Pepo baya kwenye mirathi, limepukutisha wengi

Pepo baya kwenye mirathi, limepukutisha wengi

Mkuu upo sahihi kabisa,yaani Mirathi ya Nyumba na Ng'ombe ndiyo mirathi ambayo nimeshuhudia ikimaliza watu kwa Vifo vya ajabu.
 
Aisee kuna vitu vingine vya ajabu duniani...m nayaona kwenye movie tu kama ile magic house ya kanumba nachoshindwa kuelewa ni mazingaobwe au ni uchawi?
 
mshanajr mimi ni first born,nawezaje kutojihusisha kabisa na mambo ya miradhi kama yatanikuta
 
Last edited by a moderator:
Si kweli mkuu! Ingekua hivyo hivi Jk Nyerere angevumilia huu upuuz wa ccm? Mayatima wanavyoonewa hivi yani wazazi wanaona(ktk roho) alafu wanawaacha tu?

Roho hazikai duniani bro, huyo ni shaitwan tu mtu akishakufa rohi hurudi kwa aliyetoa pumzi na mwili ndio unazikwa

Huu ndiyo ukweli ...wafu hawajui neno lololote.....hawana kumbukumbu......hiyo ni kazi ya shetani na team yake...jiulize ww ukiwa usingizini wajua lolote?kama hujui sasa unapokufa utajuaje wakati ww ni mavumbi tayari....
 
Waafrika hasa wabantu tunasumbuliwa sana na mirathi. Ni namshukuru Mungu ya kwetu iliisha salama japo kwa timbwili kidogo.
Chanzo kikubwa ni utegemezi wa (bread winner mmoja katika familia).
Mi nashukuru iliisha salama kabisaaa bila figisu,maana marehemu alikua lofa,so hakukua na mgao
 
Nna rafiki yangu bibi yake mzaa mama aliacha nyumba,sasa wakaja babu zake wanataka khidhulumu,akanambia ataenda kwa mganga ile nyumba isiuzwe,yeyote akija akitaka kuinunua aishie kuiangalia tu,nyumba ipo Mwananyamala.
Hizi mambo bwana @mshana jr kweli zinarun down the streets
 
Madame B


Wamewaza vyema kuwafuateni wangejaribu kwenda kwa sangoma wangeisoma au pengine walijaribu wakaambiwa huu ni mziiki mnene
Na hii inathibitisha kuwa roho zinaishi na ziko hapahapa duniani pamoja nasi
Mizimu ya Kiafrika huwa inatenda, sio kama Yesu wa kubumba ambae hana miujiza yoyote.
 
Last edited by a moderator:
Dawa kila mtu atafute mali zake mwenyewe. ...hii tabia ya kugombea mali za marehemu sio nzuri. Kama kila mtu ana chake ukipata inakuwa nyongeza na sio nongwa
 
Dawa kila mtu atafute mali zake mwenyewe. ...hii tabia ya kugombea mali za marehemu sio nzuri. Kama kila mtu ana chake ukipata inakuwa nyongeza na sio nongwa
Sio wote wako hivyo wengine wanasubiri uzimike ili warithi
 
mambo haya yapo na yanaleta tabu, usidhulumu mrithi, utapata tabu!
 
mshana jr uko sahihi.

Bibi kafariki kaacha nyumba kubwa sana.

Kaacha watoto wawili tu, marehemu mama yangu na mjomba wangu ambae yuko hai.

Yaani huwezi amini, upande wa wakwe wa mjomba yaani wazazi wa shangazi mke wa mjomba wanaitaka ile nyumba maana wamekuja kukaa,kwani inakalika, wakilala usiku ni mijeredi kwa kwenda mbele.

Wapangaji hawakai, usiku taa zinajiwasha zenyewe...ukiweka umeme wa 50,000 kesho yake unakuta 0.00.

Ukisahau pesa juu ya meza unakuta imeliwa na panya japo tuna uhakika panya hakuna.

Ni juzi tu wametufuata sie wajukuu eti tuwaambie bibi yetu alipandikiza nini ndani ya nyumba (sisi wajukuu wa mwanae wa kike ndio tulikuwa tunaelewana sana na bibi).

Tukawaambia bibi kasema mtoke...mbona sie tukikaa hatupati mauzauza?

Sasa wametoka na nyumba iko shwari, ila wakiingia tu wakwe wa mjomba....ngoma inogile mpaka lyamba.

Ajabu sasa, watoto wa mjomba wakija wanasema wanamuona bibi kakaa kwenye kiambaza katanua mikono ili wasiingie ndani lakini tukija wajukuu sisi wa upande wa mwanae wa kike, wala hatuoni kitu na tunaweza lala usingizi mzuri tu.

Urithi huu....muusikie kwenye bomba tu.
uwiii ...
 
Back
Top Bottom