Swali langu kwako: Je penzi lako ni la ndoa au la kustarehesha miili ya watu?

mxsdk

JF-Expert Member
Aug 11, 2014
3,585
2,045
“Hapana huyu si mume wangu, ila niko naye tu kwa ajili ya kujipumzisha” “Aah, yule msichana wa jana usiku? Siyo mchumba wangu, ‘nazuga’ naye tu, mchumba wangu yuko masomoni.” “Hapana yule ni ‘demu’ wangu mwingine, mwenyewe amesafiri” Hizi ni baadhi ya kauli ambazo watu huzitaja kuelezea namna wanavyowachukulia wapenzi wao.

Je ulishawahi kujiuliza wewe ni nani kwa mpenzi wako, ni wa ndoa au wa kustarehesha mwili?
Uchunguzi unaonyesha kuwa wanaume wengi wanafahamu mapema zaidi jibu la swali hili kutokana na kanuni za kimapenzi kuwapa nafasi ya kuanzisha uhusiano, tofauti na wanawake hasa wa kiafrika ambao husubiri kutongozwa.

Hii ina maana kuwa, wanaume hutambua mapema kuwa mwanamke wanayemtafuta kwa wakati huo huwa ni wa kustarehesha mwili, wakiamini kuwa wa kuoa wanaye au walishamchagua tayari, ingawa hutokea mabadiliko, lakini si makubwa. Tatizo hili limekuwa likiwatia simanzi wanawake wengi ambao mwanzo hudhani kuwa wamepata wanaume wa maisha, kumbe wanakuwa ni wale wanaohitaji starehe tu.

Inaumiza pale unapomchagua msichana kwa lengo la kumuoa au mvulana wa kukuoa na kujikuta umekuwa mtu wa kumtosheleza mwili na kuachwa njia panda. Hivyo basi ili watu wasiumizwe na hili wanatakiwa kujua mapema wanaume/wanawake walionao ni wa ndoa au ni wa kustarehesha mwili? Siku zote sifa za mwanaume/mwanamke wa starehe ni tofauti na wa ndoa.

Utofauti huo upo hata katika umuhimu. Hivi kama una mwanaume ambaye ni kwa ajili ya kukukata kiu huku ukitambua kuwa ana mwanamke mwingine utakuwa na wivu naye wa nini wakati unajua fika wewe ni chaguo la pili? Vivyo hivyo kwa mwanaume. Nadhani utakachojali wewe ni kupatikana kwa huduma yako, likiwemo suala la kupelekwa viwanja na kulishwa chipsi kuku.

Lakini linapokuja suala la ndoa wivu ni lazima na yote haya yanatambulika kwa mtu atakayekuwa na uelewa wa mapema kuhusu mpenzi wake. Kuna faida nyingi za kujua hili mapema, moja wapo ni kuandaa ramani ya kukufanya ufikie lengo lako. Ikiwa mwanaume uliye naye ni wa ‘kuchuna’ lazima afuate ramani ya kuchunwa anapokwepa, abanwe. Na kwa mwanamke wa kuoa naye vivyo hivyo.

Unapokuwa na mpenzi, jambo la kwanza la kufahamu ni hilo la kujua nafasi yako ni ipi kwake? Ukishatambua unachotakiwa ni kuandika ramani ya penzi lenu na kuisimamia. Kwa mfano mwanaume uliye naye akiwa ni wa ndoa, kaeni mpange lini mtaoana, malengo yenu ni yepi, mnatakiwa kufanya nini kuelekea huko, kama ni kutambulishana kwa wazazi, lisiwe ni suala la kusubiri liwe ni la lazima kwa sababu ramani inaelekeza hivyo.

Aidha kama mwanaume ni wa kustarehesha, naye awekewe ramani yake, kila wikiendi lazima atoe pesa za kustarehe, awe tayari kwa kuwa pamoja, atoe vocha, alipe kodi ya nyumba na yote yanayohusu jukumu lake asipofanya, anakuwa amepoteza sifa.
Jambo linalosikitisha siku hizi ni kuona watu wanakutana sokoni, shuleni na kupeana mapenzi bila kuwa na ramani ya kufuata aidha kuelekea kwenye ndoa au kustareheshana, matokeo yake ni mivurugano ambayo huwaliza wengi.

“Kaniacha kwenye mataa wakati nilikuwa namtegemea kabisa kuwa atanioa” Mtu anayesema hivi ukimuuliza mliwahi kupanga kuoana? Anabaki kimya, lakini kishachezewa miaka mitano mizima na hakuwahi kugutuka kuwa jamaa hafuati ramani ya ndoa.

Jamani ni vema tukawa wazi kwenye mapenzi na uwazi huo utajulikana kwa ramani. Uliyenaye ili umtambue kuwa ni wa ndoa mpe ramani yake, aende kwenu akajitambulishe, akupeleke kwao, akutunze na kukupa kipaumbele kama mke, ukiona hataki kukufanyia hayo tambua huyo ni wa starehe unachotakiwa ni kumtayarishia ramani yake ya kuchunwa kisawa sawa ili upate faida na usije kujuta atakapokuacha au kumfumania.

Mimi huwa nashangaa kuona baadhi ya wanawake wanakuwa na wivu hadi kwa waume za watu wakati wanatambua kuwa hawawezi kuolewa, na wao ni changuo la pili. Shida yote ya nini ukiwa unataka ukawe mke mwenza, andaa ramani yako na jamaa aifuate usikae ukidhani jambo litatokea kama mvua . Mwisho niwaonye watu wanaoanzisha mapenzi mashuleni hawa lazima wawe na ufahamu kuwa mapenzi ya aina hiyo mengi huwa ni ya kustareheshana tu na mwisho wake huwa ni baada ya kumaliza shule.

Tena ni vigumu kuyawekea ramani mapenzi ya kishule shule kwa vile wote huwa katika safari ya kutafuta maisha ambayo mwisho wake huwa hayajulikani. Ni vema kusoma kwanza kisha baada ya kupata mwanga wa maisha ndipo suala la mapenzi likatazamwa kwa upana, vinginevyo ni kuchezeana na kuharibiana maisha tu.
 
tunaishi mara moja tuu.....jichoree ramani yako mwenyewe, ukisubiri kuchorewa......haitaisha....
 
Ukimuonesha ramani yakustareheshana anaweza akasepa wakat bado unahitaj starehe yake
 
Sitakagi kuweka prediction kwenye mahusiano cause muda wowote anaweza kuchange... Mimi huwa nakuwa neutral tu chochote kikitokea sawa tu
 
Back
Top Bottom