MAMA POROJO
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 4,974
- 793
Wapendwa wa Chadema,
Mimi naomba Dr Slaa awanie ubunge Arumeru kusudi arudi Bungeni kuweka nguvu mpya
Damu mpya kama huyu....Keshachoka kisiasa huyu..
Kwa sasa tunahitaji dam mpya za zenye nguvu bungeni na kwenye ulingo wa siasa!
Hawa hapa...Mnahitaji nyie akina nani? wavua gamba bila shaka mmechoka na ndio maana hapa tunazungumzia mambo ya chadema lakini vidudu watu hamchoki kujiingiza kwenye mambo yasiyowahusu.
Damu mpya kama huyu....
Mnahitaji nyie akina nani? wavua gamba bila shaka mmechoka na ndio maana hapa tunazungumzia mambo ya chadema lakini vidudu watu hamchoki kujiingiza kwenye mambo yasiyowahusu.
Hii sredi wapi imeandikwa ni ya wanamagwanda?mtoa mada ameweka wazi kuwa hii ni kwa wanachadema tu, inanipa wasiwasi kuwa unaweza kuhudhuria kitchen party wakati ni kwa viburudisho tu
Keshachoka kisiasa huyu..
Kwa sasa tunahitaji dam mpya za zenye nguvu bungeni na kwenye ulingo wa siasa!
Mkuu hata posho wabunge wametemeshwa!!!!!Achilia mbali hilo, hata Ikulu pia anaipika, kasi, uwajibikaji. Bila yeye unadhani CCM wangevuana magamba, wangeridhia kuandika katiba mpya? wangekubali mabadiliko ya sheria mbovu ya kuandika katiba mpya.
Mi naona mleta mada labda angeshauri Mkapa arudi Ikulu 2015 kupitia CCM B.
alishinda urais sembuse ubungeee, najua hata wewe una uhakika atashinda, najua hamuombolezi kumtakia Sumari maisha mema, mnaomboleza kupoteza jimbo, nikupe matokeo?
Wapendwa wa Chadema,
Mimi naomba Dr Slaa awanie ubunge Arumeru kusudi arudi Bungeni kuweka nguvu mpya
Unaelewa maana ya kuchoka kisiasa? Unaelewa maana ya kuishiwa sera?unamaana gani kuchoka kisiasa?
Nikuwekee picha za wabunge wa ccm waliochoka bongo zao kazi kulalalala.
Keshachoka kisiasa huyu..
Kwa sasa tunahitaji dam mpya za zenye nguvu bungeni na kwenye ulingo wa siasa!
Kumbe nakuumiza kichwa eeh!! Powle sana...Huwa najiuliza sana kama medula oblangata yako ni ya kibinadamu ama la, huwa sipati jibu.
CCM mngetuonyesha njia mbona kwenu kuna vibabu hata meno havina bado vipo kwenye safu yenu???au ndo kamati ya ufundi??Keshachoka kisiasa huyu..
Kwa sasa tunahitaji dam mpya za zenye nguvu bungeni na kwenye ulingo wa siasa!
Una uhakika gani kama Slaa akigombea lazima atashinda?, manake umeandika as if akigombea lazima ashinde
Wakuu mleta hoja si mtu mwema kwa Chadema ana nia ya kuidhoofisha Chadema, hivi unadhani Meru kuna mchanganyiko wa makabila kiasi gani hata wamchague mtu ambaye siyo wa kabila lao? Unafikiri leo Mzee Mwinyi au Mkapa pamoja na kuwahi kuwa rais wakigombea pale Meru watachaguliwa? Na pia watanzania tumechoka na watu ambao hawana makazi ya kudumu katika maeneo wanayogombea na je wanaishi katika hilo? Mtoa hoja nia yako si nzuri, hivyo kajipange upya.