SEHEMU YA 149
“Ich liebe immer noch Partner , deine Liebe zu mir tut.“(Bado ninakupenda mpenzi, penzi lako kwangu halitokufa)
“Sind Sie sicher?“ (Una uhakika?)
“Warum liebst du sie?” (Ndiyo! Kwani huyo malaya umempendea nini?)
“Nur seine Popularität,“ (Umaarufu wake tu.)
“Verließ ihn , Popularität nicht etwas haben, gerade jetzt, dass ich ufuike schnell , nicht möglich ist, treffen Sie angekommen?“
(Achana naye, umaarufu hauna kitu sasa hivi, naomba ufuike haraka, si inawezekana kuonana ukifika?)
“Vollständig , dies sehr seltsam.“(Sijajua kabisa, huyu malaya kaniganda sana.)
“Struggling Partner! Aber ich werde es nicht mehr reagiert Tonhöhe sein, werden Sie im Hotel ein beliebter präsentieren.“ (Jitahidi mpenzi! Hata mimi nitakuwa uwanjani hapo kukupokea, nitakuwepo katika hoteli mtakayokuwepo kipenzi.)
Buffet alikuwa bize akichati simuni, muda wote aliokuwa akichati, uso wake ulijawa na tabasamu pana, alifurahia kile alichokuwa akiandikiwa, moyo wake ukajisikia amani kubwa.
Pembeni yake alikuwepo mpenzi wake, Tatiana aliyeonekana kuchoka mno, alipokuwa amelala, akachukua nafasi hiyo kuchati na msichana wake aliyekuwa nchini Ujerumani, msichana ambaye alimpenda kwa moyo wa dhati kuliko alivyompenda Tatiana.
Msichana huyu aliitywa Nikola, alikuwa Mjerumani halisi ambaye alikuwa mtoto pekee wa tajiri mkubwa nchini Ujerumani, bwana Kurt. Wawili hawa walionana zamani mno, walipendana kwa kuwa walisoma shule moja na mpaka Buffet alipokuwa akifika nchini Ujerumani, mtu wake wa kwanza kuonana naye alikuwa msichana Nikola.
Mapenzi yao hayakufa, waligombana mara kwa mara na kurudiana, waliishi pamoja na baadae kugombana tena, ndivyo walivyoishi na hata katika kipindi ambachjo msichana Nikola aliposikia kwamba Buffet kapata msichana aitwaye Tatiana, moyo wake ulimuuma mno.
Hakuwa na cha kufanya, kila alipokuwa akiona picha walizopiga Tatiana na Buffet, moyo wake ulimuuma mno ila hakuwa na cha kufanya, akabaki na maumivu makali ya moyo.
Siku ziliendelea kukatika, alipoanza kusikia kwamba mwanamuziki huyo alikuwa njiani kufanya shoo nchini Ujerumani, kitu cha kwanza kabisa akaanza kuwasiliana na Buffet kwa lengo la kurudiana tena kama uilivyokuwa kawaida yao.