Pendo bandia! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pendo bandia!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by kilimasera, Feb 25, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Niambie, Pendo Bandia,
  Wapi Linapoanzia,
  Moyoni au Kichwani?
  Huzaliwa Jinsi Gani?
  Hulelewa Jinsi Gani?
  Nijibu Hima Nijibu!
  Nalisubiri Jawabu,
  Macho Ndivyo Hulizala
  Na Chakula ni Kulola
  Na Hufia Pendo Hilo
  Pa Pale Penye Malalo
  Sote Tupige Malalo
  Kwa Kifo Cha Pendo Lile
  Ninaanza, Ngoo Ngooo
  Ngooo, Ngooo, Ngooo!

  KIBWAGIZO
  Nahitaji Mwanamke Halisi!
  Ni Mwanamke Makini
  Sitaki Mwanamke Feki
  Nahitaji Mwanamke mimi
  Atumie Muda kunifahamu mimi
  Sihitaji Mwanamke wa Mahotelini
  Ndiyo tiba ya kunipenda mimi.

  MAWAZO YA PENDO LILE!
  Ulizaliwa Peke Yako,
  Kutoka kwa mama yako,
  Ni wazi uko peke yako,
  Unapaswa kuangalia yako,
  Namna gani utaishi kivyako,
  Hata kama uko Peke yako
  Yote yanawezekana

  Iwaze amani
  tafakari furaha ni nini?​
   
 2. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  Pendo bandia huanzishwa kichwani na katu haliko moyoni!
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,640
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  shairi lako zuri sana mheshimiwa ..ningekujibu lakini thijui nianzie wapi!!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...