Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,400
- 465,165
mapenzi mafala san hahahaha
Asante mpenzi ila dominick mngese sana wala hata sijamuonea huruma*PENZI LA UMAUTI-13*
Mtunzi:Juma Hiza
Maneno ya Chris yalizidi kuniumiza sana, nilikumbuka mambo mengi ambayo yalitokea katika maisha yangu, jinsi ambavyo nilipigana kiume mpaka nikahakikisha nafanikiwa kumuoa Julieth japo alisababisha mpaka nikagombana na Mama yangu lakini hilo sikutaka kujali.
Licha ya mapenzi yote ambayo nilimuonyesha na kumthamini kama mke wangu wa ndoa lakini ghafla! alikuja kubadilika.
Alibadilika katika kipindi ambacho nilikuwa nampenda sana, sikutarajia kama angeweza kubadilika katika kipindi kile nilichokuwa namuhitaji zaidi.
Sikutaka kuweka mlolongo mrefu wa mazungumzo kati yangu na Chrispine, aliponiambia kuwa alikuwa akinionea huruma kwa yale yaliyokuwa yakinitokea nilimwambia asijali hivyo abaki na amani, niliamini kile kilikuwa ni kipindi cha mpito na muda wowote kingeweza kufika mwisho.
Nilimuaga Chrispine kisha nikaondoka kuelekea nyumbani kwangu, barabarani nilikuwa mwingi wa mawazo sana, kuna muda nilikuwa nikiongea peke yangu kama mwendawazimu.
Nilipofika nyumbani nje nililiona gari alilodai mke wangu kuwa ni lake, nikalitazama kwa muda wa sekunde kadhaa kisha nikaingia ndani, nikamkuta mke wangu akiwa amekaa sebuleni, alionekana kunisubiri kwa hamu kubwa sana.
Wakati huo Glory alikuwa ameshaenda shule.
“Umetoka wapi?” bila hata salamu aliniuliza huku akiwa ameikunja sura yake kwa ghadhabu.
“Bila hata salamu mke wangu?” nilimuuliza kwa sauti ya upole.
“Salamu ya kazi gani sasa au itakusaidia nini, nimekuuliza umetoka wapi?” aliniuliza.
“Nimetoka kwa Chris,” nilimjibu.
“Kwa Chris?” aliniuliza.
“Ndiyo,” nilimjibu.
“Kwahiyo unataka kuniambia jana umelala huko huko?”
Kila swali nililokuwa nikimjibu mke wangu nilimjibu kwa sauti ya upendo lakini nilishagazwa na muonekano wake, alionekana kutawaliwa na hasira na yote ilisababishwa na kutorudi kwangu nyumbani, nilipomuuliza kuhusu mwanangu Glory alishindwa kunijibu alikuwa shule mwisho tukaingia katika ugomvi.
Alidai kuwa amenichoka na hivyo hakutaka kuendelea na mimi tena, kama ni ndoa basi ule ndiyo ulikuwa mwisho wake wa uvumilivu.
Hakutaka kuendelea kuumiza akili yake juu ya vitu ambavyo havikuwa na msingi katika maisha yake.
Sio siri nilishangazwa na maamuzi aliyokuwa ameyachukua mke wangu, nikazidi kumuona kuwa mwanamke wa tofauti sana hasa ukilanganisha muonekano wake, kazi yake pamoja na mambo aliyokuwa akiyafanya vilikuwa ni vitu viwili tofauti.
Kwakweli nilizidi kuchanganyakiwa kutokana na uamuzi aliyokuwa ameuchukua mke wangu, nilikuwa nampenda sana japo alianza kunifanyia visa lakini sikutaka kuupunguza upendo niliyokuwa nao kwake.
Kwa wakati ule ambapo alikuwa ameniambia amenichoka na kutaka tuachane nilijaribu kumsihi asichukue maamuzi hayo kwani tayari tulikuwa tumejaaliwa kupata mtoto katika maisha yetu na alikuwa akitutegemea kwa kila kitu, sikutaka Glory apoteze muelekeo wa maisha yake baada ya kuachana kwetu, nikajaribu kumsihi mara mbilimbili asichukue uamuzi huo mgumu ambao ungeweza kumuathiri kisaikolojia.
“Tafadhali mke wangu naomba usichukue uamuzi huo, mimi bado nakupenda sasa kwanini unataka kunipa hukumu nisiyoistahili?” nilimuuliza kwa sauti ya kulalamika, nilikuwa nikiyalalamikia mapenzi ya mke wangu na kwa wakati huo hakuonekana kujali, alikuwa amenikinai.
