Pendekezo: Prof. Lipumba awe mgombea wa upinzani Igunga

CDM ilimshinikiza DK Slaa kuwa mgombea urais japo mwenyewe alikuwa hataki. Tumeona faida yake kuingiza wabunge wengi upinzani.

Kwa hivyo kwanini tusichukue nafasi ile kumshinikiza Mh Lipumba ili agombee ubunge Jimbo la Igunga:

  • Ni mzaliwa wa Tabora
  • Ni mwenyekiti wa Chama cha CUF ili kuongeza nguvu za upinzani akisaidiana na kina Mbowe, Lissu na wengine
  • Itaijenga Cuf kisiasa na kujenga Upinzani wenye nguvu bungeni
  • CDM haina nguvu sana kulinganisha na CUF kwa kuwa lipumba ndipo anapotoka.
Suala la Lipumba kuwa mzaliwa wa Tabora halimaanishi kuwa CUF ina nguvu mkoani tabora kuliko Chadema. Angalia matokeo ya uchaguzi uliopita katika Majimbo ya Nzega na Igunga kisha useme ni nani alikuwa na nguvu.

Lipumba na moja ya manabii wasiokubalika kwao na ndiyo maana CUF haijawahi kushinda hata jimbo moja mkoani Tabora tangu mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa, na kila mwaka imekuwa ikiporomoka kwa kasi ukilinganisha na CHADEMA ambayo imeanza kuwa na wafuasi wengi sana mkoani humo.
 
Kwa hiyo lini unataka CDM ianze kuwa na nguvu Tabora kama si sasa.

Mkuu,

Lipumba ni mtu anayekubalika Tabora ni kwao, pia ni msomi aliyebobea katika uchumi. Historia inaoonyesha hii nchi ikiwa na upinzani imara serikali inanyooka na kuwa na serikali imara ni pamoja na kuwa na bunge imara. Lipumba ni valuable asset kwasababu mosi ya usomi wake pili experience yake na tatu kukosekana kwa mtu makini anayefahamu masuala ya policy making nchini.

Lipumba kama ataachana na fikra za urais anaweza kwenda kugombea Igunga akaliimarisha bunge kuikosoa serikali inayotuingiza katika mkenge kila siku kwenye mikataba mibovu, sera mbovu na uwajibikaji mbovu. Pia kutachangia kuwepo kwa umoja kwa wapinzani baada ya tofauti zao tangu kumalizika kwa uchaguzi wa 2010.

CCM ni nyumba inayotaka kuvunjika au tembo anayetaka kuanguka bila ya upinzani imara CCM inaweza kurudi tena ulingoni na kuwa imara zaidi. Sasa hivi ndio wakati muafaka ya kuimalizia mbali CCM mwaka 2015 kiwe chama cha upinzani. Chadema, CUF, NCCR wakitoana ngeu CCM ndio itapata nguvu ya kuwamaliza kwa kudai wapinzani hawafai kupewa nchi ni watu wa fujo.
 
Nakubaliana na wewe lakini hapo kwenye red umechemka, CUF ina nguvu zaidi Tabora mjini
na vijijini lakini nje ya hapo (Nzega, Igunga, Urambo, BUkene) hakuna kitu
Hapo umenena ukweli mtupu. CUF haikubaliki Igunga ukilinganisha na CHADEMA
 
Rostam ana mtu wake pale. Alitupatia Rais wa NCHI hawezi kushindwa kutupatia mbunge pale Igunga.
 
Mkuu,

Lipumba ni mtu anayekubalika Tabora ni kwao, pia ni msomi aliyebobea katika uchumi. Historia inaoonyesha hii nchi ikiwa na upinzani imara serikali inanyooka na kuwa na serikali imara ni pamoja na kuwa na bunge imara. Lipumba ni valuable asset kwasababu mosi ya usomi wake pili experience yake na tatu kukosekana kwa mtu makini anayefahamu masuala ya policy making nchini.

Lipumba kama ataachana na fikra za urais anaweza kwenda kugombea Igunga akaliimarisha bunge kuikosoa serikali inayotuingiza katika mkenge kila siku kwenye mikataba mibovu, sera mbovu na uwajibikaji mbovu. Pia kutachangia kuwepo kwa umoja kwa wapinzani baada ya tofauti zao tangu kumalizika kwa uchaguzi wa 2010. CCM ni nyumba inayotaka kuvunjika au tembo anayetaka kuanguka bila ya upinzani imara CCM inaweza kurudi tena ulingoni na kuwa imara zaidi. Sasa hivi ndio wakati muafaka ya kuimalizia mbali CCM mwaka 2015 kiwe chama cha upinzani. Chadema, CUF, NCCR wakitoana ngeu CCM ndio itapata nguvu ya kuwamaliza kwa kudai wapinzani hawafai kupewa nchi ni watu wa fujo.
Tupe data kuwa Lipumba anakubalika nyumbani kwake, aligombea lini na nini

kama unatumia data za urais tupe maendeleo yake ukilinganisha na vyama vingine kama CDM.

Unasema anaweza kugombea kama ataachama na fikra za urais kumbe unajua ndoto zake kuwa si ubunge,

Halafu lini CUF wakaomba ushirikiano na CDM au ni kwa hili tu

je Rostam asingejiuzulu ushirikiano nao hakuna napenda kujua hili,

twende bungeni umesahau kambi rasmi na isiyo rasmi umesahau matamshi ya HR mbele ya Mbowe

umesahau uchaguzi wa Spika umesahau uchaguzi wa Meya kule Mwanza, zingatia hayo halafu ndipo muombe

ushirikiano kule Igunga.
 
Jamani ninaomba tuthamini kazi inayofanywa na vijana wenye uchungu na nchi hii. Tumeona kigugumizi na mvutano uliopo huko bungeni mpaka tunaona ya kuwa kumbe tunaweza kuikosoa serikali na ikathamini watanzania.

Hawa akina Lipumba tuachane nao tuangalie vijana mchapa kazi asiekuwa na subiri subiri. Lipumba ni kigeugeu kama kinyonga hafai. Wanaigunga wenyewe wanatakiwa wabadilike waachane na hela za kupewa wadhamini maendeleo na mtu atakae waletea maendeleo kama ajira nk.

Wasituletee mtu asie na kitanda nyumbani kwake akachape usingizi kwenye viti vya bunge.
 
CCM matumbo motto nina uhakika watatumia mbinu zote ili tendwa asitangaze uchaguzi usitangazwe mapema.. Sasa hivi imekula wao wakiingia kwenye jimbo lolote la uchaguzi lazima ile kwao.
 
Mbowe na Mrema waligombea Urais walivyoshindwa wakagombea Ubunge na kupata, kwahiyo inawezekana kwa Prof. Lipumba naye kugombea ubunge wa Igunga na kupata.
 
CDM ilimshinikiza DK Slaa kuwa mgombea urais japo mwenyewe alikuwa hataki. Tumeona faida yake kuingiza wabunge wengi upinzani.

Kwa hivyo kwanini tusichukue nafasi ile kumshinikiza Mh Lipumba ili agombee ubunge Jimbo la Igunga:

  • Ni mzaliwa wa Tabora
  • Ni mwenyekiti wa Chama cha CUF ili kuongeza nguvu za upinzani akisaidiana na kina Mbowe, Lissu na wengine
  • Itaijenga Cuf kisiasa na kujenga Upinzani wenye nguvu bungeni
  • CDM haina nguvu sana kulinganisha na CUF kwa kuwa lipumba ndipo anapotoka.

Good suggestion , lakini Lipumba mbona muda mwingine huwa analeta mashaka ni nia thabiti ya upinzani. Sasa wao na CCM ni ndugu, ataleta nguvu kwenye upinzani kweli!!!!!!???????. Urafiki wa mashaka na LIPUMBA
 
Sidhani kama CCM watasimamisha mgombea, watashirikiana na wenzao CUF wasimamishe mpinzani wa CHADEMA!
 
CDM ilimshinikiza DK Slaa kuwa mgombea urais japo mwenyewe alikuwa hataki. Tumeona faida yake kuingiza wabunge wengi upinzani.

Kwa hivyo kwanini tusichukue nafasi ile kumshinikiza Mh Lipumba ili agombee ubunge Jimbo la Igunga:

  • Ni mzaliwa wa Tabora
  • Ni mwenyekiti wa Chama cha CUF ili kuongeza nguvu za upinzani akisaidiana na kina Mbowe, Lissu na wengine
  • Itaijenga Cuf kisiasa na kujenga Upinzani wenye nguvu bungeni
  • CDM haina nguvu sana kulinganisha na CUF kwa kuwa lipumba ndipo anapotoka.

You have a point! Lakini hapana
 
wakati naunga mkono prof na mchumi mahili katika karne yetu hii aichukue Igunga ili awe na influence kubwa katika kuujenga uchumi unaoendelea kuporomoshwa na wana magamba ningevisihi vyama vya upinzani viungane na viache vita ya panzi kwani magamba watalinyanyua jimbo hilo kiulaini sana!

Igunga hivi sasa inahitaji mtu makini sana kuendeleza maendeleo yaliyofikiwa au la mtu ajae anawezajikuta anapwaya sana.
 
Back
Top Bottom