Pendekezo: Prof. Lipumba awe mgombea wa upinzani Igunga

Pendekezo: Prof. Lipumba awe mgombea wa upinzani Igunga

kwani kubenea si alitaka kugombea mafia 2010, hatutaki wakimbizi wa kisiasa : mara slaa mara nani sijui waacheni watu wa igunga wamchague kijana wao mwenye uchungu na jimbo lao!
 
Nakwambia anagombea. Jana alikuwa na kikao kirefu na Membe na Msekwa. CCM wanaona njia pekee ya kushinda jimbo la Igunga ni kumuweka Kubenea. Wamemhakikishia vikao vya chama vitampitisha. Lakini mkakati mzima unaonekana kutaka kumyamazisha yeye na gazeti lake. Wanaamini kuwa akijitosa katika mbio za ubunge Igunga, basi hataweza tena kuwachapa.
mkuu source pls
 
akienda chama cha magamba atajishushia uanaharakati wake, na mwisho wa cku ataishia kuwa shetan asie na kitengo maalum
 
Sasa akigombea via magamba na akashinda mwanahalisi si ndio tutaizika?
 
Mh Saidi S Kubenea Mbunge mteule wa Jimbo la Igunga CHADEMA
.

kubenea ili heshima iendelee kuwepo tafadhali usigombee ubunge ,mimi naona kwenye mwana Halisi unafanya vizuri zaidi kwa kutuelimisha kuhusu uozo wa ufisadi unaotokea nchi hii
 
Kubenea ni CCM mwadilifu, huko IGUNGA inabidi afikirie kwa makini. Akienda tu napoteza iman kabisa na siasa zetu.
 
Wadau kama ni kweli kubenea kugombea kupitia magamba sawa ni haki yake kikatiba lakini nijuavyo mimi kwa upiganaji anaoufanya hata nec wakimpitisha ujue lengo ni kulimaliza gazeti lake,magamba siku zote ni wanafki tu mtazamo wangu kwako kubenea kama taarifa hizi ni kweli think twice unaomaadui wengi sana hasa mafisadi na wote wako ccm ,hapo shasha.
 
Utapewa ubunge na nafasi ya kukuingiza hatiani kwa rushwa/ufisadi na hapo itakuwa mwisho wako, kumbuka yaliyompata Jerry Murro
 
Kama wameona anafaa, na yeye mwenyewe anaona anafaa kuwatetea wana Igunga kwa dhati yake na sio unafiki. Basi hata hukohuko magamba kazi atapiga.

Gazeti litafanya kazi yake kama gazeti just atamuajiri Mhariri mwingine machachari ili gazeti liwe na kasi ile ile. tatizo bado lipo kwenye katiba haikuweka mipaka ya uhuru wa mtu kugombea, otherwise asingefaa kwenda huko ila wana Igunga wenyewe wakae wapendekeze jina la muwakilishi wao. Kuna wanaoonesha kuwa na shaka na Kubenea ivi ni kweli wote walioko CDM wana fanya kazi tuliyotarajia sisi wananchi?

CDM msimdhanie vibaya Kubenea, acha akaungane na NAPE na January wafanye kazi ya ukweli kukirudishia hadhi chama.
 
Tatizo hapa tumeona kila mtu akiingia huko ccm ana tubadilika hasa akipewa kauwaziri 2meona Mwakyembe 2memuona sita,pia mtoto wa mkulima alianza vizuri leo hii ana subutu kusema kuwa hela za posho ni kidogo saana amekimbia ukulima.Siyo mtoto wa mkulima tena,sasa tena Kubenea TUNAJUA FIKA AKIWA KWENYE MAGAMBA HAWEZI KUTU TETEA TENA CC WANYONGE NA INAWEZEKANA MWANA HALISI LIKAWA KAMA UHURU.HIKI NDICHO KINA NIPA WASI WASI KWA KUBENEA 2MEONA TBC IKICHAKACHULIWA BAADA YA KUONDOLEWA TIDO IVYO MWANA HALISI LITA CHAKACHULIWA 2.KUBENEA 2ANGALIE WENGI
 
TUYUKU- Acha kupakazia mwenzako. Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Mtambo ule Kubenea ameuziwa na Mengi. Na mpaka sasa upo pale IPP Mikocheni, hajauondoa. Acheni kumchafua kwa mambo yasiyokuwa na kichwa wala miguu.
Mtambo ameuza mengi, amenunuliwa kubenea na RA??? Hapo vipi? Umeelewa sasa?
 
Tatizo kubwa la Igunga ni ukosefu wa huduma muhimu kama maji, elimu, miundo mbinu kama barabara imara. Hivyo ni muihimu sana akayatabua haya matatizo na kuyawekea mkakati wa kuyakabili.
 
Mtoa hoja,hujaeleza source.ww unasema 2 habar zlozokufukia,kutoka wapi?mbinguni?km nawe umeoteshwa useme.sio utuwekee habar za kwenye baraza za kahawa hapa.JF is for seriou people and serious business.TUACHE WAKATI UTUPE MAJIBU.
 
Igunga ni ngome ya CCM, na itabaki kuendelea kuwa hivyo.
 
Hilo linawezekana kwani nyie hamjui maana ya siasa kubenea anaweza vizuri sana siasa,Na mabadiriko na maendeleo ya wananchi wa Tanzania yatatokea ndani ya chama chetu cha kijani.Si vinginevyo,kwa hiyo kama ni kweli kuhusu kubenea basi atapita huko igunga.Hakuna chama zaidi ya cha kijani.Wengine wanachagiza ili kifanye vizuri hapo baadaye.
 
Back
Top Bottom