Penzi bila maumivu

Penzi bila maumivu

SEHEMU YA 35...
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa ukaribu wao. Wasichana wengi walionekana kuumizwa na ukaribu wa Tatiana na Nathan kwa kuwa kila mmoja alitaka kuwa karibu na mvulana huyo aliyekuwa na sura nzuri.
Kwa Maria ndiye aliyeonekana kukasirika zaidi, wivu mkali ukamkamata moyoni mwake, alimpenda mno Nathan na hakutaka mvulana huyo awe na msichana yeyote zaidi yake.

Kitendo cha Tatiana kuanzisha ukaribu na Nathan tayari kwake kukawa na maumivu makali ya moyo kiasi kwamba kila alipokuwa akiwaona, alisikia kitu chenye ncha kali kikiuchoma moyo wake.
Taratibu chuki ikaanza kujengeka dhidi ya Tatiana, hakutaka kumshikia fimbo yake na kumuongoza tena kama ilivyokuwa zamani, alichokifanya ni kumsusa hivyo Nathan kuchukua jukumu hilo ambalo likamfanya kuwa karibu zaidi na msichana huyo.

Siku zikaendelea kukatika, japokuwa kila mmoja alikuwa muimbaji lakini waliikubali sauti ya Tatiana ambayo iliwasisimua wote waliokuwa wakiisikia. Sauti ile ikawavunja moyo na kuona kwamba ilikuwa ni lazima wao kuwa wasindikizaji na msichana huo kuchukua ushindi katika shindano hilo.

“Unajua kuimba,” alisema Nathan.
“Nashukuru! Hata wewe unajua.”
“Najua ila si kama wewe. Unanifurahisha sana, unautetemesha mtima wa moyo wangu kila nikusikiapo,” alisema Nathan huku akimshika mkono Tatiana pale walipokaa, Tatiana akashtuka.
“Nathan! Kuna nini?”
“Sikiliza Tatiana!”
“Kuna nini?”
“Nimeshindwa kuvumilia.”
“Kuvumilia nini?”
“Nataka nikwambie ukweli wa moyo wangu,” alisema Nathan.
“Ukweli upi?”
“Kwamba ninakupenda.”
“Unanipenda?”

“Ndiyo! Ninataka nikuoe kama ikiwezekana,” alisema Nathan, moyo wa Tatiana ukapiga paaaaaaa! “Unataka......”
“Nikuoe! Usiwe na wasiwasi, ninataka niwe nawe, haijalishi tutaishi wapi, ukitaka Tanzania, sawa, Liberia, sawa pia ila ukweli, popote pale lakini mwisho wa siku nataka kuwa na wewe, uwe mama wa watoto wangu,” alisema Nathan, hapohapo Tatiana akaanza kububujikwa na machozi, maneno aliyoongea Nathan, yaliugusa moyo wake.
 
SEHEMU YA 36...
Peter alikuwa na mawazo tele juu ya mpenzi wake ambaye kwa kipindi hicho hakuwepo nchini Tanzania. Kila wakati, alionekana kuwa na mawazo mengi huku wakati mwingine akijilaza kitandani kwa ajili ya kupata usingizi lakini haukuweza kuja kabisa.

Alimpenda mno Tatiana kuliko msichana yeyote yule, alimthamini sana lakini mwisho wa siku aliamua kuondoka nchini Tanzania pasipo kumuaga. Moyoni aliumia lakini hakuwa na jinsi, aliamua kukubaliana na hali iliyojitokeza na hivyo kuaanza kumsubiria.

Aliposikia kwamba kulikuwa na shindano kubwa la muziki lilitaka kuanza nchini Marekani, akili yake ikamwambia kwamba hicho ndicho kilichopelekea msichana wake kuchukuliwa na kupelekwa nchini Marekani.
Alichokifanya, kwa kuwa lilikuwa likitangazwa sana, ndipo alipoamua kuanza kufauatilia kwenye mitandao juu ya washirika ambao wangeshiriki katika kinyang’anyirto hicho.

Zaidi ya watu elfu kumi walikuwa wamejiandikisha ila alichokifanya ni kwenda kwenye sehemu ya watu kutoka barani Afrika, hapo ndipo alipoliona jina la msichana wake, Tatiana.
Akalibonyeza jina hilo, picha ya Tatiana ilitokea. Alichanganyikiwa, uzuri wake ukampagawisha zaidi kiasi cha kuona kama alikuwa akiibiwa mali yake huko nchini Marekani.

Akakosa raha, moyo wake ukapoteza amani, alichokifanya ni kuanza kumuomba Mungu ili kama itawezekana basi aweze kumlinda na kusitokee mtu yeyote yule kulichukua penzi lake
“Natumaini atarudi tu, nitataka nimwambie ukweli kwamba nimeshindwa kuvumilia, hata kama itawezekana, aje kulala nyumbani,” alisema Peter.
 