“Sitaki Dominick naomba tuachane nimekuchoka,” aliniambia huku akinionyesha hasira za waziwazi.
Kuna wazo lilinijia kichwani na nilihitajika kulifanyia kazi kwa wakati huo ili kuinusuru ndoa yangu ambayo ilikuwa inaendea kuangamia.
MSAMAHA hili ndilo wazo lililonijia kichwani kwa wakati huo, nilichoamua kukifanya ni kuanza kumuomba msamaha mke wangu. Niliamua kufanya hivyo ilimradi amani ya mapenzi yetu ya ndoa irejee kama hapo awali lakini naweza kusema haikuwa kama nilivyodhani.
****
Huo ndiyo ukawa mwanzo wa kuyapokea maumivu mengine yaliyouumiza moyo wangu wa mapenzi, Julieth aligeuka kuwa ncha ya kisu kikali na kisha akawa ananichomachoma moyoni mwangu.
Nilikuwa nikiyapokea maumivu makali ambayo sikuyatarajia katika maisha yangu. Hatimaye ya mapenzi niliyoyafananisha na simulizi nzuri ya kimapenzi iliweza kugeuka kuwa simulizi ya kusikitisha.
Kipindi ambacho Julieth alikuwa amebadilika na kuwa mbogo ndani ya nyumba nilianza kuyasikia maneno ya chinichini ya watu wakisema alikuwa akitembea na wanaume mbalimbali wenye pesa ambao ndiyo walikuwa wakimuhonga magari pamoja na pesa.
Sikutaka kuamini macho yangu pale nilipoziona picha za Julieth mitandaoni akiwa kitandani na mwanamuziki maarufu aliyekuwa akijulikana kwa jina la Gibson David lakini alifahamika zaidi kama G Malove.
Nilihisi kuchanganyikiwa baada ya kusikia Julieth alikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Gibson na kibaya zaidi alikuwa ana ujauzito wake. Maumivu hayakuishia hapo tu, Mwanamuziki huyo alimpangia nyumba pamoja na kumfungulia biashara mbalimbali mke wangu.
Kilichokuwa kimetokea katika maisha yangu kilimsikitisha sana rafiki yangu Chrispine, alinionea huruma sana kutokana na madhila niliyokuwa nimeyapata.
Hakutaka kuamini kama Dominick niliyekuwa nikiishi maisha ya kuifurahia ndoa yangu wakati huo nilikuwa nikiteseka, nikinyanyasika, nikiumizwa na ndoa yangu.
Ulifika wakati nilikosa mtetezi wa kunitetea si kwa Chrispine tu! bali hata kwa upande wa Mama yangu mzazi hatukuwa na mawasiliano mazuri, tuligombana na sababu kubwa alikuwa ni mke wangu.
“Hutakiwi kuendelea kuwa mnyonge inabidi ufanye maamuzi katika hili,” aliniambia Chrispine.
“Hivi kweli mke wangu anaweza akanifanyia unyama huu?” nilimwambia Chrispine kisha nikamuuliza swali ambalo lilinifanya nidondokwe na machozi, nilikumbuka mambo mengi niliyowahi kuyafanya kwa mke wangu lakini yalionekana kuwa ni bure, hayakuwa na faida yoyote kwa wakati huo.
“Najisikia vibaya sana ndugu yangu najua unapitia katika wakati wa maumivu kiasi gani lakini huna budi kukubaliana na hali halisi, yule mwanamke ni muuaji kweli, hana utu kabisa,” aliniambia Chrispine.
“Lakini angeniambia mapema kuwa amenichoka, nimewekeza dhamana ya upendo, uvumilivu na kujitoa lakini mwisho wa siku amekuja kunilipa maumivu, amenilipa dharau nadharaulika mimi kila kona, naonekana labda pengine simridhishi mke wangu na ndiyo sababu amenisaliti,” nilimwambia Chrispine huku machozi yakiendelea kunibubujika mashavuni mwangu.
“Usiseme hivyo,” aliniambia Chrispine.
“Kwanini anasahau wema wangu wote niliyomtendea katika maisha yake, kwanini anasahau kwamba tuna mtoto mdogo ambaye anatutegemea, kwanini anachukua kunipa hukumu hii?
Anasahau kuwa yeye ndiyo chanzo cha mimi kugombana na Mama yangu, kwanini amesahau mapema kiasi hiki?” nilimuuliza Chrispine huku nikiendelea kudondokwa na machozi mfululizo.
Nililia sana, niliumia mno wala maumivu yangu sidhani kama kulikuwa kuna mtu wa kuyatibu kwa wakati ule. Nilitokea nikayachukia mapenzi, nikayawekea uadui mkubwa mno.
Niliyekuwa namsikia akiyasifia mapenzi nilimuona kuwa kipofu asiyeona mbele ni kitu gani kilichokuwa kinakwenda kumtokea, mimi nilikuwa mfano bora wa kuwasimulia yale yaliyowahi kunikuta katika maisha yangu, nilikuwa kipofu wa mapenzi.
Nakumbuka nyumba niliyopanga kujenga kisirisiri, ilinishinda mwisho wa siku nikaamua kuiuza.
****
Baada ya mambo yote hayo kutokea katika maisha yangu niliamua kwenda nyumbani kwa Mama yangu kwa lengo kwa kuomba msamaha. Nilichokutana nacho baada ya kwenda nyumbani kwa Mama yangu huku nikiwa na mwanangu ni kaburi ambalo niliambiwa alizikwa hapo miaka miwili iliyopita.
Kiukweli sikutaka kuamini kwa kile nilichokuwa nikielezwa na majirani, nilihisi kuchanganyikiwa, hakukuwa na kitu kingine zaidi ya machozi ya uchungu, nilimlilia Mama yangu ambaye alikufa bila kusema neno lolote na mimi, alikufa huku akiwa ananichukia, niliumia mno.
****
Niliporudi nyumbani kwangu sikuonekana kuwa mwenye furaha hata kidogo, nilikuwa mnyonge sana na kila wakati taswira ya kaburi la Mama yangu ilikuwa ikinijia kichwani.
Sijui niseme nini ila naweza kusema nilichanganyikiwa na kila nililokuwa nalifanya haikuwa ni akili yangu kwa wakati huo.
Usiku wa siku hiyo mke wangu hakurudi tena nyumbani, nikabaki nikitabasamu huku nikiamini alikuwa na huyo mwanamuziki wake.
“Kwako Chrispine,
Najua utashtushwa na aina ya maamuzi ambayo nimeamua kuyachukua, sina maana kwamba nimeshindwa kuyavumilia hapana ila imebidi iwe hivi.
Najisikia kufanya mauaji na sitaki kusabababisha mauaji kwa damu isiyokuwa na hatia. Najiona nikielekea mahali pabaya sana na hakuna wakunisaidia.
Nimeteseka sana katika kupigania maisha ya mke wangu lakini mwisho wake amekuja kunilipa zawadi ya maumivu, amenipa jeraha la mapenzi na sijui kama nitaweza kupona.
Najua nitaishangaza dunia kwa maamuzi yangu haya ninayokwenda kuyachukua lakini kabla sijayachukua naomba uyafanyie kazi haya nitakayokuandikia.
Hakikisha unasimamia vyema biashara zangu, hakikisha unabaki na mwanangu Glory, naamini ninamuacha katika mikono salama.
Nachukua maamuzi ya kujiua lakini nitakapokufa hakikisha nazikwa pembeni na kaburi la Mama yangu pengine kwa kufanya hivyo nitapata wasaa wa kuzungumza naye na kumuomba msamaha kwa mara nyingine. Atanisamehe.
Maiti yangu chonde tafadhali hakikisha mke wangu haisogelei, sitaki tukio hili litokee katika msiba wangu kwa maana yeye ndiyo chanzo cha yote haya na kama utapata bahati ya kuisoma barua hii basi usiache kumwambia mke wangu kuwa nakufa huku nikiwa namchukia sana.
Ni mimi mfu Dominick.”
Ilikuwa ni barua iliyoambatana na simulizi ya maisha aliyoiandika Dominick, kifo chake hakika kilimsikitisha kila mtu. Marehemu Dominick alijiua kwa kujinyonga na kifo chake kilisababishwa na mapenzi.
MWISHO.
Asanteni nyote mliyokuwa nami kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa simulizi hii ya maisha. Hii ni simulizi ya kweli iliyowahi kutokea katika maisha.
Mwisho wa simulizi hii ndiyo mwanzo wa simulizi nyingine nzuri na yenye mafunzo mengi.
Imeandikwa na mwandishi Juma Hiza.
*PENZI LA UMAUTI-13*

Asante mpenzi ila dominick mngese sana wala hata sijamuonea huruma
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji120][emoji120][emoji120]Rest in peace bro Dominicky.
Hii story, ipo more realistic....kiukweli imenigusa sana.
Asante sana Shunie
#Chizoba
Sent using Jamii Forums mobile app