Pepo baya kwenye mirathi, limepukutisha wengi

Kuna nyumba IPO Ubungo Chai Bora karibu na shule ya Msingi Omwanda aiseee ile nyumba imetanguliza watu balAa
 
Mkiwa na mirathi kwenye familia/ukoo wenu na ikaisha kwa amani na salama ni jambo la kumshukuru Mungu sana.

Niandikapo mada hii leo hii kuna kesi nyingi mahakamani zinazoendelea lakini walioteuliwa kusimamia mirathi hiyo wakikwepa kwenda kwakuwa watangulizi wao wa mirathi hiyo hiyo walikufa kwa namna za ajabu ajabu kabisa.

Mirathi mibaya kabisa inayoteketeza na kutesa wengi ni mirathi ya nyumba, kuna nyumba nyingi tu mpaka leo hazikaliki kisa mirathi, asipokufa mtu basi yeyote atakayelala tu nyumba hiyo ni mauzauza tupu kama si kucharazwa viboko usiku mzima basi utatokewa na vitu vya ajabu ajabu vyenye kutisha mno.

Haya mambo yanahusisha na roho na mapepo mabaya kwa asilimia kubwa sana na roho ya marehemu mhusika ikihusishwa na kuhusika moja kwa moja lakini pia kwa baadhi ya kesi uchawi ukihusika pia.

Kama nilivyosema kuwa nguvu ya giza haitibiki kwa nguvu ya giza wala kwa sheria za binadamu ni vema mambo ya mirathi yakatatuliwa kwa kupewa haki mhusika ambaye kwa mazingira ya kawaida anaonekana ndio kadhulumiwa na mara nyingi huwa ni wanawake wajane watoto wa kambo au ndugu wasio na uwezo lakini kwa utashi wa marehemu akawachagua wao kurithi mali zake.

Kuna kesi moja ya mtu wangu wa karibu kabisa inayohusu mirathi imeshapukutisha watu wanne mpaka sasa akiwemo baba yake mzazi. kisa? Babu yake mzaa baba aliuza nyumba kwa housegirl wake bila maandishi na baada ya kufariki dada wa marehemu akiwa na documents zote muhimu akadai nyumba aliachiwa na kaka yake.

Cha marehemu acheni kibaki cha marehemu hasa nyumba na mkishahisi tatizo tokeni kabisa kwenye taratibu za kisheria za kidunia na mambo ya giza!!mtaishia kumalizana tu.

Kisheria mnaweza kushinda kesi kutokana na nyaraka na wakili na Rushwa lakini baada ya hapo jueni fika kwamba nyumba hiyo haitakalika na pengine haitauzika na ikitokea ikauzika hamtakaa mfaidi hiyo pesa!mabalaa yatawaandameni mwanzo mwisho.

Mkiamua kutumia nguvu za giza ndio shetani atashangilia hasa mtauana mpaka mmalizane.

Cha muhimu na cha lazima kufanya ni kuangalia uhalisia na ukweli ulipo na kumpa anayestahili hata kama ni ghorofa la bei kubwa ili muweze kupona na laana ya mirathi.
Ushauei murua.
 
haya mambo ya urithi me nayaogopa sana lakini najua ipo sku ntakuja kuexperience ugumu wake,mama yangu hii nyumba tunayoishi alirithishwa na bibi yake na kaijenga upya ilikuwa na vyumba viwili vilivyochoka saiv ina vyumba karibu tisa vizuri,sasa ananiambiaga ikitokea amefariki nisiwe legelege nikomae wajomba zangu wasije kuniletea zengwe.Huwa najiuliza maswali mengi mno,kwa mfano"hv kwa nini ndugu wa marehemu huwa wanataka kuwadhulumu urithi watoto wa marehemu? najiuliza ikitokea waseme wana haki si ndo itakuwa mwanzo wa uhasama?
 
