Ni msemo wa kikwetu?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,997
Ninayasifu mahaba, ya wale walopendana,
Mapenzi yasiyo haba, moyoni yamejazana,
Siyo yale ya kuiba,hadharani kupeana,
Penzi ni kupenziana, mpenzie akupenziaye!!*

Ni mguso wa mahaba, mikono mkishikana,
Ni hisia iso tiba, miili ikikutana,
Utavijaza viriba, kwa mapenzi yalo tana,
Nyege ni kunyegezana, mnyegeze akunyegezaye!!

Mkayashiba mahaba, ndimi mnapopeana,
Wakasema huyu baba, na mama wanapendana,
Vijana wakayaiba, siri yao wasichana,
Denda ni kudendeana, mpe denda akudendeaye!!

Si mzigo ni mahaba, nawaambia vijana,
Moyoni mkiyashiba, furaha itajazana,
Ni kama mbingu ya saba, pale mnapopeana,
Cheka ni kuchekeana, mchekee akuchekeaye!!

Haya ninyi mahababa, ninyi mnaopendana,
Iwe ni yenu akiba, kila mnapokutana,
Msipeane khotuba, bali mapenzi mwanana,
Chaku ni kuchakuana, mchakue akuchakuaye!!

Tamaa siyo mahaba, ni mapenzi ya kitwana,
Yasotolewa kwa riba, yatoka kwa Maulana,
Wallahi hayana toba, mapenzi ya kiungwana,
Tomasa ni kutomasana, mtomase akutomasaye!!

Nimeyasifu mahaba, aibu sikuiona,
Yule wangu wa habiba, mgongo ameukuna,
Na sasa nimpe tiba, ya mahaba yalo shana,
Dondo ni kudondoana, mdondoe akudondoaye!!

(*) - Niliandika shairi hili miaka kama mitatu hivi iliyopita baada ya kusoma shairi zuri la majibu la Mzee A. S. Andanenga liitwalo "Nyege ni kunyegezana". Kabla ya majibu yake aliandika shairi ambamo ndani yake alitumia msemo huo wa "nyege ni kunyegezana". Baadhi ya washairi walipomjibu walimtuhumu kutumia matusi kwa mtu mzima kama yeye na ya kuwa kwanini ameamua kutukana katika utunzi wake. Ndipo alipoandika shairi hilo na kuongeza kuwa "nyege ni kunyegezana, ni msemo wa kikwetu".
Ni hapo nilipapata wazo la mimi nami kuchezea maneno! I hope you enjoy.. na kama utakwazika, basi ndiyo hivyo yote hayo ni "msemo wa kikwetu!"
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
 
Last edited by a moderator:
'.......Denda ni kudendeana, mpe denda akudendeaye!!..........'

MWANAKIJIJI NAONA HUJAMBO KWENYE HAYA MAMBO EEH?!basi kama ni mchezaji soka,wewe nakufananisha na NURDIN BAKARI,anayefit kwenye kila namba
 
NURDIN BAKARI,anayefit kwenye kila namba

Huyu ni kilaka mzuri sana.Simba walikosea kumwacha saizi wanamtolea mimacho.
Ana bahati alipo kuwa Simba Maximo hakumwona kabisa kaja Jangwai dah anafunika bovu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom