Mkoroshokigoli
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 14,593
- 5,583
Wakfu,mbona wapo watu wanadhulumuDawa ni kuacha mali zote ziwe za msikiti au kanisa. ...siku inasomwa mirathi wanabaki wanatoa macho
Wakfu,mbona wapo watu wanadhulumuDawa ni kuacha mali zote ziwe za msikiti au kanisa. ...siku inasomwa mirathi wanabaki wanatoa macho
Mi nna mfano wa watu walodhulumu WAQFU BRO @mshana jr binadam waache tuWallah watatamani kucharaza bakora kaburi lako
Mmh unajua hii ni laana...!!! Wakaishia wapi??? Kuna watu wana guts za ajabuMi nna mfano wa watu walodhulumu WAQFU BRO @mshana jr binadam waache tu
mshana jr uko sahihi.
Bibi kafariki kaacha nyumba kubwa sana.
Kaacha watoto wawili tu, marehemu mama yangu na mjomba wangu ambae yuko hai.
Yaani huwezi amini, upande wa wakwe wa mjomba yaani wazazi wa shangazi mke wa mjomba wanaitaka ile nyumba maana wamekuja kukaa,kwani inakalika, wakilala usiku ni mijeredi kwa kwenda mbele.
Wapangaji hawakai, usiku taa zinajiwasha zenyewe...ukiweka umeme wa 50,000 kesho yake unakuta 0.00.
Ukisahau pesa juu ya meza unakuta imeliwa na panya japo tuna uhakika panya hakuna.
Ni juzi tu wametufuata sie wajukuu eti tuwaambie bibi yetu alipandikiza nini ndani ya nyumba (sisi wajukuu wa mwanae wa kike ndio tulikuwa tunaelewana sana na bibi).
Tukawaambia bibi kasema mtoke...mbona sie tukikaa hatupati mauzauza?
Sasa wametoka na nyumba iko shwari, ila wakiingia tu wakwe wa mjomba....ngoma inogile mpaka lyamba.
Ajabu sasa, watoto wa mjomba wakija wanasema wanamuona bibi kakaa kwenye kiambaza katanua mikono ili wasiingie ndani lakini tukija wajukuu sisi wa upande wa mwanae wa kike, wala hatuoni kitu na tunaweza lala usingizi mzuri tu.
Urithi huu....muusikie kwenye bomba tu.
uwiii ...
Duuuh huo uchawi noma hadi kwenye umeme tena wa Luku,muhongo akisikia sijui ata comment vipi?
Listen to your heart.. Hata ukienda nenda Kwa kujiandaaMm nmeitwa na baba mdogo anipe sehemu ya shamba lake japo baba yangu kipindi anaumwa nilmwambia nataka kumtafuta baba mdogo aje ila baba alikataa akaniambia uachane nae hutampata! Baada ya baba kufariki nikaja kukutana nae. Siku hz ananisisitiza niende anipe sehemu ya shamba lake ila mm moyo wangu umekuwa mzito xana wa kwenda. Kila siku namwambia nitakuja. Xx sjuh nifanyeje @mshana jr
uwiii ...
...huyo mganga hawezi fanya yake na sie watu wa Mkwajuni tusalimike?!!Nna rafiki yangu bibi yake mzaa mama aliacha nyumba,sasa wakaja babu zake wanataka khidhulumu,akanambia ataenda kwa mganga ile nyumba isiuzwe,yeyote akija akitaka kuinunua aishie kuiangalia tu,nyumba ipo Mwananyamala.
Hizi mambo bwana @mshana jr kweli zinarun down the streets
nendeni kwa mganga tu aisee...huyo mganga hawezi fanya yake na sie watu wa Mkwajuni tusalimike?!!
...wiki moja tu imebaki,wafilisti wanatujia!
duh inatishaMiss, haya mambo yaone hivihivi tu, kiudani ni ushirikina mtupu
Mkiwa na mirathi kwenye familia/ukoo wenu na ikaisha kwa amani na salama ni jambo la kumshukuru Mungu sana.