SEHEMU YA 37...
Nathan akapata wakati mgumu wa kumbembeleza Tatiana na kumfuta machozi yaliyokuwa yakimtoka. Aliguswa na machozi yale, hakutaka kuona msichana huyo akilia huku yeye akiwa moja ya sababu iliyomfanya kuwa hivyo.
Alijaribu kumbembeleza lakini hakuacha kumwambia ukweli juu ya kile kilichokuwa kikiendelea moyoni mwake. Mapenzi ya msichana huyo yakamlevya, hakutaka kusikia kitu chochote kwa wakati huo zaidi ya kuwa na Tatiana tu.
Siku zikaendelea kukatika, wiki zikasonga mbele na hatimaye siku ambayo watu walikuwa wakiisubiria kwa hamu kufikia. Watu elfu kumi waliokuwa

wamejiandikisha nchini Marekani, wakachunjwa mpaka kufika watu elfu moja, kwa maana hiyo, Afrika ilitoa watu elfu moja na Marekani ikatoa idadi hiyo ya watu. “Kesho ndiyo kesho, mpambano unaanza,” alisema mtangazaji mmoja wa Redio ya Number One.
Siku iliyofuata, mpambano mkali wa kuimba ukaanza. Majaji waliandaliwa kwa ajili ya kuanza kazi zao. Kila mmoja alikuwa makini katika uimbaji, watu wengi waliokuwa wakisimama mbele ya jukwaa katika ukumbi waliopangiwa alikuwa makini kuhakikisha kwamba hatoki nje ya biti.

Zaidi ya watu elfu tano walikuwa wakikusanyika ndani ya ukumbi huo, televisheni nyingi za Marekani zilikuwa zikionyesha shindano hilo lililovuta hisia za watu wengi duniani kwa kipindi hicho.
Ka sababu alihitajika mtu mmoja tu, watu wakaanza kuchujwa. Kila mtu aliyeambiwa kwamba asingeweza kuendelea, alikuwa akilia tu huku wale waliofanikiwa kuvuka wakiwa watu wenye furaha kwa kuona kwamba wanakaribia kunyakua kitita kile cha fedha.

“You are the best Tatiana,” (Wewe ni bora Tatiana) alisema jaji mmoja, alikuwa akimwangalia Tatiana aliyesimama jukwaani huku mkononi akiwa na kipaza sauti, alikuwa amekwishamaliza kuimba.
Uwezo wa Tatiana ulikuwa gumzo kwa kila mtu aliyekuwa akilifuatilia shindano hilo, watu wengi walivutika kwa ajili ya kumsikiliza Tatiana aliyeonekana kuwa na kipaji hasa cha kuzaliwa.
Sauti yake ilikuwa na mvuto, watu wengi walikuwa wakikifuatilia kipindi hicho kwa kuwa tu kulikuwa na msichana aliyekuwa na sauti nzuri na kali hata zaidi ya mwanamuziki Celine Dion.
 
SEHEMU YA 38...
Wamarekani wakaanza kumuogopa Tatiana kwa kuwa ndiye aliyeonekana kuwa kizuizi kikubwa katika kuuchukua ushindi huo. Washiriki wao walikuwa wazuri lakini kila wapokuwa wakimsikiliza Tatiana, msichana huyo alionekana kuwa moto wa kuotea mbali.
Hawakujua ni kitu gani walichotakiwa kufanya ili heshima ibaki nchini kwao. Hawakutaka kutulia, baadhi yao, kitu walichoona kufaa kufanywa ni kucheza na majaji wale tu.

“Jamani huu si mchezo wa chumbani, kumbeba mtu yeyote yule litakuwa kosa kubwa kwa kuwa shindano linaonekana dunia nzima,” alisema jaji mmoja.
“Sasa unataka ushindi uende kwa mtu ambaye si Mmarekani?”
“Tunaangalia uwezo wa mtu tu, vinginevyo, heshima ya shindano hili litashuka,” alijibu jaji huyo.
Stori za kutaka kupewa ushindi Wamarekani zikaanza kuvuma, zilisikika kila kona na mwisho wa siku kumfikia bwana Warren aliyeonekana kupandwa na jazba.
Alichokuwa akikiangalia kwa wakati huo ni fedha tu, kitendo cha kusema fulani alikuwa mshindi na wakati watu wote waliona kilichokuwa kikiendelea ilikuwa ni sawa na kulishusha thamani shinano hilo.
Alichokifanya ni kuwaita majaji na kuongea nao. Japokuwa aliwaonya sana lakini bado tetesi zikaanza kusikika kwamba lile suala la kuibeba nchi ya Marekani lilikuwa palepale hivyo kuamua kuwaondoa majaji hao na kuwaleta wengine.

