t blj
JF-Expert Member
- Dec 2, 2011
- 6,396
- 14,823
Inawezekana ila ni ngumu mie ilikuwa ninakunywa wastani wa soda 6 kwa siku,Mara ya kwanza nilipojaribu nile chakula bila kunywa soda niliona maisha magumu sana, chakula hakishuki, sina hamu ya maji wala juisi ya matumda wala chochote kile, yaani natamani soda tu, hapa ndipo nilipogundua kumbe hii ni shida, ni kama madawa ya kulevya, nina mashaka kuna kitu wanaweka mule, hii si kawaida.
Mwezi uliopita nikasema hata ikibidi nife kwa kukosa soda, so be it, ila sinywi hata iweje, ni wiki ya 5 leo sijanywa soda, napitia wakati mgumu sana, ila namshukuru Mungu, naendelea vizuri.
Asubuhi kabisa moja , baada ya chai asu supu moja , katikati ya mchana na asubuhi moja. Chakula cha mchana lazima kiambatane na coke baridi , Jioni moja na wakati wa chakula cha usiku lazima ipatikane coke baridi pia
Ilitokea siku moja , nikawa nakunywa soda ila sipati ladha yoyote nikaamua kuacha
miaka 2 sasa ila cha ajabu ile hamu ya coke baridi hasaa baada ya supu ya asubuhi imerudi tena at rime nakunywa moja moja japo siruhusu initawale tena.