~~Penzi la Kumegeana~~ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

~~Penzi la Kumegeana~~

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 10, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 10, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Penzi la kumegeana, si penzi la kupeana,
  Penzi la kutegeana, kwa kibaba kupeana,
  Penzi la kutishiana, la nini la kugawana?
  Penzi la kumegeana, si penzi hilo hiana!

  Penzi la kumegeana, ni penzi la kuchokana
  Penzi la kuringishana, hilo la kuchomoana,
  Penzi la kutafutana, ni mwiba wa kuchomana,
  Penzi la kumegeana, si penzi hilo hiana!

  Penzi la kumegeana, ni penzi la kutesana,
  Penzi la kuudhiana, ni penzi la kushindana,
  Penzi la kunyimiana, mabaya kutafutana,
  Penzi la kumegemeana, si penzi hilo hiana!

  Penzi la kumegeana, la vipande kugawana,
  Penzi la kutukanana, ni penzi la kuumizana,
  Penzi la kukorogana, siyo penzi la mwanana,
  Penzi la kumegeana, si penzi hilo hiana!

  Penzi la kumegeana, la sirini kuitana,
  Penzi la kukimbizana, la mwingine kugawana,
  Penzi la kuchakuana, gizani kutafunana,
  Penzi la kumegeana, si penzi hilo hiana!

  Penzi la kumegeana, mwenzenu ninalikana,
  Penzi la kuulizana, maswali ya kiaina,
  Penzi la kuudhiana, na vidonda vikatona,
  Penzi la kumegeana, si penzi hilo hiana!

  Ukitaka kweli penzi, sitake la kumegeana!
  Tafuta wako muenzi, mpende mkapendana,
  Awe wako wa aziz, wa penzi lililoshibana,
  Penzi la kumegeana, si penzi hilo hiana!


  Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
   
  Last edited by a moderator: Jul 12, 2009
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  MKJJ,
  i hope kwamba utakuwa na stock kubwa ya mashairi,why dn't you compile a book?u cn do it men,then yatatumika wizara ya elimu.

  Kwasasa kuna uhaba mkubwa sana wa washairi,na baraza la mtihani linarudia rudia tu vitabu.

  MAKE USE OF U R TALENT BWANA
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Jul 10, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  shukrani.. lakini hata vitabu si vitakuwa vya bure.? watu wafurahie tu siku moja mtu mwingine ataamua kuyakusanya.
   
 4. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  is that so?vitabu vya bure how?iwapo tu wakubwa wizarani wataarpove basi umeula!cha muhimu print vitabu vyako hata kopi kumi tu peleka wizarani pale,na hapa TUKI,wavifanyie assessments then we pray for the best wavikubali!

  Hamna ishu ya bure bwana!
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jul 11, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  nashukuru kwa kunipa moyo; nataria kutoa vitabu vitatu kabla ya uchaguzi mkuu! Tatizo ndiyo hilo inabidi nigawe bure wabongo hawanunui.. na wakinunua basi wanaazimana utadhani maktaba!
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Jul 11, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Sasa hao TUKI wanapatikana vipi?
   
 7. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #7
  Jul 12, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ahsante

  mimi huwa napenda kukusanya kazi zako zote popote ninoziona kwa ajili ya kuhifadhi tuki wako chuo kikuu cha dsm Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili au tembelea pia mkahawa wa vitabu Untitled Document hiyo ni cafe ya watu wanaopenda kusoma wanaweza kukusaidia pia unaweza kuweka kazi zako pale
   
 8. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Naaaaaaaaam! Manshallah
   
 9. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  MKJJ una kipaji sana keep ur spirit up 4ever
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Jul 12, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  thank you very much.
   
 11. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Swadakta
   
 12. GP

  GP JF-Expert Member

  #12
  Jul 14, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  kila siku kupigana, ni aibu barazani,
  hamuishi kutukanana, matusi mazito ya nguoni,
  hakuna kuheshimiana, nyumba ikawa na amani,
  penzi la kumegeana, ni baya sana jamani.

  kalamu naweka chini, pumzi imekata kifuani,
  wangu usia usikieni, wakike na wa kiumeni,
  penzi la mafichoni, baya si kama hadharani,
  penzi la kumegeana, ni baya sana jamani.
   