Alichokuwa akikihitaji ni heshima ya shindano tu, alikwishajua kwamba endapo wangepata mshindi aliyeonekana kutokufaa basi sifa ya shindano hilo ingeshuka hivyo hata wadhamini kulipuuzia, kabla ya kitu hicho kutokea, akaamua kuwawahi kwa kuwaondoa majaji hao.

Kati ya watu elfu kumi waliokuwa wakishindana katika kinyang’anyiro hicho, ni watu mia tano tu ndiyo waliokuwa wamebaki. Mpaka kufika hapo, tayari idadi kubwa ya washiriki walikuwa wamekwishaondoka nyumbani kwao hivyo wale waliobakia wakachukuliwa na kupelekwa Las Vegas kulishuhudia jiji hilo.
 
SEHEMU YA 39...
Si Tatiana wala Nathan, wote wawili walikuwa wamebakindani ya kinyang’anyiro hicho, uwezo wao katika uimbaji ulikuwa mkubwa kiasi kwamba kila mtu alikuwa akiwahofia. Ukaribu wao haukupungua, kila siku bado waliendelea kuwa pamoja huku msichana Maria ambaye naye alinusurika kutolewa zaidi ya mara tatu akiendelea kuumia moyoni mwake kiasi kwamba uwepo wake ndani ya nchi hiyo uligeuka na kuwa maumivu makubwa.

Washiriki wakapangiwa hoteli nzima ya nyota tano jijini humo, watu wawili walilala katika chumba kimoja kwa staili ya ‘double’. Japokuwa bwana Warren alitumia fedha nyingi lakini aliingiza kiasi kikubwa cha fedha kiasi cha kufanya utajiri wake kuongezeka.

Huku akiwa chumbani kwake, mara Tatiana akaanza kusikia simu ikiita. Hakuweza kuinuka kwenda kuipokea zaidi ya msichana aliyekuwa naye chumbani humo, Angelia ambaye alikuwa Mmarekani kwenda kuipokea na kuanza kuzungumza na mtu wa upande wa pili.
“Naweza kuzungumza na Tatiana?” ilisikika sauti kutoka mapokezini.
“Bila shaka. Wewe nani?”
“Ni dada wa mapokezi hapa. Kuna mgeni wake,” alisikika dada huyo wa mapokezi.
“Mgeni gani?”
“Smith Warren,” alisikika.
Hapohapo Angelina akamfuata Tatiana na kumuinua kitandani kisha kumuongoza mpaka katika simu ile kwa lengo la kuzungumza na msichana wa mapokezi. Kitu kikubwa alichokisema ni kwamba kulikuwa na mtu ambaye alikuwa akihitaji kumuona kwa wakati huo, mtu huyo aliitwa Smith.

Hilo halikuwa tatizo, alimfahamu Smith kama mtoto mkubwa wa bwana Warren. Mara ya kwanza kumuona kijana huyo ilikuwa nchini Tanzania kipindi walichokuja kwa ajili ya kumfuata, hivyo kwake hakuwa na wasiwasi hata kidogo.
Angelina akamuongoza mpaka mapokezini, hapo, Smith alikuwa akimsubiria kitini. Alipomuona tu msichana huyo, akasimama, uso wake ukaachia tabasamu pana na kuanza kuwasogelea.

“Tatiana, habari yako!” alisema Smith huku akiwa ameachia tabasamu pana.
“Salama tu, u mzima Smith?”
“Nipo poa. Tunaweza kutafuta sehemu tukakaa na kuzungumza?” aliuliza Smith.
“Kuna nini? Kuna tatizo limetokea nyumbani?”
 
SEHEMU YA 40...
“Wewe twende, utajua hukohuko, ila usihofu, ni jambo la kawaida tu,” alisema Smith hivyo kuanza kumuongoza msichana huyo huku akimwambia Angelina arudi tu chumbani kuendelea na mambo yake.

Smith akamchukua Angelina na kwenda naye katika mghahawa mdogo uliokuwepo hotelini hapo. Wakiwa hapo, akaagizia kahawa na Tatiana akiagizia maziwa na kuanza kunywa. Muda wote huo Smith alibaki akimwangalia msichana huyo kwa umakini sana.
“Smith...!”
“Tatiana....!”
“Kuna tatizo?”
“Hapana, hakuna tatizo.”
“Sasa kuna nini?” aliuliza Tatiana.
“Usiwe na pesha, kunywa kwanza, kuna mengi ya kuzungumza nawe,” alisema Smith.
“Mmmh!”
“Ndiyo hivyo!”
****

Kwa jina aliitwa Smith Warren, alikuwa mtoto wa kwanza wa bilionea Warren ambaye kwa kipindi hicho alikuwa tajiri wa ishirini duniani. Smith alikuwa kijana mpole, mtaratibu sana aliyesoma kwa kiwango kikubwa.
Akiwa na umri wa miaka ishirini na tatu, tayari alikuwa na digrii mbili za biashara kutoka katika Chuo cha Mississippi cha nchini Marekani kitu kilichomfanya kuziendesha baadhi ya biashara za baba yake pasipo tatizo lolote lile.

