yani anashikilia kiapo cha ndoa kidhati kabisa
inataka moyo kuishi na mume kama huyo mtu had mtoto wake hana imani naye n mtihani
Kanogewa mauaji ssPENZI LENYE MAUMIVU-09
Mtunzi:Juma Hiza
Simu:0712988278
Maneno ya Lydia yaliendelea kuniumiza sana moyo wangu, aliponiambia kuwa Christopher alipanga Magomeni Mapipa na Getrude ndiye ambaye aliyekuwa akimuhudumia kila kitu nilihisi kuchanganyikiwa.
Nilichokiamini kwa muda huo ni kwamba pesa zangu ambazo nilikuwa nikimpa Getrude ndizo ambazo zilitumika kumuhudumia Chistopher kwa upande wa pili. Hilo lilizidi kuniumiza mno.
Lydia hakutaka kuwa mzungumzaji sana, alichoamua kukifanya ni kunionyesha picha ya Christopher kwenye simu yake.
“Huyo hapo,” aliniambia baada ya kunionyeshea picha ya Christopher. Nilizidi kushikwa na hasira baada ya kumuona mwanaume ambaye alikuwa akizitumia pesa zangu.
Sikutaka kupoteza muda, nilimwambia Lydia anitumie picha hiyo WhatsApp kisha akafanya kama nilivyomwambia. Baada ya mazungumzo kumalizika nilimpatia pesa kiasi cha shilingi milioni moja kutokana na kazi nzuri aliyokuwa ameifanya, alifurahi mno baada ya kumpatia kiasi hicho cha pesa, akaniahidi kunipa ushirikiano kwa msaada wowote ambao ningeuhitaji kutoka kwake.
“Usijali kuhusu hilo,” nilimwambia.
“Ok shem,”aliniambia.
Uso wangu ulitawaliwa na furaha, nilifahamu fika kazi iliyokuwa imebakia mbele yangu haikuwa na ugumu tena kama ilivyokuwa hapa mwanzoni.
Mpaka kufikia muda huo Lydia hakufahamu ni tukio gani ambalo nilikuwa nikienda kulifanya kwa Christopher na laiti kama angefahamu nadhani asingekubali kunipa taarifa za Christopher.
Roho ya mauaji ilikuwa imeshaniingia, sikuwa na huruma hata kidogo, nilichokuwa nikihitaji kukiona ni mwili wa Christopher ukiwa maiti, hiyo ndiyo ilikuwa furaha yangu, nilitaka afe tena kifo cha kikatili.
Kuhusu hilo wala sikuwa na mashaka yoyote, nilichokifanya nilimtafuta jamaa mmoja aliyejulikana kwa jina la Maxwell, alikuwa akiishi Kinondoni. Aliogopeka mno kwa kinondoni nzima.
Michezo yote michafu aliifahamu na yeye ndiyo aalikuwa akitumika katika matukio mbalimbali hususani ya utekaji. Nilipokutana naye nilimpa dili la mauaji, nilihitaji kuona akimuua Christopher.
Baada ya kumpa picha yake pamoja na kumwambia mahali ambapo alikuwa akiishi alihitaji nimlipe kiasi cha shilingi milioni hamsini. Aliponiambia kuwa alihitaji kiasi hicho cha pesa nilitabasamu, nilikiona ni kiasi kidogo mno ukilinganisha na kiasi cha pesa ambacho nilikuwa nikimiliki katika akaunti yangu benki.
Kutokana na hitaji langu kubwa la kuona Christopher akiuwawa nilimuahidi kumlipa kiasi cha shilingi milioni themanini za kitanzania. Akaonekana kufurahi, hii ilikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza kumuona Maxwell akitabasamu tangu nilipokutana naye, muda wote alikuwa ameikunja sura yake iliyoonekana kuwa ngumu na yenye kutisha.
“Huu ni mwaka wa kumi sasa nimekuwa nikiifanya kazi hii ya kutoa roho za watu hivyo tegemea kazi yako ikifanikiwa kwa asilimia mia moja,” aliniambia Maxwell.
“Nitafurahi sana,” nilimwambia huku nikikenua.
“Usijali mkuu baada ya siku mbili utaikuta maiti yake ufukwe wa coco,” aliniambia Maxwell maneno yaliyozidi kunifurahisha mno.
Hakukuwa kuna mtu aliyefahamu kile kilichokuwa kikiendelea, hata kwa upande wa mke wangu hakufahamu kitu chochote. Baada ya kupita siku mbili bila kupata taarifa zozote kutoka kwa Maxwell kama alivyoniahidi nilianza kuingiwa na wasiwasi. Nilihisi labda mpango wa kumuua Christopher ulishindikana, hilo lilinisononesha, sikutaka kuamini kama hilo liliwezekana kutokea.