Urithi uandikwe mapema kuepusha ya mbeleni, BTW kiwanja ni cha nani? Mna mna mengi ya kunyoosha hapo maneno pekee hayatoshi
 
Kuna nyumba ipo block 41 kinondoni,ukipanga umo nasikia usiku utakula bakora na vifinjo na vibao vya hatari!warithi walizulumiana basi mmoja akasema hatoishi mtu humo mpk wa leo.
Alofanya hayo mambo nae haishi......................................
 
Urithi uandikwe mapema kuepusha ya mbeleni, BTW kiwanja ni cha nani? Mna mna mengi ya kunyoosha hapo maneno pekee hayatoshi
kiwanja cha huyohuyo bibi aliyemrithisha nyumba mama,yani ilitokea bibi yake mama akamrisha nyumba mama yangu (mjukuu wake)wakati mwanake yupo hai.yani mfano wewe mr mshana umrithishe mjukuu wako nyumba wakat mwanako yupo hai kwa sababu za kiusalama,maana alijua akimrithisha mwanae ataiuza nyumba kutokana na kuwa alikuwa anapelekeshwa sana na mke wake kwa hyo ktk urithi akamuandika mjukuu wake ambae ni mama yangu.mama ni wa kwanza kuzaliwa(hao wajomba zangu ni wadogo kwake).
 
Ushauri wangu mwema kwako jitahidi haya yawepo kwenye maandishi na ikiwezekana yapate nguvu ya kisheria
 
its true kabisa!!
ukiwa unaelekea Chamazi Luna kituo kinaitwa "nyumba nyeupe" asili ya hicho kituo ni kua, mzee mmiliki wa hyo nyumba alijenga Ila alidhulumu pesa za mpemba mmoja hv, Huyo mzee Mwenye nyumba alikua muuza kahawa so Sikh Mona akaja mpemba mmoja na kapu lake lenye fedha kunnua kahawa,alivyoondoka akasahau like kapu kumbe lilikua na fedha nyingi,akarudi kuwaambia kua amesahau kapu lake wamrejeshee wakadai hawakuliona,alirudi Siku tatu mfululizo pas na mafanikio..bas baada ya muda kupita ndo yule muuza kahawa akaenda kujenga nyumba kule km unaelekea chamaz akapaka rangi nyeupe!Siku anahamia akafariki,kila ndugu wa yule made aliyehamia pale aliishia kuitwa marehemu ikabdi ndugu waanze Lusaka chanzo cha Vifo vile wakaja kuambiwa na wakaelezwa usalama wao in kumuomba msamaha yule mpemba many Mali but hawakujua watampata wapi!!wakaishia kujuta na mkipangisha while pesa haikai mikononi mwenu inapotea ghafla so mwisho wakawa wanakaa walevi tu wa pombe za mnazi na wagemaji.
HV vtu vipo sana yaaani na mpk Leo mile kituo kinaitwa nyumba nyeupe
 
Kuna mkasa wa siku nyingi kidogo.
Kipindi cha nyerere waliokuwa hawana uraia walifukuzwa ktk nyumba zao hasa wahindi ndo mana hadi leo wahindi hawajengi tanzania!
Sasa kuna mhindi mmoja baada ya kasheshe la kufkuzwa akawa kapoteza passport na visa alikuwa anaenda nairobi baada ya kuona imeshindikana akaamua kurudi ktk nyumba yake usiku na kujinyonga!ikapika kama wiki harufu watu ndo wakagundua basi akazikwa ikapita hiyo!
Jamaa wa kwanza kuhamia akalawitiwa usiku yeye na mkewe!akakimbia kesho yake na vitu akaacha akaamua kuhamia mhindi labda akizani itakuwa shwari na yy akapigwa nao tena usiku kucha kahangaika nao!yaani kila aliehamia alipigwa nao mwisho hadi leo nyumba tupu miaka mingi.
Vipi mshana hapo katest labda wewe itakuwa shwari
 
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji134] [emoji134] [emoji134] [emoji134] [emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Umekacha!hahaha
 
Kim nana sio nyumba tu, hata kwa baadhi ya vyombo vya usafiri au wanyama.