Wanawake walimpenda Smith kwa kuwa alikuwa mtoto wa bilionea hivyo waliamini kama wagekuwa naye basi maisha yao yangekuwa mazuri. Smith hakuwa na habari na msichana yeyote yule, kitu pekee alichokuwa akikifikiria kwa wakati huo ni kusoma zaidi na kufanya mambo mengine hasa kusimamia biashara za baba yake.

Siku ziliendelea kukatika mpaka siku ile alipoambiwa na wazazi wake kwamba walitakiwa kwenda nchini Tanzania kwa lengo la kutembelea mbuga za wanyama na kupanda Mlima Kilimanjaro.
Kwake ilikuwa ni furaha tele, hakuwahi kufika nchini Tanzania hivyo kufika huko kungemaamaanisha kwamba angekuwa na furaha zaidi kwa kubadilisha hali ya mazingira, hasa hali ya hewa,

Walipofika huko, wakafanya kila kitu na hata wazo la kuliboresha shindano la American Pop Idol lilipotolewa, kwake aliliona wazo zuri kufanyika. Walifanya kila kitu kilichotakiwa kufanywa, siku ambayo waliambiwa kwamba kulikuwa na msichana aliyekuwa akiimba sana, akajikuta akiwa na kiu ya kutaka kumuona msichana huyo.
 
Mkuu Shunie endelea kuliamsha dude!
 
Daah hii hadithi ni nzuri sana,wenye machozi yakaribu hapa tutakoma
 
Daah hii hadithi ni nzuri sana,wenye machozi yakaribu hapa lazima
 
SEHEMU YA 41...
Wakaelekea Shinyanga mpaka katika Kijiji cha Chibe, alipomuona msichana huyo, uzuri wake na sauti yake, akajikuta akianza kumpenda kwa mapenzi ya dhati.
Uzuri wa Tatiana ukamchanganya mno, hakuamini kama angeweza kukutana na msichana mrembo kama alivyokuwa Tatiana tena akiwa ndani ya nchi masikini kama Tanzania.

Alibaki akimwangalia Tatiana ambaye alikuwa kipofu, moyo wake ukazama katika penzi la dhati hali ambayo hakuwahi kuihisi tangu azaliwe. Alijitahidi kuvumilia lakini kamwe hakuacha kuuthaminisha uzuri wa Tatiana.
Siku hiyo waliporudi hotelini, mawazo yae yalikuwa juu ya msichana huyo aliyeonekana kuwa na uzuri wa ajabu. Kadiri siku zilivyozidi kwenda mbele na ndicyo ambavyo alizidi kumpenda msichana huyo kwa mapenzi ya dhati kutoka moyoni mwake.

“I really love her from the bottom of my heart,” (Ninampenda sana kutoka katika mtima wa moyo wangu) alisema Smith huku akionekana kulewa kwa penzi juu ya msichana huyo kipofu.
Siku zikakatika mpaka ile siku ambayo waliamua kurudi nchini Marekani. Katika kipindi chote hicho alikuwa akimfuatilia msichana huyo ambaye aliendelea kuuteka moyo wake vilivyo.
Walipofika Marekani, alipewa kazi kubwa ya kufuatilia biashara mbalimbali za baba yake nchini Urusi na China. Kila kitu alichokuwa akikifanya kwa wakati huo alikifanya harakaharaka ili amalize na kurudi nchini Marekani kumuona Tatiana ana kwa ana.

Akiwa nchini Urusi, alilifuatilia shindano la American & African Pop Idol katika televisheni, uwezo wa Tatiana ulimshangaza, alifahamu kwamba alijua kuimba lakini katika shindano hilo alionekana kuwa moto wa kuotea mbali.
Kila siku alikuwa akiwaita marafiki zake aliokuwa nao nchini Urusi na kuwaambia waangalie kile kilichokuwa kikiendelea, aliwaamia kwamba alimfahamu sana Tatiana na walimtoa barani Afrika tena ndanindani kabisa kitu walichokikataa marafiki hao kwa kuamini kwamba msichana huyo alitoka Afrika Kusini.
Alihakikisha anafanya vitu vyote mpaka alipomaliza na ndipo alipoamua kurudi nchini Marekani ambapo akapata nafasi ya kuendelea kulifuatilia shindano hilo kwa ukaribu zaidi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom