Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,054
- 463,971
- Thread starter
- #101
SEHEMU YA 42...
Ili kuonyesha ni jinsi gani alikuwa amedata kwa penzi la msichana huyo, kila siku alikuwa akielekea sehemu ya mazoezi, alipofika huko, alikuwa kimya pembeni akiwaangalia wanamuziki hao waliokuwa wakifanya mazoezi kwa nguvu zote.
Ukaribu wa Tatiana na Nathan ukamtia mashaka, ukamfanya kuanza kuona wivu kupita kawaida, kila alipokuwa akiwaangalia, ukaribu ule ukaanza kumuumiza mno. Hakujua kama watu hao walikuwa wapenzi au marafiki kama walivyokuwa wengine, alichokifanya ni kuanza kufuatilia.
Kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kumfuatilia Nathan. Akagundua kwamba mvulana huyo alikuwa ametoka nchini Liberia katika Jiji la Monrovia hivyo hakuwa na haki ya kuwa na msichana huyo kwani yeye ndiye alikuwa mtu wa kwanza kumuona nchini Tanzania.
Hakutaka kuendelea kuumia zaidi, alichokifanya ni kuanza mishemishe za kuonana na Tatiana. Siku ambayo walichukuliwa na kupelekwa katika Jimbo la Nevada ndani ya Jiji la Las vegas, hapo ndipo alipoamua kumfuata hotelini ili japo apate nafasi ya kumwambia kile kilichokuwa kikiendelea moyoni mwake.
Alipokwenda hotelini na kuitiwa msichana huyo, mapigo yake ya moyo yakaanza kumdunda mno, akahisi akizidi kumpenda msichana huyo zaidi ya kipindi kilichopita. Kila alipokuwa akimwangalia, uso wake ulijawa na tabasamu pana kiasi kwamba akajiona kushindwa kuvumilia kwa mapenzi yake.
“Niambie kuna nini,” alisema Tatiana huku akinywa maziwa aliyoletewa.
“Tatiana...”
“Abeeee.”
“Kuna kitu ninataka kukwambia, nimeshindwa kuvumilia, naomba nijiweke wazi kwamba nina....” alisema Smith na kukaa kimya.
“Una nini?”
“Ninakupenda mno, ninataka uwe mke wangu wa ndoa,” alisema Smith.
Moyo wa Tatiana ukashtuka, hakutegemea kusikia kile alichokuwa amekisikia mahali hapo, alihisi kama masikio yake yalizembea kusikiliza kile alichokizungumza Smith mbele yake, akauliza tena na tena lakini jibu la Smith lilikuwa lilelile kwamba alikuwa akimpenda kwa mapenzi ya dhati.
“Smith....”