Niandikapo mada hii leo hii kuna kesi nyingi mahakamani zinazoendelea lakini walioteuliwa kusimamia mirathi hiyo wakikwepa kwenda kwakuwa watangulizi wao wa mirathi hiyo hiyo walikufa kwa namna za ajabu ajabu kabisa.
Mirathi mibaya kabisa inayoteketeza na kutesa wengi ni mirathi ya nyumba, kuna nyumba nyingi tu mpaka leo hazikaliki kisa mirathi, asipokufa mtu basi yeyote atakayelala tu nyumba hiyo ni mauzauza tupu kama si kucharazwa viboko usiku mzima basi utatokewa na vitu vya ajabu ajabu vyenye kutisha mno.
Haya mambo yanahusisha na roho na mapepo mabaya kwa asilimia kubwa sana na roho ya marehemu mhusika ikihusishwa na kuhusika moja kwa moja lakini pia kwa baadhi ya kesi uchawi ukihusika pia.
Kama nilivyosema kuwa nguvu ya giza haitibiki kwa nguvu ya giza wala kwa sheria za binadamu ni vema mambo ya mirathi yakatatuliwa kwa kupewa haki mhusika ambaye kwa mazingira ya kawaida anaonekana ndio kadhulumiwa na mara nyingi huwa ni wanawake wajane watoto wa kambo au ndugu wasio na uwezo lakini kwa utashi wa marehemu akawachagua wao kurithi mali zake.
Kuna kesi moja ya mtu wangu wa karibu kabisa inayohusu mirathi imeshapukutisha watu wanne mpaka sasa akiwemo baba yake mzazi. kisa? Babu yake mzaa baba aliuza nyumba kwa housegirl wake bila maandishi na baada ya kufariki dada wa marehemu akiwa na documents zote muhimu akadai nyumba aliachiwa na kaka yake.
Cha marehemu acheni kibaki cha marehemu hasa nyumba na mkishahisi tatizo tokeni kabisa kwenye taratibu za kisheria za kidunia na mambo ya giza!!mtaishia kumalizana tu.
Kisheria mnaweza kushinda kesi kutokana na nyaraka na wakili na Rushwa lakini baada ya hapo jueni fika kwamba nyumba hiyo haitakalika na pengine haitauzika na ikitokea ikauzika hamtakaa mfaidi hiyo pesa!mabalaa yatawaandameni mwanzo mwisho.
Mkiamua kutumia nguvu za giza ndio shetani atashangilia hasa mtauana mpaka mmalizane.
Cha muhimu na cha lazima kufanya ni kuangalia uhalisia na ukweli ulipo na kumpa anayestahili hata kama ni ghorofa la bei kubwa ili muweze kupona na laana ya mirathi.
Ndugu wamefanyiana mambo machafu kwasababu ya mirathi wengine wameuana na hata kuwaua wazaziAkili nyingi za waafrika wengi zimejikita penye mirathi.Yaani unatafuta mali kuna ndg zako wanakuwa anamuheshimu mkeo kinafiki siku umezimika wanamtimua nyumbani yaani hapana nawachukia sana wanaosubiri penalty.
Inakera sana unabaki unajiuliza waqt wa marehemu kuna baadhi ya ndugu walikuwa hawatii timu hapo unawaza watu wangapi maisha yao yameharibika baada ya wazazi wao kufariki na walikuwa na uwezo?Ndugu wamefanyiana mambo machafu kwasababu ya mirathi wengine wameuana na hata kuwaua wazazi
Kuna nyumba ipo block 41 kinondoni,ukipanga umo nasikia usiku utakula bakora na vifinjo na vibao vya hatari!warithi walizulumiana basi mmoja akasema hatoishi mtu humo mpk wa leo.Nna rafiki yangu bibi yake mzaa mama aliacha nyumba,sasa wakaja babu zake wanataka khidhulumu,akanambia ataenda kwa mganga ile nyumba isiuzwe,yeyote akija akitaka kuinunua aishie kuiangalia tu,nyumba ipo Mwananyamala.
Hizi mambo bwana @mshana jr kweli zinarun down the streets
Halafu wewe ulikuwa mpendwa Wa bibiHapana ya huku Kinondoni