Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,054
- 463,869
- Thread starter
- #121
SEHEMU 51...
“ Mungu, naomba umpe ushindi Tatiana, Mungu, nakuomba sana ufanye hilo,” alisema Nathan huku akiona washiriki watano wa mwisho wakiwa wamekaa tayari mbele ya ukumbi tayari kwa matokeo kutangazwa. Mapigo yake ya moyo yakaanza kumdunda.
*****
Tatiana hakuamini kile alichokuwa amekisikia kwamba alikuwa ametangazwa na kuwa mshindi wa shindano hilo lililodumu kwa miezi sita. Alisikia vizuri kwamba akitajwa jina lake lakini hakuamini kama alisikia vizuri au alikuwa amesikia jina jingine lililofanana na lake.
Kilichomshtua na kuamini kwamba alikuwa ametajwa yeye ni kelele za watu waliokuwa ukumbini pale ambao walikuwa wakilitaja jina lake kwa shangwe kubwa. Hapo ndipo akaamini kwamba yeye ndiye aliyeibuka mshindi katika shindano lile.
Furaha iliyoje! Alishindwa kuamini, hakuendelea kusimama, akajikuta akichuchumaa chini na kuanza kulia kama mtoto. Kile kiasi cha dola milioni tano ambazo zilikuwa ni zaidi ya bilioni kumi zilikuwa zake.
Majaji wote wakasimama na kuanza kumfuata Tatiana aliyekuwa amezungukwa na washiriki wengine na kisha kumkumbatia kwa fuaraha, walikuwa wakimfariji, aache kulia kwani ule ulikuwa ni ushindi wake, alikuwa amejipatia kiasi kikubwa cha fedha ndani ya siku 180 tu.
Kila mtu aliyekuwa akifuatilia shindano lile alishangilia kwa kuona kweli haki ilitendeka, yule mtu aliyekuwa amestahili kuchukua ushindi ule, aliuchukua kitu kilichompa sifa sana bwana Warren kwa kuonekana kwamba hauwa na shindano lililokuwa na upendeleo.
Hapohapo vyombo vya ahabari vikaanza kutangaza juu ya ushindi ule, kila sehemu, picha za Tatiana akilia jukwaani zilikuwa zikionekana, kwa kipindi cha dakika kadhaa tu, tayari akawa maarufu mkubwa duniani.
“Tattie, don’t cry baby, I told you you are the best ever,” (Tattie, usilie kipenzi, nilikwambia wewe ni bora haijawahi kutokea) alisema Smith huku akimkumbatia Tatiana.
Watu kutoka ukumbini pale tayari walikwishajazana jukwaani na kila mmoja kutaka kumshika Tatiana ambaye kwa kipindi hicho alikuwa msichana mwenye uwezo mkubwa kifedha japokuwa hakuwa bilionea kama wengine.