Hii njia kama unaelekea Mkwajuni...kuna Toyo imepaki mwaka wa 3 huu...nasikia mwenye nayo alifariki...mrithi akaiuza, weee, imeua watu 3, mpaka leo imepaki tu.
ila cha ajabu, kila ukiikuta ni safi na anayeisafisha hajulikani.
Uongooo!!!!!!
 
Mkiwa na mirathi kwenye familia/ukoo wenu na ikaisha kwa amani na salama ni jambo la kumshukuru Mungu sana.

Niandikapo mada hii leo hii kuna kesi nyingi mahakamani zinazoendelea lakini walioteuliwa kusimamia mirathi hiyo wakikwepa kwenda kwakuwa watangulizi wao wa mirathi hiyo hiyo walikufa kwa namna za ajabu ajabu kabisa.

Mirathi mibaya kabisa inayoteketeza na kutesa wengi ni mirathi ya nyumba, kuna nyumba nyingi tu mpaka leo hazikaliki kisa mirathi, asipokufa mtu basi yeyote atakayelala tu nyumba hiyo ni mauzauza tupu kama si kucharazwa viboko usiku mzima basi utatokewa na vitu vya ajabu ajabu vyenye kutisha mno.

Haya mambo yanahusisha na roho na mapepo mabaya kwa asilimia kubwa sana na roho ya marehemu mhusika ikihusishwa na kuhusika moja kwa moja lakini pia kwa baadhi ya kesi uchawi ukihusika pia.

Kama nilivyosema kuwa nguvu ya giza haitibiki kwa nguvu ya giza wala kwa sheria za binadamu ni vema mambo ya mirathi yakatatuliwa kwa kupewa haki mhusika ambaye kwa mazingira ya kawaida anaonekana ndio kadhulumiwa na mara nyingi huwa ni wanawake wajane watoto wa kambo au ndugu wasio na uwezo lakini kwa utashi wa marehemu akawachagua wao kurithi mali zake.

Kuna kesi moja ya mtu wangu wa karibu kabisa inayohusu mirathi imeshapukutisha watu wanne mpaka sasa akiwemo baba yake mzazi. kisa? Babu yake mzaa baba aliuza nyumba kwa housegirl wake bila maandishi na baada ya kufariki dada wa marehemu akiwa na documents zote muhimu akadai nyumba aliachiwa na kaka yake.

Cha marehemu acheni kibaki cha marehemu hasa nyumba na mkishahisi tatizo tokeni kabisa kwenye taratibu za kisheria za kidunia na mambo ya giza!!mtaishia kumalizana tu.

Kisheria mnaweza kushinda kesi kutokana na nyaraka na wakili na Rushwa lakini baada ya hapo jueni fika kwamba nyumba hiyo haitakalika na pengine haitauzika na ikitokea ikauzika hamtakaa mfaidi hiyo pesa!mabalaa yatawaandameni mwanzo mwisho.

Mkiamua kutumia nguvu za giza ndio shetani atashangilia hasa mtauana mpaka mmalizane.

Cha muhimu na cha lazima kufanya ni kuangalia uhalisia na ukweli ulipo na kumpa anayestahili hata kama ni ghorofa la bei kubwa ili muweze kupona na laana ya mirathi.

Mgosi Mshana jnr

Hii hili suala limenigusa moja kwa moja na umenikumbusha mbali sana.

Ila naweza kusema suala la urithi si suala la mzaha.

Mimi ni mmoja wa watu ambao tumepitia masuala haya.

Urithi unahitaji mpango mzima na wosia utakaosomeka na kueleweka kwa kila mtu awe mwanasheria au yule wa kutoka kijijini ile Kilulu au Mafere.

Ila suala la mirathi ni gumu sana khasa kama ndugu wengi wanamtegemea marehemu kwa kila kitu.
 
[emoji115] [emoji144] [emoji144]
 
Back
Top Bottom