Pengo: Nchi imeoza!

Watu wakiacha hoja wakaanza kuleta chuki zao za kidini na ubinafsi ni uchovu wa akili na uzembe wa kuwaza .
 
Hamukujibu hoja yangu.

Nimesema wapi ndani ya vitabu vyake 73 ameamrishwa kukemea maovu na munakimbilia logic, common sense, haki kama Raia. Nimedai reference ya kitabu nikiamini kwamba anaongozwa na Kitabu chake kwa kuwa yeye amezungumza kama kiongozi wa dini.

Kukwepa hoja yangu nadhani ni ushahidi kwamba hakuna linalomwarisha akemee uovu, kama lingekuwepo lingeletwa.

Kama majibu na misimamo ya viongozi wa dini yanatokana na common sense sasa muongozo wa vitabu una faida gani?

Kesho akija mwingine na common sense ikimwambia jibu ni kupindua Serikali kwa mtutu wa bunduki itakuwaje?
 

Mkuu kama kweli Kanisa lingekuwa linaongoza serikali, tusingekuwa na serikali ya namna tuliyonayo sasa, na watanzania wangekuwa much better than they are now. Like wise kama nchi hiiingeongozwa na msikiti isingekuwa na hali hii tuliyonayo sasa. Sijui kama kuna mahali popote pale kwenye msahafu wanapounga mkono watu dhulumat, mafisadi au wababaishaji madarakani. Sidhani kama biblia inaunga mkono watu wa namna hiyo.

Hali ya Rwanda ni tofauti sana na hali ya Tanzania. Wauaji wa Rwanda kwenye genocide hawakuwa waislamu, wala waliouliwa hawakuwa waislamu. Mauaji ya Rwanda yalikuwa ni ujinga mwingine tu wa binadamu. Somalia kwenye waislamu karibu kote sio wakristo wanaowaua wenzao au sio wakrito wanaouawa.

Ni huu huu ufisadi, upindishaji wa sheria, kuwafanya watu wajinga ndio kulianzisha yaliyotokea kwenye nchi hizo mbili. Hayo mengine yote ni catalyst tu, hakuna lolote.

Tusiingie kwenye mtego wa mafisadi kutumia dini na kuwagawa watanzania kama njia ya kuwaokoa. Au tusiingie kwenye mkenge wa watu wanaosema kuwa Waraka utatugawa, ni ujinga tu. waraka haumgawi mtu. Waraka unamtaka kila mtanzania achague kiongozi anayefaa, kama unaona mwislamu anafaa, si fisadi, hapindishi sheria ana lengo la kuwaendeleza watanzania basi achaguliwe tu. Kama mkirsto ni mwizi, fisadi na mjinga mwenye akili fupi na asiyeweza kuongoza hatufai.
 
Sina haja wala nguvu za kupambana na kanisa. Kwa sababu naamini kuwa kanisa lilikuwepo, lipo na litaendelea kuwepo. Hivyo kupambana na kanisa ni kuongeza matatizo. Ninachojitahidi kufanya kutafuta balance pale ambapo kanisa litaweza kuishi na jamii nyingine (wapagani, waislam, wahindu, materialist, wakomunist na serikali) kwa amani.

Sina mkononi hii kanuni bado na ndio maana nimeuleta huu mjadala hadharani, nikijua kwamba penye wengi ni rahisi kupata ufumbuzi.

Kuhusu masali yako mawili ningependa kuyajibu kama ifuatavyo:

1) a)Utata wa waraka unakuja pale ambapo, ili upate maudhui yake ni lazima uhudhurie kanisani
b) kuna watu hawana imani na katoliki, hivyo ni vigumu kuuamini waraka huo, wakifikiri kwamba hii ni danganya toto.
c) Italeta mvutano na waumini wengine, kitu ambacho mmeshakiona kimeanza kutokea kwa waislam kutoa wakwao baada ya kuuona ule wa katoliki. Hii si dalili nzuri
d) Serikali inahisi kuingiliwa katika kazi zake.

2) Issue ni ya Katoliki na Serikali. Pengo akiwa ni kiongozi wa katoliki ndiye mwenye kubeba mzigo wa katoliki, na kwa upande mwingine Kikwete naye ni kiongozi mkuu wa Serikali ndie mwenye kubeba mzigo wa Serikali.

Waraka umeandikwa kwa baraka zote za Katoliki (Pengo). Ni vigumu kumueleza mtanzania yeyote kuwa Pengo yuko nje ya barua hiyo. Na mpaka leo tamko la Pengo juu ya barua hiyo huwa na uzito mkubwa kuliko kiongozi/mtu yeyote yule.

JK, Kama utamaduni wa CCM ulivyo ndiye mtarajiwa kugombea nafasi hiyo ya uchaguzi mwaka 2010 kwa tiketi ya CCM. Hivyo barua hiyo inamhusu yeye moja kwa moja na sijui kama analala usingizi. Fikiria kama wewe ndiye ungekuwa mgombea!
 

Huu waraka sio mara ya kwanza kutolewa, ule wa mwanzo haukuleta matatizo kama inavyosemekana yatakuja kusababishwa nao. Zawadi kama ungetaka kubalance story ungezungumzia hatari ya MWONGOZO wa waislamu hata kama umekuja baada ya waraka wa wakatoliki. MWONGOZO huo umeji-isolate zaidi kwamba wafuasi wake watapiga "kura maslahi." Sasa linganisha na waraka ambao unataka watu wachague viongozi waadilifu! Usipobalance story hata kama una pointi nzuri namna gani huna tofauti na wale ambao unawalaumu kimakosa kwenye thread hii huku na wewe unayafanya yaleyale, kwa maana hiyo unajihukumu mwenyewe!
 
Na Mkapa je??
 
Jamani natafuta Mwongozo wa Shura ya maimamu kuhusu uchaguzi. Haujaingia tu jamvini? Nisaidieni jamani.
 
hata kama waraka wao ungekuwa mzuri kiasi gani nitaupinga mbaka kufa,wao ni watu wa dini hivyo wanatakiwa kuwaandaa watu kiroho,wawaelimishe waumini wao namna ya kuishi ili wafike mbinguni na si vinginevyo ndio maana hata yesu alikataa kushugulikia mambo ya duniani hata kama utawala wa kiyahudi ulikuwa mbovu ingawa watu walijua yeye ndiye mfalme lakini yeye alisema hana shida ya ufalme wa duniani yeye ni mfalme wa mbinguni,sasa nyie mnaohangaika na mambo ya dunia ndo biblia ya wazungu ilivyowaagiza hivyo?
 
 
Na Mkapa je??


Umesingizia maudhui yake kupatikaa kanisani lakini kuna wengi wameununua na unaendelea kununuliwa nao wanatakiwa kuingia kanisani kama kivutio ?

Kanisa katoliki litafute waumini kwa kuvutia na waraka ? Nadhani sasa una matatizo makubwa kuwazoa haya .
 

Asante kwa kuwa mkweli.

Nilijaribu kujenga hoja kama hii na kuomba ushahidi ndani ya Biblia kama dini ya Kikristo ina support waliyoyasema nikajibiwa eti mambo yanakwenda kwa common sense wakati kauli imetolewa na chombo cha dini.

Ila naomba nikukumbusha jambo moja.Katika dini ya Kiislamu kuna muongozo si tu wa kiroho bali hata wa kidunia na waislamu wameamrishwa kukemea na kupiga vita maovu mbalimbali hapahapa duniani pamoja na uovu wa ufisadi. Kwa hiyo ukisikia waislamu wanapiga vita ufisadi kumbuka kwamba hawa wameamrishwa kufanya hivyo ndani ya vitabu vyao.

Tena, asante kwa kuwa mkweli na muwazi.
 
Tatizo ni chanzo. Kama Kanisa katoliki lingesikia ombi la Serikali na kufuta waraka huo, hayo ya waislam yasingetokea.

Na ingekuwa rahisi sana kwa serikali kupiga marufuku kwa taasisi yeyote ile kuleta waraka kama huo.

Baada ya Pengo kukataa kuufuta waraka huo, Serikali ilishindwa kusema lolote juu ya ule wa kiislam.
 