 13. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #13
  Jul 14, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hapana chako na changu, hivi vyote ni shirika
  Mimi wako wewe wangu, kipi cha kugawanyika?
  Kuungana walimwengu, ni neno lenye mwafaka,
  Linapendeza kwa Mungu, pamoja na malaika

  Kukwambia nenda zangu, sithubutu kutamka,
  Na kadhalika mwenzangu, sidhani hilo wataka,
  "Hutaki" lina uchungu, na kwangu ni kadhalika.
  Dunia ina mizungu, nikwambiayo kumbuka.
   
 14. Kyakya

  Kyakya JF-Expert Member

  #14
  Jul 14, 2009
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 397
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mliyonena ni kweli, kayafundisha Mwenyezi,
  Tuache kuwa tapeli, kwa kumegeana penzi,
  Tupeane kwelikweli, si mara moja kwa mwezi,
  Penzi la kumegeana, alifai asilani.
   
 15. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #15
  Jul 14, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mkuu Shy,

   
 16. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #16
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Haya mzee..nimekupata vilivyo. Mimi namegewa penzi kwahiyo shairi lako limepiga kumoyo
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Jul 14, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  sasa mkuu fuata ushauri wa Barubaru.. wengine tulishajaribu hayo ya kugawa matokeo yake ni maumivu tu.
   
 18. GP

  GP JF-Expert Member

  #18
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hodi hodi jamvini, kwakasi kubwa leo nakuja,
  nguvu nyingi mwilini, kama mabomu ya faluja,
  ari nayo akilini, ndio inipayo na ujanja,
  penzi la kumegeana, si penzi hilo hiana

  magonjwa ni mengi, ukimwi ni namba wani,
  shule za msingi, umetapakaa hadi vyuoni,
  vijana kwa madingi, mijini mpaka vijijini,
  penzi la kumegeana, si penzi hilo hiana.

  penzi la kumegeana, ni penzi la kifisadi,
  mashaka tele kupeana, si kutongozana hata miadi,
  penzi dhahiri kukosekana, ukibisha muulize mchukia_fisadi,
  penzi la kumegeana, si penzi hilo hiana

  dada belinda sikia, kuna mjanja yo-yo usimmegee,
  hata kwalolote akikwambia, usiruhusu akusogelee,
  nyaningabu na mpitanjia, jihadhari usiwape wachekelee,
  penzi la kumegeana, si penzi hilo hiana

  mama joe heshima kwako, nyingi sana kama kilo,
  usigawe penzi lako, kwa bujibuji au masanilo,
  siwasahau asilani mamaparoko, mzee mwanakijiji na lunanilo
  penzi la kumegeana, si penzi hilo hiana.

  kuna mambo ya tigo, vijana siku hizi ndio mtindo,
  ndugu yangu kigogo, haraka mjulishe hata invizibo,
  kumegeana hata tigo, siku hizi ndio mtindo,
  penzi la kumegeana, si penzi hilo hiana.

  ingawa la kumegeana, wanasema tamu kama asali,
  lakini mgoni akijulikana, kipigo lazima kulazwa hospitali,
  manundu usoni yamelundikana, afya yake haina hali,
  penzi la kumegeana, si penzi hilo hiana.

  cha mtu ni mavi, wahenga walitwambia,
  usimege kama kiwavi, utakuja jijutia,
  upatwapo na kimavi, usiseme George_Porjie sijakwambia,
  penzi la kumegeana, si penzi hilo hiana.


  mwanajamiiOne anajua hatari kumegemeana, hata masanilo alitoswa,
  wasingeweza kuelewana, mwanajamiiOne hapendi kunyanyaswa,
  alijua wasingeshibana, mchakamchaka angepelekeshwa,
  penzi la kumegeana, si penzi hilo hiana.
   
  Last edited: Jul 15, 2009
 19. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #19
  Jul 15, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Georgie ... mbona?
   
 20. GP

  GP JF-Expert Member

  #20
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  mbona nini?
   
Loading...