Baada ya sakata la viongozi wa dini na tuhumu za madawa ya kulevya kusimama kwa muda sasa limerejea tena baada ya Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo kueleza jana masikitiko yake ya kutaka kunyamazishwa kwa kuhusishwa na sakata hilo kama njia ya kumnyamaziaha.
KUJIKANGANYA KWA SERIKALI
1. Wakati wa baraza la Idd, Rais Kikwete alisema kauli yake ilieleweka vibaya, akasema taarifa alizopewa ni za mchungaji mmoja wa Kanisa la Biafra Kinondoni na Shehe mmoja, na hakumaanisha viongozi wote.
2. Waziri Mkuu Pinda wakati akijibu swali la Susan Lyimo (MB.) alisema Rais alieleweka vibaya kwani waliokamatwa, kwa kauli yake ni "wachungaji waswahili wa vikanisa vidogo" na wala si maaskofu kama ilivyochukuliwa na vyombo vya habari.
Wakati propaganda hii ikizidi kushika kasi, mtu yeyote makini lazima azingatie yafuatayo.
Kwanza, kwa mfumo wa Kanisa Katoliki, haliitaji kusubili intelijensia ya wabongo iwaambie kiongozi fulani amekengeuka.Kanisa lina intelijensia yake ambayo hata CIA pamoja na nguvu zote wanalitambua hilo.Kiongozi yeyote hata awe Papa akikengeuka kwa issue nyeti kama hii anathibitiwa mara moja,Kwa wale wanaomjua Askofu Koda wa Same waulize leo hii yuko wapi'
Pili, kwa mfumo wa kanisa Pengo kama kiongozi hata nguo zake hajui bei yake. Matunzo yake yote yanafanya na kanisa hadi anakufa, yeye kama yeye haruhusiwi kumiliki hata hela bali alichonacho chote ni mali ya kanisa na hakuna anachokosa.
Tatu, kanisa aligawi vyeo kwa kujuana wala promotion, ni integrity yake, kwa hiyo hadi Pengo anachaguliwa kuongoza kanisa la Tanzania, integrity yake ni beyond any reasonable doubt. Hata akikengeuka upo mfumo wa kudeal naye hata before intelijensia ya bingo kubaini.
Kwa ufupi, Kanisa Katoliki limekuwepo takriban miaka 2000 na litaendelea kuwepo kwa sababu ya misingi yake kiimani na mfumo wake wa kumdhibiti yeyote. Ni mwendawazimu tu atakayedhani serikali hii ya awamu ya nne itapambana nalo kwa kuzusha tuhuma za kitoto ili kuwanyamazisha viongozi wake. Kwa ushauri tu, serikali zote (na vyama vyao) zilizojidai kupambana na kanisa zimefall apart (revise your history), fanyeni tu wanayowakemea for your political survival.