababu ya nguvu ya pesa?

ok, elfu 10 ya tz ukiondoa sifuri tatu za mwisho utaita elfu 10 tena au shs 10? lakini 1 USD moja kununua kwa hela ya TZ unahitaji hizo shs 10 ngapi?

Kinachofanya thamani ya hela kupanda na kushuka ni demand na supply ya sarafu yako sasa hilo lakutoa sifuri inafanya kazi wapi?
 
Leo nikiwa na Rand 100 sawa na dola moja.

Kesho nikafuta sifuri 2 kwenye hiyo Rand, ikawa Rand mpya.

Kesho hiyohiyo Rand mpya moja itakuwa sawa na dola ngapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiondoa sifuri 2 kweny rand 100 unapata rand 1!

1 USD ilikuwa rand 100. sasa ukiwa na rand1 unatakiwa kuzidisha mara 100 ilikupata 1 USD

1USD= 1Rand x100=100 Rand
 
Lakini kuondoa sifuri inaweza kuwa sababu ya nguvu ya pesa?

ok, elfu 10 ya tz ukiondoa sifuri tatu za mwisho utaita elfu 10 tena au shs 10? lakini 1 USD moja kununua kwa hela ya TZ unahitaji hizo shs 10 ngapi?

Kinachofanya thamani ya hela kupanda na kushuka ni demand na supply ya sarafu yako sasa hilo lakutoa sifuri inafanya kazi wapi?
Kwa mfano wako huo.

Elfu kumi ya Tan,ania tutoe sifuri tatu.

Exchange rate ya US dollar TZS itakuwaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiondoa sifuri 2 kweny rand 100 unapata rand 1!

1 USD ilikuwa rand 100. sasa ukiwa na rand1 unatakiwa kuzidisha mara 100 ilikupata 1 USD

1USD= 1Rand x100=100 Rand
Wewe yani hesabu ndogo hii inakutoa jasho?

Hebu jaribu tena.Usituletee aibu ya ungumbaru wa hesabu hapa.

Hints-

Call the old Rand "Old Rand" and the new Rand "New Rand" to avoid confusion..

100 old Rand = 1 USD

100 old Rand = 1 New Rand

How many New Rands equals 1 USD?

Sent usi g Jamii Forums mobile app
 
Hakuna Nchi kwa upande wa fedha yake naikubali Kama Zambia. Sijui wametumia Effort gani kubadii kutoka Kuwa pesa ya thamani ya Chini mpaka ubora huo.
Maana Kwacha ilikuwa mara mia kabisa TZS.
Lakini toka akamate Nchi Lungu, Mambo yanaenda Mswano kwa Ustable wa Currency yao. Tanzania CCM ndiyo Shida.
yes Zambia wamefanya mema kuimarisha sarafu yao,ila walichokifanya sio rocket science!! na sio president Lungu aliyefanya haya,soma upande wa pili wa story,unamkumbuka yule president wa mpito??ndiye aliyeleta mabadiliko haya within 6mths za utawala wake(President Scott.....ila ni mzungu huyu!!)
 
Hayo ni mazingaombwe matupu.

Uchumi haupandi kwa kuondoa sifuri kwenye hela. Ingekuwa hivyo kika nchi ingeondoa sifuri.

Uchumi unapanda kwa kuongeza uzalishaji.

Wachina hela yao ikioanda thamani, wanaishusha makusudi.

Kwa sababu wao, kama major exporters, hela yenye thamani kubwa si kitu kizuri kwa uchumi wao.

Na Wamarekani wanawalalamikia Wachina kila mara. Kwamba wanaishusha thamani ya Chinese Yuan artificially.

Yani Mchina na Mmarekani wanagombana, sababu Mchina anashusha thamani hela yake.

Hapo ndipo utajua hela kuwa na thamani kubwa si kitu kizuri mara zote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom