mshana jr uko sahihi.
Bibi kafariki kaacha nyumba kubwa sana.
Kaacha watoto wawili tu, marehemu mama yangu na mjomba wangu ambae yuko hai.
Yaani huwezi amini, upande wa wakwe wa mjomba yaani wazazi wa shangazi mke wa mjomba wanaitaka ile nyumba maana wamekuja kukaa,kwani inakalika, wakilala usiku ni mijeredi kwa kwenda mbele.
Wapangaji hawakai, usiku taa zinajiwasha zenyewe...ukiweka umeme wa 50,000 kesho yake unakuta 0.00.
Ukisahau pesa juu ya meza unakuta imeliwa na panya japo tuna uhakika panya hakuna.
Ni juzi tu wametufuata sie wajukuu eti tuwaambie bibi yetu alipandikiza nini ndani ya nyumba (sisi wajukuu wa mwanae wa kike ndio tulikuwa tunaelewana sana na bibi).
Tukawaambia bibi kasema mtoke...mbona sie tukikaa hatupati mauzauza?
Sasa wametoka na nyumba iko shwari, ila wakiingia tu wakwe wa mjomba....ngoma inogile mpaka lyamba.
Ajabu sasa, watoto wa mjomba wakija wanasema wanamuona bibi kakaa kwenye kiambaza katanua mikono ili wasiingie ndani lakini tukija wajukuu sisi wa upande wa mwanae wa kike, wala hatuoni kitu na tunaweza lala usingizi mzuri tu.
Urithi huu....muusikie kwenye bomba tu.