Muda wote nilikuwa makini kuitazama simu yangu kuona kama Maxwell angenipigia na kunipa taarifa za kufanikiwa mpango wa kumuua Christopher. Yaani kwa jinsi nilivyokuwa makini kuitazama simu yangu siku hiyo ilikuwa ni kama mtu aliyekuwa akisubiria meseji ya ushindi ambao angeupata mara baada ya kubeti.
Usiku wa siku hiyo majira ya saa saba nilipokea ujumbe mfupi kutoka kwa Maxwell, aliniandikia maneno machache ya kingereza “I’m Done,” yaliyomaanisha kwa Kiswahili (Nimemaliza).
Sikutaka kuamini hilo, nilihitaji kuthibitisha na kama nilivyohitaji Maxwell alinitumia picha za mwili wa Christopher ambaye tayari alikuwa maiti.
“Kazi nzuri sana kwahiyo maiti yake umeende kuitelekeza coco beach?” nilimuuliza.
“Ndiyo asubuhi watakuta mzoga wao,” alinijibu.
“Aisee umenifurahisha mno, sikutegemea kwa kweli.”
“Nilikwambia kazi yako lazima ifanikiwe kwa asilimia mia moja,” aliniambia.
Kadri nilivyozidi kuzungumza na Maxwell ndivyo ambavyo furaha ilizidi kunitawala, hakika kifo cha Christopher kilionekana kuwa sababu ya furaha yangu kwa wakati huo.
Siku iliyofuata wala sikutaka kupoteza muda, kama nilivyomuahidi, nilimlipa pesa zake kupitia akaunti yake benki na huo ndiyo ulikuwa mwanzo wangu wa kufanya kazi na Maxwell, nilimuhitaji zaidi na zaidi katika kazi zangu nyingine.
****
Mke wangu Lillian alikuwa ni muumini wa kanisa la Praise and Worship lililokuwepo Mwenge jijini Daresalaam. Aliamua kumkabidhi maisha yake Mungu kwani aliamini yeye ndiye pekee ambaye alikuwa na uwezo wa kumponya Brighton.
Kilikuwa ni kipindi ambacho alisali na kumuomba Mungu kwa nguvu zote lakini pia hakuacha kuiombea amani na furaha ya ndoa yetu ambayo ilionekana kurejea kwa kipindi hicho.
Nilipokuwa nyumbani hakuacha kunikumbusha uwepo wa Mungu katika maisha yangu, alipomaliza kuniambia hayo aliniomba nifunge macho kisha maombi yakaanza. Hayo yote hayakuonekana kuniingia akilini mwangu, japokuwa kila ambalo alilokuwa akihitaji nifanye nilifanya kwa muda huo lakini siri iliyokuwepo moyoni mwangu niliijua mimi peke yangu pamoja na Mungu.
“Asante Mungu kwa kuirudisha furaha ya ndoa yangu,” alisema Lillian huku akiwa ameyafunga macho yake, wakati huo nilikuwa nikimtazama, moyoni mwangu nikajisemea laiti kama ungejua sikupendi wewe pamoja na huyo mwanao wala usingejisumbua hata kumshukuru huyo unayemuita ni Mungu wako.
****
Taarifa zilizagaa kila kona kuhusu tukio la kukutwa maiti ufukwe wa coco, ilikuwa ni maiti ya Christopher. Vyombo mbalimbali vya habari, magazeti nayo hayakuwa mbali kuripoti habari za mauaji yao yaliyoonekana kuwa ya kikatili.
Mwili wa Christopher ulikutwa ukiwa umejeruhiwa vibaya mno sehemu mbalimbali za mwili wake kisha ukiwa ndani ya kiroba. Kila aliyeishuhudia maiti yake hakutaka kuamini, yalikuwa ni mauaji ya kikatili.
Jeshi la polisi likaingilia kati, hakukuwa kuna mtu aliyemfahamu muuaji aliyehusika na mauaji mpaka kufikia muda huo. Hatimaye msako wa kumtafuta muuaji kila kona ukaanza.
Lydia ndiye mtu wa kwanza ambaye aligundua kuwa mimi ndiye niliyesababisha kifo cha Christopher kwani mazingira ambayo Christopher aliuliwa pamoja na siku ile ambayo nilihitaji taarifa zake yalikuwa ni matukio mawili ambayo aliyafananisha.
Hilo lilianza kunipa wasiwasi, niliamini kwa vyovyote ni lazima Lydia angemweleza ukweli Getrude na hata kwenda polisi kutoa ushahidi kwa kile kilichokuwa kimetokea.
Kitendo cha kumuona Lydia akiendelea kuishi kilinihatarishia maisha yangu, sikutaka kujiuliza mara mbilimbili, nilichopanga kukifanya ni kama nilivyofanya kwa Christopher na yeye nilitaka afe ili siri iendelee kubaki ni yangu.
Je, nini kitaendelea?
K