KIM KARDASH
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 5,139
- 1,149
- Thread starter
-
- #181
Joshua anafaa na anaweza sana , tusitumie bomu kuua sisimizi jamani. ile ni nafasi ya kijana Nassary na tayari ameshajijenga sana kisiasa Meru
tatizo langu kama umenifuatilia mimi huwa sijali kama namfurahisha ama namuudhi mtu bali hupenda kusema kile ambacho kipo ila watu wengi hawapendi kukisikia,mimi huwa nasema tu ili wasikie kwa nguvu!Umetoa wazo watu wote wamelipinga unakomaa nalo tuuuu! we vipi umetumwa? ushindwe.
Joshua Nasari ni kijana machachari anayekubalika pia
Kabla ya kuleta upupu hapa kashauri kwanza ccm wenzako namna ya kujivua gamba
kwanini hamsemi nimepewa na slaa?mkuu hiyo ni kazi maalum aliyopewa na magamba
Kwa hadhi ya dkt.SLAA kusimama na MAGAMBA kwenye kinyang'anyiro cha ubunge ni kumdhalilisha kisiasa. Pia MAGAMBA wako tayari kuhamishia jeshi,vifaru mizinga, usalama wa taifa maguruneti, silaha zote za kivita vigagura na wachawi wao kwenye jimbo husika kuhakikisha dkt SLAA anashindwa.
akisemea bungeni kama mbunge ndio inanoga na kuinyima usingizi serikali,bila kuwa mbunge wapinzani wake watasema mwacheni aseme yuko katika jitihada za kufanya propaganda kukijenga chama chake,leo hii akiongea sam ruhuza mwenye cheo sawa na dr slaa(wote ni makatibu wakuu tu wa vyama vyao)neno lake linaweza kuwa na uzito kama akiongea kafulila ambae ni mheshimiwa mbunge?kim, unatumia nguvu nyingi sana ktk hoja zako! Hivi hujui kwamba tatizo la nchi hii ni system nzima ya uongozi? Hivi wewe unaamini dr akirudi mjengoni ndio tanzania itageuka kuwa paradise?. Binafsi sijaona fursa ambayo dr kaipoteza kwa kutokuwa mbunge kama ni nyaraka za serikali amezidaka anaweza kufanya kama alivyofanya wakati alipoitoa kwa umma ile list of shame. Na je hakuna mbunge wa cdm unayemuamini kwamba akitumwa na dr kitu fulani akakiseme /kukifanya bungeni atakifanya? Na je dr hawezi akaitisha press conference na waandishi wa habari na akanena lake jambo? Na je unaimani/evidence kwa kiasi gani kwamba hitaji la wana arumeru ni dr kuwa mbunge wao? Nina wasiwasi na uelewa wako kuhusu watu na demokrasia na muktadha wa siasa kwa ujumla.
Una uhakika mwanzisha mada ni mchaga?...na je ni mwanachama wa CDM?...nyie wachaga mna tabu sana.tamaa ya utajiri itawaua.hapo mnaitumia siasa kama kivuli tu hamna lolote wabaguzi wakubwa nyie.yaani mnafikiria uchaguzi mtu hajazikwa?kweli hiki ni chama maslahi
Mkuu mimi naamini matendo yetu hapa duniani ndio yatafanya tupumzike kwa amani huko tuendako na si kwa maombi ya wanadamu,kwa hiyo hata mzee sumary matendo yake ndio hukumu yake,na si kwake ni kwa wanadamu wote
Ati shetani akizeeka anakuwa malaika mwema ni kweli?
Naam! Upendo wa shetani ni kuhakikisha unaishia pale alipo yeye - Jehanamu. Ushauri kutoka kwa mafisadi na magamba ni wa kuepukwa kama ukoma.
Akili yako haina akili!tatizo langu kama umenifuatilia mimi huwa sijali kama namfurahisha ama namuudhi mtu bali hupenda kusema kile ambacho kipo ila watu wengi hawapendi kukisikia,mimi huwa nasema tu ili wasikie kwa nguvu!
Huenda unapiga kura USA au Uingereza lakini si Tanzania. Unachosema ni kuwa watu washinde kwa kura nyingi ili wasiibiwe. je, mgombea wa upinzani akishinda kwa kura 1000 ni halali tu aibiwe? Je hujaona sehemu ambako watu wamebeba mapanga na Marungu ndipo mpinzani anatangazwa mshindi? Labda unaandika ukiwa kwingine si hapa Africa na hasa Afrika mashariki.Nimekua kimya nikijaribu kufuatilia hoja zenu waungwana,mnaodai ukatibu mkuu wa slaa ni mkubwa kuliko ubunge,hoja yenu dhaifu sana,umaarufu wa slaa hautokani na ukatibu mkuu wake bali ulitokana na ubunge sasa kwa nini asirudi bungeni akamalizie kazi aliyoianzisha?au mnataka asubiri nafasi ya ubunge wa kuteuliwa na rais mwaka 2013 mwishoni kufuatia muafaka wa haya mazungumzo ya upenuni kati ya jk na mbowe?kama hamjui ndio tunakoelekea!
Na nyie mnaodai eti slaa ni rais mnamdanganya pamoja na kujidanganya nyie!na pia mnaosema eti sijui ataibiwa kura na kufirisika kisiasa pia ni uongo!hivi kura huwa zinaibiwaje?ndugu zanguni amkeni msikubali kudanganywa na wanasiasa,tatizo wanasiasa wetu wa africa huwa hawasemi ukweli kwa kuogopa kuwajibika kutokana na kushindwa chaguzi ndio huwa wanakuja na kisingizio cha kuibiwa kura wakishindwa,hivi hamjiulizi kama wizi wa kura upo kwanini cuf inairesa ccm pemba?au kwanini Ndesambura anaitesa kila wakati ccm moshi mjini?au kwanini Mzee Said Arfi makamu mwenyekiti wa cdm amekua kwa muda mrefu hata wakati slaa hajulikani amekua akiitesa ccm huko mpanda kwake?au zitto kwa nini anitesa ccm?Huwezi kuiba kura,huwa mnakua mmeshindwa tu,msidanganyike na watu kujaa kwenye mikutano yenu ya kampeni au hapa jf watu wengi kuonekana wanaipenda chadema,wengi sio wapiga kura!
Una uhakika mwanzisha mada ni mchaga?...na je ni mwanachama wa CDM?...