Mkuu wangu kama kweli ungekuwa huna udini usingeandika hivi hata iwe kwa kutolea mfano tu, kwa kufanya hivi unachochea moto zaidi badala ya wewe pia kujadili mada yenyewe..Sijawa huko na sitaruhusu kujirahisisha kujadili udini, hapa nilikuwa najaribu tu kumwambia tunaja mengi na historia kuliko wanavyofahamu ila hatuko tayari kwani tukifanya hivyo wenye moyo mchache wa kujadili ukweli watakimbilia majambia.
Ndio maana nasisitiza tujadili hoja iliyoletwa hapa na kama hoja ya dini aanzishe anayetaka thread yake na kama mod ataruhusu ndipo tuijadili. Kwa hapa tunajadili Cardinal pengo anapoonya maovu na udhaifu wa serikali kwa manufaa ya watanzania wote.
Tunaoonja makali ya maisha ni sote, na tukiendekeza ushabiki kwa misingi ambayo wengine wanaendekeza hapa tutaishia umaskini wa kutupwa na kuona tatizo ni yule unayemwona mbele yako badala ya kuelewa ukweli wa nini viongozi wetu wafunguke mioyo na akili zao kuona, kusikia na kufanya tunayowaambia, maana kujitetea kwa viongozi na kutafuta visingizio vya hapa na pale si hoja ya kuondoa matatizo yaliyopo.
Shukran sana tena hapa ndio mfano wako unaleta maana kabisa.. Kama Pinda au Mkapa angekuwa ktk sherehe ya kiislaam kisha akawaambia Masheikh waache kujihusisha na biashara za madawa ya kulevya.. mkuu wangu, Usingesikia Muislaam hata mmoja akipiga kelele kwa sababu sisi waislaam hatuna daraja la ubora wa mtu (binadamu) mbele ya Mungu isipokuwa mitume. Sheikh na mimi hatuna tofauti yoyote ya kimatendo isipokuwa tofauti ni kwamba yeye kasoma dini na kakabidhiwa mamlaka ya kuongoza zaidi ya hapo kila mmoja anabeba msalaba wake..
Na ndio maana mimi naweza kabisa kuandika hapa kwamba Sheikh Mkuu Simba ni fisadi na fisadi kweli kwa sababu najuua fika anauza mali za waislaam kwa kupitia bakwata. bakwata ni kundi la Mafisadi kitu ambacho wewe ktk Ukristu huwezi kusema hivyo kumshutumu Pengo. Na ndio maana kesi zozote zinazohusiana na kanisa huwa hazifiki mahakamani kwa sababu kanisa linachukua dhamana ya makosa ya watu hao..
Umeniuliza kazi ya Pengo, yeye ni kiongozi wa dini tena basi ni balozi wa Vatican... kazi yake ni dini na amepewa Immunity kwa sababu ya kazi yake. Alichotakiwa kufanya angemfuata JK na kuomba majina ya wauza unga kutoka kanisa lake ama angetazama list ya watuhumiwa walioko mahakamani tayari na kufuatilia kesi zao kuhakikisha kwamba kanisa lake halihusiki kabisa na vitendo hivyo. Lakini badala ya yeye kuchukua njia na taratibu zinazotakiwa karukia kwenda jukwaani na kudai yeye Pengo sijui apewe majina ya wauza Unga na rais wetu wa jamhuri ya Muungano, ILI IWEJE..Unaleta kusutana na rais wetu ati awataje wauza unga wakati hujawahi kumfuata ukaomba majina kama utaratibu wa kawaida tu..Haya nambie Pengo akipewa hayo majina ya wauza unga unategemea atayafanyia nini - Kuyaombea au?
Hili ndilo swali langu ambalo pia ktk maandamano ya Washington nimeuliza wanaandamana Marekani ili IWEJE... Tunachotafuta hapa sio ubishi na kunyoosheana vidole bali ni kupata suluhisho la matatizo sugu tuiliyokuwa nayo..Unga ni moja ya mchango mkubwa wa fedha za madafu nchini. Leo hii maisha yamepanda sana Tanzania kwa sababu ya mchango mkubwa wa unga na money laundry ndio maana nyumba za Kariakoo zimefika hadi billioni moja na baadhi ya watu wanalipa cash.. Haitokea watu kujiuliza hii purchasing power inatoka wapi ktk nchi maskini ambayo haina umeme, maji, usafiri na hata ku abuse maliasili na rasilimali zake..
Sasa kama mnataka tuhalalishe biahssra za Unga na Bangi semeni na itakuwa jambo bora zaidi iwe kama Afghanstan kila mtu atajirike kwa biashara haramu kuliko kupiga marufuku biashara za madawa ya kulevya kumbe viongozi wa dini zetu ndio wako mstari wa mbele kabisa kuziendesha na sisi wananchi tunawawekea kifua..I would careless kujua kama viongozi hao ni waislaam au wakristu kwa sababu tamaa ya kufanya biashara haramu haitokani na dini ya mtu..
Shukran sana tena hapa ndio mfano wako unaleta maana kabisa.. Kama Pinda au Mkapa angekuwa ktk sherehe ya kiislaam kisha akawaambia Masheikh waache kujihusisha na biashara za madawa ya kulevya.. mkuu wangu, Usingesikia Muislaam hata mmoja akipiga kelele kwa sababu sisi waislaam hatuna daraja la ubora wa mtu (binadamu) mbele ya Mungu isipokuwa mitume. Sheikh na mimi hatuna tofauti yoyote ya kimatendo isipokuwa tofauti ni kwamba yeye kasoma dini na kakabidhiwa mamlaka ya kuongoza zaidi ya hapo kila mmoja anabeba msalaba wake..
Na ndio maana mimi naweza kabisa kuandika hapa kwamba Sheikh Mkuu Simba ni fisadi na fisadi kweli kwa sababu najuua fika anauza mali za waislaam kwa kupitia bakwata. bakwata ni kundi la Mafisadi kitu ambacho wewe ktk Ukristu huwezi kusema hivyo kumshutumu Pengo. Na ndio maana kesi zozote zinazohusiana na kanisa huwa hazifiki mahakamani kwa sababu kanisa linachukua dhamana ya makosa ya watu hao..
Umeniuliza kazi ya Pengo, yeye ni kiongozi wa dini tena basi ni balozi wa Vatican... kazi yake ni dini na amepewa Immunity kwa sababu ya kazi yake. Alichotakiwa kufanya angemfuata JK na kuomba majina ya wauza unga kutoka kanisa lake ama angetazama list ya watuhumiwa walioko mahakamani tayari na kufuatilia kesi zao kuhakikisha kwamba kanisa lake halihusiki kabisa na vitendo hivyo. Lakini badala ya yeye kuchukua njia na taratibu zinazotakiwa karukia kwenda jukwaani na kudai yeye Pengo sijui apewe majina ya wauza Unga na rais wetu wa jamhuri ya Muungano, ILI IWEJE..Unaleta kusutana na rais wetu ati awataje wauza unga wakati hujawahi kumfuata ukaomba majina kama utaratibu wa kawaida tu..Haya nambie Pengo akipewa hayo majina ya wauza unga unategemea atayafanyia nini - Kuyaombea au?
Hili ndilo swali langu ambalo pia ktk maandamano ya Washington nimeuliza wanaandamana Marekani ili IWEJE... Tunachotafuta hapa sio ubishi na kunyoosheana vidole bali ni kupata suluhisho la matatizo sugu tuiliyokuwa nayo..Unga ni moja ya mchango mkubwa wa fedha za madafu nchini. Leo hii maisha yamepanda sana Tanzania kwa sababu ya mchango mkubwa wa unga na money laundry ndio maana nyumba za Kariakoo zimefika hadi billioni moja na baadhi ya watu wanalipa cash.. Haitokea watu kujiuliza hii purchasing power inatoka wapi ktk nchi maskini ambayo haina umeme, maji, usafiri na hata ku abuse maliasili na rasilimali zake..
Sasa kama mnataka tuhalalishe biahssra za Unga na Bangi semeni na itakuwa jambo bora zaidi iwe kama Afghanstan kila mtu atajirike kwa biashara haramu kuliko kupiga marufuku biashara za madawa ya kulevya kumbe viongozi wa dini zetu ndio wako mstari wa mbele kabisa kuziendesha na sisi wananchi tunawawekea kifua..I would careless kujua kama viongozi hao ni waislaam au wakristu kwa sababu tamaa ya kufanya biashara haramu haitokani na dini ya mtu..
<br />
<br />
Kaka fungua google search....type (the secret terrorists) ikifunguka download web namba mbili yenye PDF by Bill Hughes
Mkuu wangu Uislaam hauna Tanzania wala nje sisi wote tunasali sawa dunia nzima na tunafuata kitabu dunia nzima tofauti zetu zipo ktk baadhi ya mila na tamaduni za makabila na watawala ktk madhehebu ya Shia lakini sio kwetu Sunni. hakuna mtu mbora mbele ya mwenyezi Mungu isipokuwa yule mwenye kufanya Ibada hivyo kwetu waislaam kila mmoja wetu ana equal opportunity ya kuwa mtukufu mbele ya bwana kutokana na matendo yake.. Mimi naweza kuwa mbora mbele ya Mungu kuliko Mufti Sheikh Mkuu.. Hii haina maelezo zaidi na kama umeona tofauti basi ni sawa na kumuona Mkristu anakunywa pombe ukasema ndio Ukristu huo..Mkuu ningependa kujua kama ume reside tanzania au nje ya nchi!! kwa sababu kwa hali halisi iliyopo Tanzania sidhani kama maneno " sisi waislaam hatuna daraja la ubora wa mtu mbele ya Mungu isipokuwa mitume. " yana apply. Kama kauli za maaskofu za kutaka serikali kutenda haki , kupambana na ufisadi nk zinatafsiriwa vibaya na mshehe kwamba maaskofu wanasema hivyo kwa sababu rais ni mwislam ,unategemea kauli kama aliyoitoa kikwete ingeamsha nini kama ingetolewa na kiongozi wa kikristo mbele ya mhadhara wa waislam?
Mkuu hapa hali ni tete na sielewi ni kwanini viongozi wa serikali na wa dini hawataki ku address hii issue..!
Mkuu ni sawa unaweza kubandika hapa kama sheikh mkuu Simba ni visadi...hii inatokana na kwamba una proof za huo ufisadi..mathalan ameuza viwanja vya waislam..! Na mimi naweza kumshutumu Pengo kama kuna proof za ufisadi wake. Kwanini unasema kesi zote zinazohusiana na kanisa hazifiki mahakamani? Kuna kesi moja ya padre kumlawiti kijana mmoja aliyekuwa mfanyakazi wake wa ndani kama sikosei...hiyo kesi ipo mahakamani! Hiyo kitu ya kanisa kuchukua dhamana ya makosa yao sijaielewa ,ina bidi labda unitolee mfano!
Sioni ni kwanini Pengo alitakiwa amfuate JK kutafuta majina ya wachungaji wanaofanya biashara ya madawa ya kulevya. Kikwete mwenyewe siyo kazi yake kusema kile alichokisema. Hiyo ni kazi ya mkuu wa kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya..Mr Godfrey Nzowa...! Nzowa angetoa taarifa kwenye vyombo vya habari kama kawaida..watu x na y wamekamatwa kwa kujihusisha na _ _ ! kwa hiyo tunarudi kule kule ..kikwete hakutakiwa atoe ile kauli pale ndiyo maana inaonekana kama uchokozi!
Hujaniambia kama Pengo ana wajibu au la wa kukemea ,kuomba watuhumiwa wa ufisadi/madawa ya kulevya watajwe , washtakiwe ili haki itendeke!
mkuu kwa mtazamo wangu nimeona hii issue kila pande unaichukulia kivyake..tunaweza tukabishana sana hapa....! kwa upande wangu mimi kama mkatoliki naona kidogo nimekuwa offended na kauli ya kikwete!
kweli mkuu hapa tunaweza kulumbana mpaka asubuhi...! Nilichosema mimi ...hiyo ni kazi ya mkuu wa kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya. Yaani kilichotakiwa kufanyika ni kama kawaida..wakikamatwa watu iwe airport au majumbani mwao huwa zinatolewa taarifa kwa vyombo vya habari. kuna wakati mwingine huwa hawatoi habari mpaka wawakamate wahusika wote ....! hiyo ni kazi ya Nzowa! Kama kikwete asingetoa kauli yake kulikuwa hakuna sababu ya Pengo kutaka awataje majina...!. Instigator wa malumbano haya yote ni Kikwete.Mkuu wangu Uislaam hauna Tanzania wala nje sisi wote tunasali sawa dunia nzima na tunafuata kitabu dunia nzima tofauti zetu zipo ktk baadhi ya mila na tamaduni za makabila na watawala ktk madhehebu ya Shia lakini sio kwetu Sunni. hakuna mtu mbora mbele ya mwenyezi Mungu isipokuwa yule mwenye kufanya Ibada hivyo kwetu waislaam kila mmoja wetu ana equal opportunity ya kuwa mtukufu mbele ya bwana kutokana na matendo yake.. Mimi naweza kuwa mbora mbele ya Mungu kuliko Mufti Sheikh Mkuu.. Hii haina maelezo zaidi na kama umeona tofauti basi ni sawa na kumuona Mkristu anakunywa pombe ukasema ndio Ukristu huo..
Pili, Namshutumu Sheikh Mkuuu kwa Ufisadi sio nina Ushahidi hapana sina ushahidi lakini kesi zake ni sawa na za Mkapa kuuza nyumba za serikali.. sina ushahidi zaidi ya kuona kwa macho au Mkataba wa Barricks/Richmond na kadhalika. Binafsi sina ushahidi isipokuwa naamini vitu hivi vimetokea kulinagana na ushahidi ulotolewa. Na hakika sidhani kama Pengo au Simba wakifanya biashara ya Unga, wewe na mimi tunaweza kukusanya ushahidi dhidi yao..
Tatu, umesema huoni sababu ya Pengo kwenda kuchukua majina ya wauza unga..Sasa kama haikuwa na haja huyo Pengo kataka JK awataje ili iweje?.Nijibu hapo tu tumalize mjadala na malumbano..
Na kama kazi hii sio ya rais imekuwaje Pengo asiende kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya kupata majibu yake..Na kwa nini unafikiri ..Mr Godfrey Nzowa alitakiwa kutangaza majina ya wahusika.WHY?.. unafikiri ingekuwa bora zaidi viongozi hao kuanikwa ktk vyombo habari kukamatwa kwao kuliko kuwakanya waumini wote wasijihusishe na biashara hizo baada ya kuonekana baadhi wameisha kamatwa..
Lengo la JK ni kuwaonya wale ambao hawajakamatwa au hawajajihusisha wasifanye vitendo hivyo.. Ushahidi tayari umesha jitokeza kwa kukamatwa kwa baadhi ya viongozi wa dini kwa hivyo humshutumu mtu ktk mkutano huo laa ila unawaonya wengine wasifanye vitendo vile vya kiovu baada ya baadhi yao kukamatwa. Hii haifanyi kanisa zima kuhusika..
|
ATAKA AWE NA UJASIRI WA MWANAMKE MJAMZITO na Datus Boniface |
Bado unashindwa kuelewa.. List ya wauza Unga alopewa JK na marehemu Amina Chifupa sio swala tunalozungumzia hapa wala sio ombi la Pengo kutaka majina hayo...kweli mkuu hapa tunaweza kulumbana mpaka asubuhi...! Nilichosema mimi ...hiyo ni kazi ya mkuu wa kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya. Yaani kilichotakiwa kufanyika ni kama kawaida..wakikamatwa watu iwe airport au majumbani mwao huwa zinatolewa taarifa kwa vyombo vya habari. kuna wakati mwingine huwa hawatoi habari mpaka wawakamate wahusika wote ....! hiyo ni kazi ya Nzowa! Kama kikwete asingetoa kauli yake kulikuwa hakuna sababu ya Pengo kutaka awataje majina...!. Instigator wa malumbano haya yote ni Kikwete.
Sidhani kwenye utawala wa sheria kuna haja ya kutoa onyo! kama wahalifu/mafisadi wanakamatwa na kushtakiwa nadhani hilo ni onyo tosha kabisa lenye kufanya kazi kuliko maneno matupu!
Mkuu, kikatiba Kikwete ana madaraka makubwa sana ..probably kwa tanzania baada ya Mungu anafuata Kikwete kwa kuwa na nguvu.
Hayo majina ya mafisadi serikalini/ndani ya chama chake, wauaza madawa nk anayo mda mrefu tu lakini amekuwa mtu wa kutoa maonyo na kutabasamu tu badala ya kushinikiza wakamatwe, washtakiwe ..ili .haki itendeke!
Thread hapo chini nadhani umeiona!
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/257-majina-ya-wauza-madawa-ya-kulevya-jk-anayo.html
Kwanini Pengo ilimuuma ile kauli ya Kikwete? au ni mmoja wa washukiwa.
lakini siku hizo hana uzito wowote kulinganisha na Wakati za Nyerere.
Pengo amnyoshee kidole Mkapa kwanza; then sisi wengine tutamchukulia serious.
Kwani Mkapa alisema anawajua ukitaka hivyo mbona series itakuwa ndefu, unaanza na anayewajua then watatajana kama na Mkapa atakuwemo sawa.Pengo amnyoshee kidole Mkapa kwanza; then sisi wengine tutamchukulia serious.
Kwa hiyo unataka kusema Pengo mdini? Anamuandama Kikwete kwa sababu Kikwete muislam na hajamuandama Mkapa kwa sababu Mkapa Mkatoliki?
Au una maana gani?
Maana watu wawili wakifanya vibaya sina haki ya kumyooshea kidole mmoja? Mpaka niwanyooshee wote wawili? Nitanyooshea wangapi? Na nikinyooshea wawili napo kweli hutaniambia kwamba hutanichukulia serious mpaka ninyooshee watatu, ad infinitum ?
Jana ulisema unamfahamu sana Muadhama Policarp Cardinal Pengo, sidhani. Kwa kumbukumbu zangu huyu ni mkimya sana, mtaratibu sana, hana makuu kabisa. Lakini ni mkweli, mpenda watu, mpenda maendeleo na mtetezi mkubwa wa wanyonge.
Nilimwona kwa mara ya kwanza Mwadhama Pengo mwanzoni mwa miaka ya 80 akiwa padre akitokea Rome masomoni huko Sumbawanga katika kijiji cha Ntuchi wilayani Namanyere akielekea Kate, akitembezwa na mzee wake Marehemu Askofu Carolo Msakila. Kwa vile nilimwona mara ya kwanza hakuonyesha upekee na nilishangaa kama ametoka Rome masomoni.
Punde nikaambiwa kapangiwa kazi ya kuanzisha Seminari kuu ya Segerea hapa Dar es Salaam. Baada ya miaka michache Pope akamteua kuwa Askofu wa Kwanza wa jimbo jipya katoliki la Tunduru-Masasi. Baada ya miaka michache tu Pope akamteua kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Dar es Salaam lilikokuwa likiongozwa na hayati Muadhama Laureano Cardinal Rugambwa.
Kwa mtazamo finyu ingeweza tafsiriwa kwamba kateremshwa cheo kutoka askofu mwenye jimbo na kuja dar kuwa askofu msaidizi. Lakini ilikuwa demotion for promotion, na maana yake Pope kumwandaa kwa kazi nzito aliyo nayo sasa.
Mwadhama Policarp, hakurupuki katika kuongelea kitu, si mwoga, ni mkweli, mtetezi mwenye unyofu wa moyo. Wengi hapa tunaongelea kwa mitazamo tofauti lakini si kile kilichoko ndani ya moyo wake. Tukumbuke hawa ni manabii kama akina Eliya walipowatahadharisha watawala wakakaidi na madhara yaliyotokea kwa wanahistoria ya taifa la Israel tunayajua.
Tuweke kando itikadi za kisiasa na tuangalie anachoongelea Muadhama. Kuna mengi kama hayo ambayo wengi wetu tunajua lakini hakuna hatua zinazochukuliwa zaidi ya kulalamika majukwaani kama hawana mamlaka za kutolea uvivu.
Hao wavuja pesa yanayoendelea ni kitendawili tega. Hii ya funika kombe mwanaharamu apite inazidi kutupeleka pabaya. Kiongozi asipokuwa tayari kukosolewa maana yake yupo huru kujifanyia atakavyo na kujikuta yuko juu ya sheria.
Hakuna chombo cha kumwajibisha. Na dhana ya mapokea kwa viongozi wetu hata wanapopotoka kuendelea kuwaimbia nyimbo za kuwasifu imetufikisha hapa, na wanufaika na mwenendo huu mbovu ndio watetezi wa wakuu na wanyonge kuendelea kunyongeka.
Tunapaswa kumpongeza Muadhama Policarp kwa ujasiri wa kuonya, kukemea na kushauri bila woga, maana viongozi waandamizi wa serikali hawaku tayari kufanya hivyo kwa sababu ya kutetea maslahi yao na nafasi zao katika uongozi.
Yana mwisho na ukingo unakaribia zinakoishia mbio hizi.
Kiranja,
Kardilnali Pengo anacheza karata moja mbaya sana ambayo inaweza kutafsriwa kama Udini kutokana na dhana yake kwa nini JK amesema viongozi wa dini waache kujishughulisha na biashara za Unga. Na yawezekana kweli JK hakupaswa kulitumia jukwaa lile kulingana na taratibu za Kikristu lakini alipaswa kusamehewa kwa sababu hajui tofauti na Mwinyi alokwenda ktk jukwaa la Kiiislaam siku ya maulidi na kuanza kuzungumzia ngono na matumizi ya Condom. Akatokea kijana na kumpa kofi la Kerbu mzee Ruksa! yamekwisha siku hiyo hiyo. Kisha tuliokuwa tumetulia kidogo na hizi habari za Masheikh na Mapadre ktk siasa za Bongo, mara Pengo analiibua jambo ambalo limepita toka Easter..
Tatizo ambalo linanikera mimi ni pale Kardinali Pengo anapotumia majukwaa ya dini akiwa makanisani au sikukuu za Kikristu kumzungumzia utawala wa JK jambo ambalo halijawahi kutokea nchini kwa kanisa kujiingiza ktk siasa kiasi hiki..Kama ni umaskini na Ufisadi ulikuwepo toka enzi za mwinyi, na Mkapa lakini inaonyesha wakati huu kanisa limechukua muda mwingi kujihusisha na siasa bila sababu za Kiimani..JK ambaye anakemea swala la kiimani watu kujihusisha na Unga anaonekana sii kiongozi mzuri kwa sababu tu hakuwataja na limewagusa viongozi wa kanisa na sio Biblia wala mafundisho ya YESU na mitume..
Yeye Kardinali anajua fika wapo viongozi wa dini wanaojihusisha na biashara hizi na kama hajui angejaribu kufanya uchunguzi hata kidogo kabla hajachukua maelezo ya JK kama ni kashfa ya kanisa lake.
Yeye Kardinali anajua fika acha unga wapo viongozi wa dini wanaotumia msamaha wa kodi kwa kuingiza mali za watu na kukatiwa kitu pembeni kinyume kabisa cha sheria kwa sababu lazima wanaweka hesabu ya matumizi ya hizo misamaha ilotumika. Kupitisha mali kwa kutumia kanisa/Bakwata ndio mission town vijana wa mjini wanapatia panga lao..
Watu mjini wanacheza na makanisa kupata visa za nchi za kigeni ambazo hazipatikani kirahisi ili kwenda fanya biashara na kadhalika.. Haya yote ni matatizo yatokanayo na Umaskini kanisa linawasaidiwa watu kiasi kwamba linakiuka hadi kanuni na taratibu zake.. na kama navyosema siku zote pale penye Mapungufu basi Rushwa hupenyeza!..Hii haina cha kanisa wala msikiti binadamu wote tumeumbwa na tamaa na sii vizuri kumwekea dhamana binadamu mwenzako kwa sababu hujui yaliyomo rohoni mwake. Wale waliokamatwa ni viongozi wa dini na mfano tosha kabisa kutuelewesha kwamba wapo Unga umeingia hadi sehemu za ibada.
Umenichekesha sina mbavu duuuh! ama kweli wewe Mzanaki!NA INGELIKUWA MMENICHAGUA MIMI NDO RAIS...HAKI YA MAMA YANGU MZANAKI...UNAOKOTWA UNA MSUMARI WA INCH SITA UTOSINI..POTELEA KWA MBALI ILI NCHI ITAWALIKE BILA USWAHILI.