Kuwazuia wanawake kuendesha gari na kuwa na nafasi kubwa including Elimu bora pia miongozi ya Uislam mmeamrishwa kufanya ?Kuvaa mabomu na kuua watu ambao hawataki sharia kwa kusema unapigania dini ya Mungu kumbe yote haya mmeamriwa ?Sikuyajua haya asante
 

Bring your evidence kama haya yameamrishwa na Uislamu na tathmini yako kwa nini 1.5 billion Muslims duniani hawatekelezi 'maamrisho' unayodai wamepewa. Ukilata ushahidi tutajadili your evidence.

Mdau kasema neno la Mungu halibadilishwi na namuunga mkono. Je, na haya mabadiliko yalioandikwa na Terry Watkins sio Juma Salumu sio pia ushahidi wa changes? Mdau kasema wazi neno la Mungu halibadilishwi na mtu yoyote alite objective anakubali kwamba maneno ya kweli ya Mungu hayachezewi na hayachezeleki. Mbona hapa yanarekebishwa na kubadilishwa kila kukicha?
http://www.av1611.org/biblecom.html
 
Last edited:


Njia nzuri ya kuweza kuupamba uongo ni kusema 'wataalamu wa mambo ya siasa wanasema...' Kuandika nyaraka katika Kanisa Katoliki ni kitu cha kawaida sana kwani ni namna mojawapo ya kuwasilisha ujumbe kwa waamini wake au watu wengine wanaokubaliana na ujumbe huo.

Kanisa Katoliki linaamini hakuna imani kama hakuna 'responsible social action' (faith has to be inscribed in responsible social action) - ndiyo maana Kanisa linajishughulisha na yote yanayopiga vita ujinga, umaskini na maradhi na kushirki katika yote yanayoleta maendeleo ya watu na nchi. Katika kufanya hivyo, Kanisa linahubiri habari njema kwa watu.

Baada ya waraka wa Wakatoliki kuandikwa, watu wenye nia mbaya wameweza kupotosha maudhui yake makusudi lakini mtu mweye akili hawezi kupotoka anaona ukweli uko wapi. Binafsi sioni cha ajabu hapo. Ila naona huruma kwamba Watanzania wanalishwa siasa chafu na wanakubali wenyewe kuibugia.

Kati yetu kuna wanaotetea uovu unaolinyonya taifa letu kwa kulinda maslahi yao. Baadhi ya wazushi wanatoa tafsiri kwamba Kanisa Katoliki linataka litawale kila nchi. Hata kwenye waraka, walichosoma wazushi ni waraka/Kanisa Katoliki kuwagawa Watanzania kwa misingi ya dini.

Yaani, walichokisoma ndani ya waraka ni hicho tu! Tunaona pia katika maeneo mengine wazushi wapo: Mfano, matatizo ya mgodi wa North Mara waathirika wanaambiwa ndio walioharibu miundo mbinu ya maji yenye kemikali na pia walishalipwa hela zao zote ili wahame eneo hilo; wanaharakati wanapotetea wananchi wanaonyanyasika Loliondo, wanaambiwa na wazushi waache "ubazazi"; Hakielimu ilipotoa changamoto kwa Serikali ili iboreshe elimu miaka ya nyuma, wazushi walisema kama wanataka Hakielimu iwe chama cha siasa, wajiandikishe kama chama na siyo NGO...

Mbona Watanzania tunapenda kufanya 'intellectual masturbation'?
 


1) a)Utata wa waraka unakuja pale ambapo, ili upate maudhui yake ni lazima uhudhurie kanisani

Ngoda si lazima uudhulie kanisani, mie sijaenda kanisani lakini naona ule waraka ni changamoto nzuri sana kwa serikali. Hata kama ni Waislam wangeandika waraka kama ule ingekuwa ni changamoto nzuri kwa serikali. Taking National Interest first. Understand that Tanzanian Catholic teachings and Islamic teachings are all for the betterment of the national wellbeing. Hao nao ni Watanzania.
b) kuna watu hawana imani na katoliki, hivyo ni vigumu kuuamini waraka huo, wakifikiri kwamba hii ni danganya toto.

Inatagemea sana na wewe unapoichulia imani yako. Kama wewe unaona kuwa imani ndiyo inatawala maisha yako hata kuthubutu kuona imani za watu wengine ni kama adui then, basi wewe huna upendo na dunia. Imani isiwe kuleta chuki. Nimeona waislamu wengi tu ambao huudhuria kanisani; wala hamna matatizo yoyote.
c) Italeta mvutano na waumini wengine, kitu ambacho mmeshakiona kimeanza kutokea kwa waislam kutoa wakwao baada ya kuuona ule wa katoliki. Hii si dalili nzuri
Sawasawa; wewe ukiona kama Catholic na Pengo ni rivals then this will haunt you. If you think in a broad way it will not; kumbuka kuwa Pengo na wewe wote ni same cultural heritage, hizi dini zimekuja tu, hata asili yetu siyo hiyo. So you’re more near to Pengo than to his Catholicism or your Islamism.
d) Serikali inahisi kuingiliwa katika kazi zake.
The Government should do their job; they have to do the right thing! They have already failed everybody, the country has already taken by the dogs; what then do you expect? Don’t you see that it was best for all people from all walks of life stand up and guide their people against this government? I think the Muslims and the catholic join hand and make it harder for this government. In this way they will listen as they will know their days were numbered.
2) Issue ni ya Katoliki na Serikali. Pengo akiwa ni kiongozi wa katoliki ndiye mwenye kubeba mzigo wa katoliki, na kwa upande mwingine Kikwete naye ni kiongozi mkuu wa Serikali ndie mwenye kubeba mzigo wa Serikali.
That is an exaggeration of high spin! Haijafikia hapo kabisa. Mie naona Taasisi nyingine zingesimama na kuanza vile vile ku-mobilize watu wake. Ngoda this is a failed state. Mtu anaenda BOT anachukua Pesa. Hakuna Rule of Law, then what do you expect?? Watu waungwana kama Pengo vilevile na Mashehe wangesimama na kusema ukweli. Wanaona watu wao wanavyoteseka. What is wrong for them mobilizing their people in a peaceful way??
Waraka umeandikwa kwa baraka zote za Katoliki (Pengo). Ni vigumu kumueleza mtanzania yeyote kuwa Pengo yuko nje ya barua hiyo. Na mpaka leo tamko la Pengo juu ya barua hiyo huwa na uzito mkubwa kuliko kiongozi/mtu yeyote yule.

JK, Kama utamaduni wa CCM ulivyo ndiye mtarajiwa kugombea nafasi hiyo ya uchaguzi mwaka 2010 kwa tiketi ya CCM. Hivyo barua hiyo inamhusu yeye moja kwa moja na sijui kama analala usingizi. Fikiria kama wewe ndiye ungekuwa mgombea!

Ngoda serikali zima,pamoja na wawakilishi (Wabunge) wote wameoza. Waraka hausemi ni Rais tu, hata Wabunge, acha hiyo rage and ranting yako!!
 
Wandugu nilikwesheni kuwaambieni hapo awali kuwa hila za kutaka kuisilimisha Tanzania hazikuanza leo.

Mwinyi akiwa Rais, alitaka kuibadilisha Tz iwe "The United Islamic Republic of Tanzania" kwa bahati nzuri wasomi wakamuumbua.

Alivyo chizi zaidi anataka kutekeleza azma yake kabla hajafa,kupitia Kikwete muislamu mwenzake.

Wakristu, najua si wote mnaoweza kupata taarifa nyeti kama hizi, lakini iweni makini sana na viongozi wetu hasa wa imani ya dini ya kiislamu.
 



Magobe wachape shule hawa walalamishi na wazushi . Eti kanisa limenyimwa nafasi serikalini . Ipi na kupendelewa ili iweje ? Kanisa linafanay mambo yake si kama hawa jamaa leo eti wanaenda kuomba serikali iwasaidie kujenga umoja mna kumpata kadhi.Serikali yetu haina dini na haina specific faith ial watu wanao jenga serikali wana imani zao.Chikawe anaweza kweli kuwasaidia nyie walalamishi ?

Eti anataka ushahidi wa waislam n ukatili wao kwa wanawake kwa jina la kurani wewe . Hata kua kesi huko Iraq na Sudan na malaysia wanapiga sharia ama uko shimo gani wewe ?
 
mwinyi a.k.a mzee ruksa
najua una watu wako hapa ujumbe ndio huo
kwa akili yako ulidhani hatuwezijua mkakati wako mchafu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…