Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 373,200
- 864,574
Mkiwa na mirathi kwenye familia/ukoo wenu na ikaisha kwa amani na salama ni jambo la kumshukuru Mungu sana.
Niandikapo mada hii leo hii kuna kesi nyingi mahakamani zinazoendelea lakini walioteuliwa kusimamia mirathi hiyo wakikwepa kwenda kwakuwa watangulizi wao wa mirathi hiyo hiyo walikufa kwa namna za ajabu ajabu kabisa.
Mirathi mibaya kabisa inayoteketeza na kutesa wengi ni mirathi ya nyumba, kuna nyumba nyingi tu mpaka leo hazikaliki kisa mirathi, asipokufa mtu basi yeyote atakayelala tu nyumba hiyo ni mauzauza tupu kama si kucharazwa viboko usiku mzima basi utatokewa na vitu vya ajabu ajabu vyenye kutisha mno.
Haya mambo yanahusisha na roho na mapepo mabaya kwa asilimia kubwa sana na roho ya marehemu mhusika ikihusishwa na kuhusika moja kwa moja lakini pia kwa baadhi ya kesi uchawi ukihusika pia.
Kama nilivyosema kuwa nguvu ya giza haitibiki kwa nguvu ya giza wala kwa sheria za binadamu ni vema mambo ya mirathi yakatatuliwa kwa kupewa haki mhusika ambaye kwa mazingira ya kawaida anaonekana ndio kadhulumiwa na mara nyingi huwa ni wanawake wajane watoto wa kambo au ndugu wasio na uwezo lakini kwa utashi wa marehemu akawachagua wao kurithi mali zake.
Kuna kesi moja ya mtu wangu wa karibu kabisa inayohusu mirathi imeshapukutisha watu wanne mpaka sasa akiwemo baba yake mzazi. kisa? Babu yake mzaa baba aliuza nyumba kwa housegirl wake bila maandishi na baada ya kufariki dada wa marehemu akiwa na documents zote muhimu akadai nyumba aliachiwa na kaka yake.
Cha marehemu acheni kibaki cha marehemu hasa nyumba na mkishahisi tatizo tokeni kabisa kwenye taratibu za kisheria za kidunia na mambo ya giza!!mtaishia kumalizana tu.
Kisheria mnaweza kushinda kesi kutokana na nyaraka na wakili na Rushwa lakini baada ya hapo jueni fika kwamba nyumba hiyo haitakalika na pengine haitauzika na ikitokea ikauzika hamtakaa mfaidi hiyo pesa!mabalaa yatawaandameni mwanzo mwisho.
Mkiamua kutumia nguvu za giza ndio shetani atashangilia hasa mtauana mpaka mmalizane.
Cha muhimu na cha lazima kufanya ni kuangalia uhalisia na ukweli ulipo na kumpa anayestahili hata kama ni ghorofa la bei kubwa ili muweze kupona na laana ya mirathi.